Vita kati ya wafanyabiashara na TRA haitaisha kamwe kwa sababu zifuatazo.
1. Wafanya biashara wengi hasa wadogo na wa kati hawajui sheria za kodi.
2. Wafanyabiashara wengi hasa wadogo na wakubwa hawana rekodi sahihi za mapato, matumizi na faida. Yaani hawana vitabu vya hesabu. Jambo hili linasababisha ugumu katika kukokotoa kodi.
3. Mfumo wa TRA wa sasa wa EFD ni dhaifu. Una rekodi mauzo tu, hauruhusu wafanya biashara kuweka matumizi. Hauwezi kukadiria kodi kwa mauzo tu.
4. Mianya ya ukwepaji kodi ni mingi kutokana na mfumo wa biashara kuwa holela. Huwezi ku control wachuuzi kwa mamilioni waliopo sasa hivi.
5. Mfumo wa kodi una shida. Kuna ubaguzi baina ya wafanyabiashara. Mangi hama efd wala si VAT registered, mchuuzi wa barabarani hana efd wala si VAT registerd, lakini mwenye duka kubwa ana efd ni VAT registered. Wote wanauza biadhaa zinazofanana. Huyu mwenye EFD na VAT registered wakifuata sheria watakuwa ghali kuliko hao ambao si VAT registerd na hawatauza.
6. Huduma nyingi za kibiashara hazina risiti. Kwa mfano wewe kama una duka, ukinunua bidhaa kariakoo, unazipeleka mbagala utakodi kirikuu. Ila mwenye kirikuu hatakupa risiti. How do you account for that transanction. Same kwa nyanya na nyama kama una hotel. au ukioanda dala dala kwenda kuchukua mzigo hupati risiti ya TRA.
Nini kifanyike.
1. Badala ya ku categorise wafanya biashara kwa volume ya mauzo hawa ndo wawe VAT register au la. Classification ifanywe kwa aina ya bidhaa. Kwa mfano bidhaa za kila siku ambazo zinauzwa kwa mangi maduka ya aina hiyo yasiwe VAT registered. Lakini bidhaa zingine zote bila kujali ukubwa wa biashara wawe VAT registered.
2. Mfumo wa EFD utoe uwezo wa kurekodi matumizi ya biashara. Ili jioni unapopeleka taarifa uingize na matumizi ya siku hiyo. Kwa mfano uweke manunuzi ya mzigo uliofanya siku hiyo, pamoja na matumizi mengi kama usafiri, vibarua etc.
3. Kodi ikokotolewe kutokana na hesabu za mfumo ulioboreshwa.
4. Kutoa elimu ya kutosha. Kuwe na mtihani kabisa, kabla mtu hajapata leseni ya biashara ihakikishwe kuwa amesoma nankuelewa mfumo wa kodi kulingana na aina ya biashara anayotaka kufanya. Elimu elimu elimu.