Rais Magufuli awataka TRA kuacha kubambikia wafanyabiashara kodi, asema wanakadiria kodi kubwa ili wapewe rushwa!

Rais Magufuli awataka TRA kuacha kubambikia wafanyabiashara kodi, asema wanakadiria kodi kubwa ili wapewe rushwa!

Shida ya TRA ni mindset hasi ya watendaji kwa wafanyabiashara, kufanya kazi kwa mazoea, kukimbizia malengo kwa hofu bila kueleza ukweli kuwa hayafikiki,kukosa ubunifu wa kupanua wigo wa kodi ili idadi kubwa ya wananchi washiriki kulipa kodi ya moja kwa moja direct tax na hususani kupunguza sekta isiyo rasmi. Mwisho kupenda Rushwa hususani vijana wasio na uzalendo. Kuna haja ya kuangalia upya sera,sheria na kanuni za kodi na tozo.
Solution ya haya yote ni kuiondoa CCM
 
Serikali hii shida tu,wao ndio wanawapangia TRA malengo kwa kuwambia wakusanye kiasi kikubwa cha Kodi alafu leo eti wasikadilie Kodi kubwa,mfumo wa Kodi nchini no mbovu sana
 
Kwanini msiwaroge.??

Watanzania acheni kulia lia.

Mtu akikudhurumu mpige picha kisiri au chukua majina Yake nenda hapo Pemba au tanga wilaya ya lushoto Kijiji flani hivi.

Lazima waisome namba kwa kufa au kuteseka kwa kula haki za watu.

Msiwe mnategemea serikali kwa kila kitu. Mambo mengine fanyeni kwa uwezo wenu ili kutia adabu. Mtu anakuomba rushwa na ni haki yako. Wewe mpe kiroho Safi halafu mfanyie unyama.

Maisha yenyewe mafupi haya. Mtie adabu haswa.
Mkaribishe Yesu kwenye maisha yako, utajikuta tu hamu zako za kuroga watu zimeisha.
 
Mi naona ris hayuko serious na hili kwani TRA hawashtuki hata kidogo badala yake wameendelea kutesa wafanyabiashara bila kujali kauri zake.

Baada ya kile kikao cha rais na wafanyabiashara nikajua Tra watabadirika lakini hakuna kilichofanyika.
Wanakuja na mbinu ya kuvunja record ya makusanyo ili kumpoza, nayeye anapozeka ,mchezo unaendelea.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
ukija kufahamu tatizo si TRA ni yeye Rais utasikitika sana, ni lini Rais wetu ataacha unafiki? Hizo target hao TRA hawajawekewa na mtu mwingine ila yeye anayetaka kukamilisha miradi aliyoianzisha.
 
ukija kufahamu tatizo si TRA ni yeye Rais utasikitika sana, ni lini Rais wetu ataacha unafiki? Hizo target hao TRA hawajawekewa na mtu mwingine ila yeye anayetaka kukamilisha miradi aliyoianzisha.
Sina hakika kama ni yeye , lakini hata kama siye haiingii akilini kuwa anatoa maelekezo hayatekelezwi halafu anatoa tena - hayatekelezwi tena, lakini eti bado anatoa tena.

Hapo ndipo huingia kwenye kudhaniwa kuwa ndiye mpanga kodi hizi kubwa zisizolipika.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
ukija kufahamu tatizo si TRA ni yeye Rais utasikitika sana, ni lini Rais wetu ataacha unafiki? Hizo target hao TRA hawajawekewa na mtu mwingine ila yeye anayetaka kukamilisha miradi aliyoianzisha.
Kimantiki wao wanakusanya kodi. na wanatakiwa kukusanya kodi kwa watanzania wote wanaofanya kazi. Sasa inakuwaje focus yao ni watu wachache wenye biashara zinazoonekana?
 
Rais Magufuli ameitaka TRA kuacha kuwabambikia kodi wafanyabiashara na badala yake watoe makadirio ya haki.

Rais Magufuli amesema tabia ya kubambika kodi inawafanya wafanyabiashara washindwe kulipa na kutafuta njia za kukwepa kabisa kulipa.
Rais Magufuli amesema baadhi ya watumishi wa TRA wamekuwa na tabia ya kutoa makadirio makubwa na baadae kuomba wapewe rushwa ili wayapunguze.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

Hii kweli kabisa. Kuna mmoja yupo TRA tegeta jengo la Kibo complex ni mpuuzi sana anakadiria kodi hisiyolipika.
 
Back
Top Bottom