Wakuu, MAENDELEO HAYANA CHAMA
Rais Magufuli akiwa safarini kutoka Mtwara, ameombwa na mwanakijiji Jimbo la Kilwa kwamba hawana Stendi ya Magari hivyo anaomba wajengewe. Rais Magufuli amejibu kwamba siku nyingine waangalie wawakilishi wanaowachagua ili waweze kufanya vile yeye anavyowaagiza. Mbunge wa jimbo hili aliyemaliza muda wake ni Seleman Bungara aka Bwege Mzee wa ''Umesikia Wapi'' ambaye alikuwa anatokea chama cha wananchi
CUF Habari
Rais amezidi kusema kwamba miradi kama hiyo ni ya wabunge na Madiwani ndiyo wanapaswa kuisimamia hivyo kuwataka wabaki na Bwege wao
Rais Magufuli amesema haya...
Nilikuja hapa nikasema nichagulieni watu nitakaokuwa nawaagiza wanafanya ninayoyataka mkasema hapana, Mkamchagua Bwege basi shauri yenu na bwege wenu mwambie awatengenezee stendi
Kazi ya Stendi ni ya madiwani, wabunge. Ukikosea kuchagua, nafuu ukosee kuoa au kuolewa. Ukikosea kuchagua ni tatizo kubwa.
Na hili ndugu zangu niwaombe, muwe waangalifu katika kuchagua. Mchague watu ambao watakuwa kwa ajili ya watu masikini.
Tunatuma hapa fedha za road fund, tunatuma fedha hapa za halmashauri, zimeshindwa kweli kujenga stendi?
Lakini kwa sababu mnanichagulia, wao wenyewe mastendi unategemea mimi mwenyewe nifanyeje? Huo ndiyo ukweli sitaki kuwaficha mlikosea kuchagua.
Sasa katika uchaguzi wa mwaka huu mjipange vizuri, mchague mtu ambaye mtakuwa mmempa stendi akikataa nitamfukuza hata kwenye chama. Lakini leo nitamfukuza huyo aliyeko kwenye chama sijui hata yuko kwenye chama gani, nitamchukulia hatua gani?
Chama cha
ACT Wazalendo kimelaani vikali na kuwahamasisha wananchi kukemea vikali kauli hizi za kibaguzi. Wamedai kuwa kitendo cha kuhamasisha ubaguzi na kuingilia mamlaka ya wananchi katika kuchagua mtu wamtakaye kinakiuka misingi ya Katiba yetu.
Ndio malipo ya miaka mingi sana kwa watu wa kusini kuikumbatia CCM.
Wanasoma Historia tu kuwa Babu zao walipigana Vita vya Majimaji wakati huo hapakua na CCM wala CUF.
Watu wa kusini ndio watu pekee waliopigana vita inayosomwa Duniani kote vita ya Maji maji.
Kifupi ni kwamba Mabeberu wa Kikoloni baada ya kukimbia kusini walisusia kupeleka maendeleo maeneo hayo. Nafikiri kuna agenda ya siri ya Mabeberu kuwanyima watu wa maeneo Fulani maendeleo. Huo ni mwendelezo tu.
Jambo la msingi ni ama kuungana na Mabeberu ili upate upendeleo wa maendeleo au ni kuendelea kuwakataa Mabeberu na kujipanga wenyewe kuleta maendeleo.
Dhulma haitakwisha duniani endapo bado kuna watu wananufaika na kuneemeka sana na dhulma.
Wapo wapi wale mashekhe waliosoma Duwa karne hiyo ya 15 na kuwabadili wanajeshi wa Kireno na merikebu zao za kivita kuwa Miamba ? Mambo mengine yanahitaji Maombi na kumwachia Mungu.
Maendeleo hayahitaji kufanyika kwa misingi ya vyama kwani walipa Kodi wa kubwa ni wale wasio na vyama na waliopo madarakani wengi kazi yao ni kunufaika na Kodi tu na mamishahara makubwa huku wapinzani wakiumia na kulipa Kodi na wengine kupigwa faini kama wale walevi wakiongozwa na Mlevi Mkuu Mbowe walivyofanyiwa.
Kuna maeneo Mengi tu Tanzania hayana Stand wala Barabara.
Mkoa wa Tanga unaongozwa na CCM kwa muda mrefu sana lakini Standa ukiacha ile ya Mkoa nyingine ipo Korogwe tu. Wilaya nyingine zote hakuna kitu na ushuru Mabeberu wanachukua kama kawaida.
Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ambayo haijawahi kuwa na Upinzani kabisa na haitakuja kuwa na Upinzani ni Mwanga lakini ndiyo Wilaya isiyo na stendi Mkoa mzima.
CCM ina bahati moja ya kuwaongoza wananchi wengi wenye Elimu ndogo.
Ila kiuhalisia CCM ilitakiwa ipumzishwe kidogo ili wale waliozoea kuteuliwa tu na kula Kodi za umma wa Watanzania Wote bila kujali kuwa Kodi imelipwa na wasio na vyama pia
Wajifunze kuwa na Ubinadamu na kuwatendea watu wote haki alimradi hawajavunja Sheria.
Hili la kuwabagua watu kwa misingi ya vyama ni jambo lisilo na utu mana wamemchagua kisheria na kikatiba na sio kuvunja sheria.
Mungu anawaona.
Watajenga mamiradi yao lakini hawatayafurahia mana hawana roho za amani mioyoni mwao.
CCM wapendeni watu na kuwaletea wote maendeleo bila kujali dini zao,makabila yao,vyama vyao na rangi zao ndipo mtakapofurahia Kodi zao mnazokula kupitia mishahara minono mnayolipwa na madaraka makubwa mnayoyapata .Hii ndiyo haki.