feyzal
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 7,683
- 15,128
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Karibu forum za kwetu huku: MMORPG.com: Free MMO and MMORPG Games Reviews & News
Vipi na elimu ya alietunga hiyo sheria pamoja na aliesaini?yule dada usomi wake bado haujamsaidia, wengi wanadhani elimu walizonazo ni za kwao pekee yao kumbe si hivyo.
Kama unapata shida kuona kosa lake ngoja nikupe mfano huu: Umempa mkandarasi mkataba wa kujenga nyumba. Baadae ukakabidhiwa nyumba yako na kuichukua. Baada ya siku mbili nyumba ikapasuka ufa! Je mkandarasi hatawajibika kwa sababu tu wewe ulikubali kuipokea ile nyumba?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka.
Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
> Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums
Irene Charles Isaka, Director General, Social Security Regulatory Authority - JamiiForums
.Yeye ndo alimtuma usishangae anampa shavu zaidi ya alilonalo sasa hivi
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana,kaolewa huyo ni mke wa mtuNasikia eti ni mjane, itakuwa alikuwa chakula ya wakubwa, na mpemba Dau labda alimpigia chapuo kwa JK ili ateuliwe.
Mazee sioni mantiki kwenye hoja yako.Rais aliacha maji yafuate mkondo na baade akaingilia. Rais hawezi kuwa kila mahali akifanya kila kitu. Hufanyia kazi yale anayoletewa na yale yenye uharaka! BTW mimi nimefurahi jinsi alivyojipa muda kushughulikia kwani imekuwa ni somo tosha kwa wengi.
Mwanasiasa siku zote hata awe PHD holder huwa hana tofauti na mtu aliyeishia darasa la pili B, na huwa wanafanya hivi kwa kulinda maslahi yao binafsi na sio kwa maslahi ya wengi, lakini mtaalamu mwenye PHD ukafanya ujuha kwa kulinda maslahi ya wanasiasa aisee huo ni u.pumbavu wa hali ya juuVipi na elimu ya alietunga hiyo sheria pamoja na aliesaini?
Kwi! Kwi! Kwi!Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka.
Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
> Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums
Irene Charles Isaka, Director General, Social Security Regulatory Authority - JamiiForums
Pongeza pongeza Fc kumbukeni mlivyotetea hiyo 25% kuwa ni uzalendo leo imetenguliwa mmefuata kulekule wakina zitto walipopiganiaKama alivyosema, 'tutamuelewa tu'. Hongera sana rais JPM.View attachment 979843
Sent using Jamii Forums mobile app
Nchi hii imejaa wajinga kweli kweli!Magufuli huwa hapendi ujinga na watu kufanya kazi kwa mazoea. kauli ya hapa kazi tu inaendelea kuwa wazi na lazima ieleweke Magufuli anaposema hapa kazi anamaanisha nini anasema.
ilikuwa ni bora kujiuzulu hiyo nafasi kuliko haya yanayomkuta leo.
Nyie watu mkoje? Hivi hili swali si lilitetewa bungeni? Yaani sijui hamna akili ama huwa mnajitoa akili. Irene kwani alikuwa anapanga mwenyewe bila ya kupitisha kwa wenye mamlaka ya kutunga kanuni?
Kikokotoo hutengenezwa na Waziri mwenye dhamana, mkurugenzi wa SSRA hahusiki!
Hivi akili yako inakubali kwamba mkuu wa nchi alikuwa haelewi kabisa kinachoendelea kuhusu kikokotoo na amekuja kuelewa kwenye kikao cha leo?Hakuna siasa za maji taka kilichomponza Irene ni kiherehere chake cha kila mara kujitia kudadavuwa kikokotoo ni kukitetea, na elewa kati ya waziri na Irene mtaalam wa mahaesabu na mshawishi mkuu ktk mipango yote ya kutengeneza formula ya calculation ni Irene na ndio sababu alikuwa akitetea mno katika mahojiano,
Magufuli yuko sawa,
Huwezi kupewa unga maji mwiko halafu usonge ugali mbichi kisha ulalamike eti alaumiwe na alie leta maji mwiko na sifuria, utaonekana juha,
Sent using Jamii Forums mobile app
This is a harsh punishment for her. Pigo kwa young ladies who were looking up to her.
Lady leaders, be humble and dont stop learning to lead, communicate as a leaders, learn surroundings and situations, seek opinion and advise. Ask for help.
My self I am not a leader but I've never stopped to learn leading children and house helpers.Contradiction nhaa!