Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amejikuta akitokwa machozi hadharani baada ya shindwa kujizuia wakati akielezea mazungumzo yake ya mwisho na Rais mstaafu awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam
Hilo limejitokeza leo Jumanne tarehe 28 Julai 2020 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kulipokuwa kunafanyika shughuli ya kuaga Kitaifa mwili wa Mkapa aliyefariki dunia Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 saa 3:30 usiku kwa mshituko wa moyo.
Akihutubia taifa katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya waombolezaji uwanjani hapo, Rais Magufuli amesema “hakuna mtu anayeweza kumwelezea vizuri Mzee Mkapa zaidi alivyojieleza mwenyewe vizuri kwenye kitabu chake cha My Life, My Purpose.” (Maisha Yangu, Kusudio Langu).
Katika hotuba yake, Rais Magufuli ambaye alikuwa mara kadhaa anatulia, akilengwa lengwa na machozi akisema kifo cha Mkapa ni pigo kwani ilizoeleka katika matukio makubwa anaungana na marais wenzake wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete ‘lakini leo hapa hayupo.”
“Mzee Mkapa alinilea kama mtoto wake, alikuwa ni shujaa wangu, alinionyesha upendo,
“Hata kwenye shida Mzee Mkapa hakuniacha kamwe, hakutaka nianguke, alinilea kama mtoto wake. Wakati wote alikuwa ananionyesha upendo, hivyo basi kuondoka kwake ni pigo kubwa kwangu, nimepoteza mtu muhimu kwangu.”
“Saa nyingine machozi yanakuja tu msinishangae sana, hata Mzee Kikwete nilimuona juzi anadondosha machozi tena Kikwete ni Kanali ila alitoa chozi kwahiyo msinishangae mimi,” amesema Rais Magufuli
“Nilipata fursa ya kuongea na Mzee Mkapa kwa simu akiwa hospitalini saa chache kabla hajafariki, nakumbuka aliniambia John usiwe na wasiwasi naendelea vizuri sikujua kwamba maneno yale yalikuwa ya kuniaga. kazi ameikamilisha,” amesema Rais Magufuli huku akitulia na kutoa kitambaa kufuta machozi.