Rais Magufuli awachana Kilwa kwa kumchagua mpinzani Bwege. Awataka kutofanya makosa tena uchaguzi ujao

Njia nyingine hazioni labda ana uhasama na Bwana Bwege.Bado angeweza kumwita na kumsaidia kwa hilo.Mara nyingi Raisi Magufuli amekuwa akisema maendeleo hayana vyama.
Ni Musukuma Kiswahili kama kilivyo Kingereza kinampita mbali kwa hiyo anaposema maendeleo hayana vyama huwa ana maana yana Chama cha CCM. Mwenzenu huwa najiuliza kama alikuwa mwalimu, mbona mwanafunzi hata mmoja wa darasa la nne hajajitokeza kuonyesha pride ya kufundishwa na future President, je wanatahayari kwa kuwa wanafunzi wake au wanaona aibu kwasababu hawakufuzu kila somo lake ndo maana hawakuendelea na shule waliishia kuchunga mbuzi. Hali ya kawaidà ni sifa kuwahi kuwa mwanafunzi wa aliyekuja kuwa Mbunge, Waziri au Rais!
 
Unaweza kumtoa mshamba kijijini ukamleta mjini, lakini huwezi kuutoa ushamba wake.
SASA panakua patamu/pachungu pale huyo mshamba anapofika mjini na kuwakimbiza wajanja wa mjini mchakamchaka mpaka wengine wanahama mji.
 
ILANI ya ccm inatekelezwa na wana CCM,,, ukimchagua mbunge wa chama cha Jahazi Asilia au Tadea basi atatekeleza ILANI ya chama chake
Pesa zote za miradi ziko chini ya mkurugenzi, huyo mkurugenzi si yeye ndiye anayewateua, huyu jamaa ni **
 
Ndio malipo ya miaka mingi sana kwa watu wa kusini kuikumbatia CCM.
Wanasoma Historia tu kuwa Babu zao walipigana Vita vya Majimaji wakati huo hapakua na CCM wala CUF.
Watu wa kusini ndio watu pekee waliopigana vita inayosomwa Duniani kote vita ya Maji maji.
Kifupi ni kwamba Mabeberu wa Kikoloni baada ya kukimbia kusini walisusia kupeleka maendeleo maeneo hayo. Nafikiri kuna agenda ya siri ya Mabeberu kuwanyima watu wa maeneo Fulani maendeleo. Huo ni mwendelezo tu.

Jambo la msingi ni ama kuungana na Mabeberu ili upate upendeleo wa maendeleo au ni kuendelea kuwakataa Mabeberu na kujipanga wenyewe kuleta maendeleo.
Dhulma haitakwisha duniani endapo bado kuna watu wananufaika na kuneemeka sana na dhulma.
Wapo wapi wale mashekhe waliosoma Duwa karne hiyo ya 15 na kuwabadili wanajeshi wa Kireno na merikebu zao za kivita kuwa Miamba ? Mambo mengine yanahitaji Maombi na kumwachia Mungu.
Maendeleo hayahitaji kufanyika kwa misingi ya vyama kwani walipa Kodi wa kubwa ni wale wasio na vyama na waliopo madarakani wengi kazi yao ni kunufaika na Kodi tu na mamishahara makubwa huku wapinzani wakiumia na kulipa Kodi na wengine kupigwa faini kama wale walevi wakiongozwa na Mlevi Mkuu Mbowe walivyofanyiwa.

Kuna maeneo Mengi tu Tanzania hayana Stand wala Barabara.
Mkoa wa Tanga unaongozwa na CCM kwa muda mrefu sana lakini Standa ukiacha ile ya Mkoa nyingine ipo Korogwe tu. Wilaya nyingine zote hakuna kitu na ushuru Mabeberu wanachukua kama kawaida.
Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ambayo haijawahi kuwa na Upinzani kabisa na haitakuja kuwa na Upinzani ni Mwanga lakini ndiyo Wilaya isiyo na stendi Mkoa mzima.

CCM ina bahati moja ya kuwaongoza wananchi wengi wenye Elimu ndogo.
Ila kiuhalisia CCM ilitakiwa ipumzishwe kidogo ili wale waliozoea kuteuliwa tu na kula Kodi za umma wa Watanzania Wote bila kujali kuwa Kodi imelipwa na wasio na vyama pia
Wajifunze kuwa na Ubinadamu na kuwatendea watu wote haki alimradi hawajavunja Sheria.
Hili la kuwabagua watu kwa misingi ya vyama ni jambo lisilo na utu mana wamemchagua kisheria na kikatiba na sio kuvunja sheria.
Mungu anawaona.
Watajenga mamiradi yao lakini hawatayafurahia mana hawana roho za amani mioyoni mwao.

CCM wapendeni watu na kuwaletea wote maendeleo bila kujali dini zao,makabila yao,vyama vyao na rangi zao ndipo mtakapofurahia Kodi zao mnazokula kupitia mishahara minono mnayolipwa na madaraka makubwa mnayoyapata .Hii ndiyo haki.
 
Halafu anasimama madhahabuni anasema tuliombee taifa, taifa huwa haliendeshwi namna hiyo ni afadhali tungeondoa vyama vingi ikajulikana moja
Mtamuelewa Shehe yule na ule ujumbe wake wa kudai haki kwa wote.

Ubaguzi ulifanywa na wakoloni Wazungu lakini bado waafrika wenzetu kupitia vyama vilivyokopi na kupesti Ukoloni na serikali zake vinaendelea kufanya yale yale kwa kutegemea kuwaona wananchi maskini wakiwapigia magoti kama miungu watu.

Hata hivyo wapinzani bado hawana Sera za Kizalendo mana wamekua wakipinga maendeleo na kususa kuwawakilisha wananchi bungeni kwa kutoka nje.
Wapinzani wanaipa CCM sababu ya kuwadanganya wananchi.
 
Haijawahi tokea kichaa ka huyu Tanzania, zee ovyo sana hili. Libinafsi, hasira za kijinga, kukurupuka na decisions kila wakati alafu mnafiki balaa.
Kesho anarudi utasikia mniombee, anakusanya na vijisadaka wajinga wanamkubali balaa, mtakufa maskini mkiendelea kucheza na drama za jiwe
 
Serikali inakusanya kodi kwa watanzania wote.

Hii kauli ya kuwapelekea wabunge wa ccm makusanyo ya walipakodi halali nchi nzima nikudharau Utukufu na ukuu wa Mungu kutupa mitazamo na utashi usio lingana.

Mungu hadhihakiwi
Tatizo ni moja kwa Wapinzani .
Wengi wanafikiri akili zao zinatosha kupata madaraka ya kuongoza Dola.Eti nguvu ya umma!!
Umma unamilikiwa na Mungu mwenyewe.
Lakini pia shetani ana watu wanaomuunga mkono ndio maana kura tu za maoni ushirikina ni mwingi sana na rushwa.

Walioko madarakani wanajua ndio maana wanajiweka karibu na ibada za aina zote. Lengo ni kuuteka umma na miungu yao.

Tofauti na wapinzani wanaoongozwa na MTU kama Mbowe anayekesha baa akiwaza konyagi na wanawake huku kichwani akiwa hajui hata Aya moja ya Quran wala Biblia wala Ubudha wala Ushirikina.
Ni lazima siasa na harakati za kuwaongoza na kuwatawala watu ziendane na imani zilizopo duniani.
Ndio maana Tangu ameondoka Padri Slaa Chadema imeyumba sana. Wamebaki wahuni wahuni tu japo nimemuona Lisu amerejea akiwa amejengeka zaidi kiimani. Naiona kesho njema ya Lisu mana ametambua kuwa dunia inaongozwa pia kiroho.

Zito Kabwe na Maalim Seif sina shaka nao. Na zaidi wao wana Shekhe Ponda anayeijua vizuri dini ya Mwenyezi Mungu.
Hakuna haki kama hakuna hofu ya Mungu vinginevyo itakua ni amri juu ya amri na sheria juu ya sheria zitakazowekwa na watawala huku wao wenyewe wakiwa hawazifuati.

Chadema kilipata umaarufu mpaka kikawa kinawapa nafasi za ubunge na udiwani Wachungaji kama akina Msigwa na Lema na Nasari mtoto wa Mchungaji lakini baada ya kupata Ubunge wamekengeuka na kumuiga na kutekwa na Mlevi, muongo na fisadi mkuu , Mgambo Mbowe.
 
Kwanini huyo bwana Seleman Bungara aliitwa ''Bwege''?
 
Hata marehemu kuna watu aliwaita malofa, malofa wapo marehemu kawa marehemu
Mungu ndiye mkuu wa kila kitu hilo halina ubishi na anayebisha anyooshe kidole au hata ajaribu kujikuna kichwa tumuone.
Mana yule mgombea wa malofa alisemwa kuwa hatamaliza hata kampeni lakini cha ajabu Neno linalotoka kinywani mwa Mungu lipo kwake.
Biblia inasema ,"Mtu hataishi kwa Mkate tu Bali kwa kila Neno litokalo Kinywani mwa Mungu."
 
Du kwahiyo ili tupate maendeleo ni lazima tuchague wabunge wa CCM.
Kibamba ambako ndio makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo hakuna lami zaidi ya ile ya barabara ya Morogoro huku Makumbusho, Sinza lami zinakwenda mpaka vyumbani na jenzi mbalimbali zinaendelea.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] paragraph ya mwisho mie hoi, afu umetoa kwa hisia sana lol
 
Utadhani majimbo yanayoongozwa na CCM yana maendeleo. Si kweli hata kidogo
 
Tangu Uhuru nchi inatawaliwa na CCM -the funny thing
Naa Bado watanzania ni masikini wa kutupwa

The opposite is very true
 
Alafu ndo iloilo linasemaga maendeleao hayana chama
Ungekuwa wewe ungechukua hatua gani wakati unakuwa bubu viongozi wako wanapofanya maovu, au unaishi kwa ule msemo wa "nani atamfunga kengele paka shingoni!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…