Rais Magufuli atokwa na Chozi la huzuni: Mzee Mkapa alinilea kama mtoto wake, alikuwa ni shujaa wangu, alinionyesha upendo

Rais Magufuli atokwa na Chozi la huzuni: Mzee Mkapa alinilea kama mtoto wake, alikuwa ni shujaa wangu, alinionyesha upendo

Kwa mujibu wa sifa zilizotolewa katika kipindi hiki ni wazi kuwa Mkapa alipokea taifa toka kwa Mzee Mwinyi likiwa KOPO TUPU. Sasa sijui Mzee Mwinyi sifa zake zitakuwa zipi akifa.
Siyo kweli na yeye alikuwa na mazuri yake mengi tu kumbuka alijulikana kama mzee ruksa aliwapa watu uhuru wa kufanya biashara baada ya kupokea taifa likiwa kwenye hali mbaya zaidi ya uchumi baada ya miaka michache nyuma kutoka kwenye vita na kuanza mapambano ya ulanguzi na uhujumu uchumi
 
Haya maneno alitakiwa ayaingee wakati Mkapa yuko hai. Maana mzee Mkapa angeona fahari kwamba kuna kuna fadhila ana rudishiwa.

Lakini kumsifu marehemu haileti faida zaidi ya kuongea.

Tulizowea kusikia Mh JPM akituambia watangulizi wake hawakufanya kitu. Na nchi imeliwa sana. Kumbe sio kweli? Leo ana tuambia Mzee Mkapa ndie royal model wake. Ndie mwanzilishi wa karibu vitu vyote anavyo endeleza. Tushike lipi? /RIP BABA Mkapa.
Jpm anachokiongea leo, usishangae kesho akiongea kinyume chake
 
Wakuu naomba niwaulize kitu.
Wakati nasikiliza hiki kipande machozi yamenitoka. Ni kila mmoja wetu yamemtokaaa au ni mimi tu na watu wachache. Nikimaanisha kweli kunaambae ataangalia hiki kipande asitokwe na machozi kabisa?

Je yule ambaye hayajatoka machozi kwamba yuko stronger than sisi tuliotokwa machozi??!!
Hem naombeni michango yenu ktk hili maana dah basi binadam tutakua tunatofautiana sana tena.
Haitakusaidia kwa chochote
 
[emoji16][emoji16][emoji16]
Ila wote tu mzee mkapa na mzee kikwete wamembeba Sana jamaa[emoji28][emoji28]
Naona mzee Kikwete kwa Magufuli sio saaana. Ni kwa vile tu alimtangulia, ila hawana ile chemistry kama aliyokuwa nayo na Mkapa.
 
Kanali anakuwa a humble and democratic man.

Mwalimu anakuwa sadist & a petty dictator.

that happens in the United Republic of Tanzania only.
Exposure nayo muhimu, mmoja alisukumizwa tu kwenye hiyo position
Mjeshi alikuwa groomed from the bottom
 
😜😜😜

Sasa kama mkapa ndio alikuweka hapo ulipo, yaani ulivyokuwa mtu wa kubebwa bebwa, without merit, na kwa sababu umetuambia wazi watanzania kwamba hapo ulipo sio kwa kura za wananchi, sasa Oktoba unaondoka.
 
Na sifa za Kikwete sijui zitakuwa zipi
Ina maana wasanii na vijana waliokamata hela chafu na madili ya hela ndefu ushavisahau vyote hivyo. Kauli mbiu tu ndio itawakilisha yote hayo,

"Maisha bora kwa kila mtanzania"

Ila pia vifo vya wasanii kwa ngada pamoja na mikwara ya hapa na pale baina ya raia, "Unanijua mie ni nani!"
Ni miongoni mwa sifa za awamu ya 4!
 
Unajitoa ufahamu kama hujaenda shule.
Unajua process za kufikia huo mchakato? Mchakato wake unahusisha vikundi, taasisi ngapi? Kwa muda gani? Uchaguzi utakuwa lini toka Leo?
You need to use brain in a sense.
Kama kweli alikuwa ni shujaa wake amuenzi kwa kulifanyia kazi ombi la Mkapa ili Tume Huru ipatikane kabla ya uchaguzi wa 2020.
 
Ina maana wasanii na vijana waliokamata hela chafu na madili ya hela ndefu ushavisahau vyote hivyo. Kauli mbiu tu ndio itawakilisha yote hayo,

"Maisha bora kwa kila mtanzania"

Ila pia vifo vya wasanii kwa ngada pamoja na mikwara ya hapa na pale baina ya raia, "Unanijua mie ni nani!"
Ni miongoni mwa sifa za awamu ya 4!
Kama umezisikia sifa anazopewa Mkapa, ni kama vile Mzee Mwinyi alikuwa pazia tu, hakuna chochote alichofanya.
 
Mzee Mkapa alianzisha taasisi ni ngumu sana kukwepa kumpa hio sifa.
Hilo lipo wazi
Apewe sifa anazostahili
Ila tusivuke mipaka
Tukajenga image that serikali iliyopita kabla yake haikufanya chochote.
Hata Magufuli aliwahi kuzikebehi serikali zilizopita ikafikia hatua mzee mkapa akasema, serikali ya sasa isijisifu sana kiasi cha kutaka kuonekana waliopita wote walikuwa useless.
 
Huyo mtu wanaemlilia hana maana yoyote kaua watu acha na yeye afe tu tena amechelewa mungu angemchukua mapema zaidi ingekuwa vizuri
 
Walipanda kwa kutumia ungo mmoja...Leo kabakia mwenyewe.....lazima chozi litoke..

Mwinyi na Kikwete ni watu wa pwani hawa ; waungwana hawataki harufu damu kabisa!!

Kazi inaanzia hapo
 
Back
Top Bottom