Rais Magufuli awachana Kilwa kwa kumchagua mpinzani Bwege. Awataka kutofanya makosa tena uchaguzi ujao

Huyo ndiye JPM halisi wengine wote fotokopi. Hati Maendeleo hayana vyama-wakati mtu anaonyesha ubaguzi wazi wazi. Tumuache yeye na Joni Mchungaji na Mzee Mgaya wanataka kutuamunisha kuwa maendeleo hayana vyama.
Huu ni ubaguzi. Kazi ya mbunge sio kupeleka maendeleo jimboni bali kazi yake ni kuwasemea wananchi. Maendeleo hupelekwa na serikali ilyopo madarakani.
Maana hata kama jimbo ni la upinzani bado wana lipa kodi.
Kuna mahali Mh Rais hukosea maana juna maeneo wabunge ni wa Ccm lakini wakusha pata kura hawaonekani majimboni hadi uchaguzi ukaribie.
Wengine wa Ccm ndio hao majangili. Lakini Mh Rais hawazungumzii. Hii ni aibu na anatakiwa awaombe radhi Wapinzani
 
Uchaguzi ujao hata nyinyi watz msikosee tena kuchagua rais hasiyejali kwamba mnalipa kodi na mnastahili kupewa ruzuku ya pesa za maendeleo.

Kwenye karatasi ya kupiga kura ukiona rangi ya kijani na njano, iruke ASAP
 
Watu wanahangamia kwa kukosa maarifa , fikiria kama kiongozi hana maarifa , raia wake watakuwa na hali gani
 
MH Magufuli, nimeamua nije huku Jf nikupe za uso.Wanakilwa tunataabika sana, hao unaowaita watu sahihi, kwetu si watu sahihi.Wabunge wengi tulio waamini na kuwapa nafasi ktk Majimbo ya kilwa ambao ni wanasisiemu kindakindaki hawakuwa na msaada wowote kwetu sisi raia wa wilaya ya Kilwa.Tukiwachagua huwa wanaenda mazima, hawarudi hadi uchaguzi ukaribie. Kwanini tusichague vyama vingine ambavyo vinawatu wenye uwezo wa kutesemea maono yetu!!

Ni wachumia matumbo(Wabunge waliowahi kuhudumu Kilwa-CCM) hawapo kwaajili ya kutetea maslahi ya wana Kilwa.
#MwanaGiningi nipo njiani naja kuikomboa Kilwa yangu.

Nimekuwa nikichukizwa sana na misemo ya Watz wenzetu ambao hutusema sisi ni wa mwisho kwa kila jambo, inatia hasira!! Ila Mwanaginingi nakuja, nitaifanya kilwa iwe kama ile Kilwa iliyotukuka karne ya 15 kurudi nyuma, KILWA ambayo ilikuwa na dorali yake. Kilwa94

Mwanaginingi (mkombozi) nakuja.
 
Ina maana kampeni zimeanza?
 
Naona watu mnadonoa maneno machache mpate cha kuongea.
Aliposema "stendi ni kazi ya madiwani na wabunge....na fedha za road fund hutumwa", naona hapajaonekana.
Hivi unadhani ujenzi wa stendi ni sasa na ujenzi wa darasa,Hamna Halmashauri yoyote hapa Nchini ilishawahi kujenga stendi kwa fedha za ndani,pia hela za road fund zinaenda ni TARURA nazo ni za Barbara napo unaweza ombea 3B ukaletewa milioni 500 au 1B hii nchi waliopo ndani ya serikali ndio wanajua hizii hadaa za kisiasa.
Yani full comedy,Mkapa ambaye kila mtu anamtukuza Leo kama kiongozi making kuliko wrote ukimtoa Nyerere kwa hili la kumleta Jiwe alichemka vibaya sana.
 
Point sana hii
 
Mh. Rais,Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza lilikuwa na Mbunge kutoka CCM Mabula lakini ukifika Nyamagana ndo Jimbo linaongoza kwa barabara mbovu, stand ya Nyegezi imeahimdikana kujengwa na hatima yake hatuijui. Mbunge wa Nyamagana alomaliza muda wake Bwana Mabula ni bwege kuliko bwege wa Kilwa halafu cha ajabu katembeza rushwa na kuongoza kwenye kura za maoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…