Rais Magufuli atokwa na Chozi la huzuni: Mzee Mkapa alinilea kama mtoto wake, alikuwa ni shujaa wangu, alinionyesha upendo

Rais Magufuli atokwa na Chozi la huzuni: Mzee Mkapa alinilea kama mtoto wake, alikuwa ni shujaa wangu, alinionyesha upendo

Mbona hili ni rahisi sana mkuu 'Tripo9.'
Kulia au kutolia kunategemea mawazo yako wakati unayasikia hayo maneno na jinsi huyo anayeyasikia maneno anavyomchukulia huyo aliyeyatoa maneno.

Kama msikilizaji hamwamini anayeyasema maneno, nini hasa kitamfanya alie?

Kama msikilizaji alishafanyiwa jambo la kikatili na anayetoa maneno ya kuliza, hayo maneno peke yake ndiyo yamfanye atokwe machozi bila ya kumfikiria mtu anayeyasema hayo maneno?

Kuna pia sehemu ya marehemu katika hili. Kama kulikuwepo na jambo zito sana ambalo msikilizaji hakuwa anakubaliana na marehemu, hiyo nayo inaweza kuwa sababu mhimu ya kutoamsha hisia za kutoa chozi juu yake. Kuna mambo mengine chungu nzima.
Hapa nimekuelewa volivyo kabisa
Ni kweli usemalo
 
Waliokufa aliwafufua?
Mkapa kama binadamu yoyote wa kawaida, alichoweza ni kuomba msamaha. Ni jambo jema la kuigwa.

Suala la kufufua aliowaua lipo nje ya uwezo wake.
Tumuombee mapumziko mema.
 
Wakati wa hafla ya kitaifa ya kumuaga Mwl Julius Nyerere pale Uwanja wa Taifa, Rais Mkapa alishauriwa kwamba ajitahidi kwa namna yoyote ile
asilie wala kutoa machozi hadharani. Na ndivyo alivyofanya. Pamoja na yote ambayo Mwl alimfanyia Mkapa, ikiwemo kumfanya awe Rais, Mkapa alijitahidi. Je JPM hakushauriwa kuhusu hili?

Atupe Tume Huru kama alivyotaka Mzee Mkapa.....!!
 
Kwa mujibu wa sifa zilizotolewa katika kipindi hiki ni wazi kuwa Mkapa alipokea taifa toka kwa Mzee Mwinyi likiwa KOPO TUPU. Sasa sijui Mzee Mwinyi sifa zake zitakuwa zipi akifa.
Kila mtu na nafasi yake, marais wetu wote wametufaa kwa namna zao
 
Lisu au Membe watasubiri sana,
Kutoboa uchaguzi wa urais hapa bongo lazima uwe na support ya jeshi, kura peke yake hazipewi kipaumbele, kinyume na hapo ni kujidanganya tu.
HATA AL BASHIRI WA SUDANI ALIKUWA NA JESHI. BINADAMU ANA MIPANGO YAKE NA MUNGU ANA MIPANGO YAKE.GADAFFI NAE ALIKUWA NA MIPANGO YA MIAKA MIWILI AU KUMI IJAYO LAKINI HAKUFIKA.NAE ALIKUWA NA JESHI. HATA ZANU PF YA ZIMBABWE INALAZIMISHA KUBAKIA MADARAKANI WANAIBA KURA LAKINI NCHI INAZIDI KUFA. UMEME UNAWAKA MASAA MANNE KWA SIKU NCHI INAZIDI KUFA.DOCTOR ANAPOKEA MSHSHARA DORA 70,HAO WANAJESHI NA POLISI HOI MPAKA WANAWEKA VIRAKA NGUO ZA KAZINI. HIKI CHAMA CHAKA KIKISHINDWA UCHAGUZI KIONDOKE KISITUHARIBIE NCHI
 
Wananchi wa Sudani waliingia barabarani kudai mabadiliko, huwezi fananisha na watz wanaodai mabadiliko kwenye keyboard.
 
Salamaa

NAOMBA UZI HUU usiunganishwe Wala kufutwa, maana hili ni jikwaa huru..

Kuna nchi ambayo ilipatwa msiba kwa kuondokewa na Rais wao mstaafu, natukaona bila kujali itikadi zao za kisiasa wananchi na viongoz waliungana kuomboleza na kuonesha ni WAMOJA; MPAKA VIONGOZ KADHAA WALIMWAGA MACHOZI HADHARANI.

Sasa basii baada ya mazishi, walewale ambao walikuwa WAMOJA katika msiba huo, inatokea kiongoz anawabagua wananchi eti kisa itikadi za kisiasa. Je, huu sio UNAFIKI?

Ushauri,,
Kumbukeni enyi wanasiasa wanafiki wa kiafrika, dunia hii ni mapito, na hamna mkataba na MUNGU, akisema muda umefika haangalii wewe ni nani, jaribuni kutenda yaliyo mema kwa wananchi wenu bila kubagua kisa dini, rangi, kabila Wala CHAMA CHA SIASA .... Endapo mtaendelea na ubaguzi na UNAFIKI wa kuwabagua wananchi kwa itikadi za kisiasa, hata Ile kauli mbiu yenu ya kinafiki ..." MAENDELEO HAYANA VYAMA" tutaibadili na kuwa

"MAENDELEO YANA ANGALIA VYAMA"

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom