Rais Magufuli awataka TRA kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais Dk. John Magufuli, amekemea suala la wananchi kununua bidhaa bila kupewa risiti huku pia akiiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo.

'Wananchi hakikisha unachukua risiti kwa kila bidhaa unayonunua na muuza duka pia atoe risiti ambayo hela yake amepokea. Kumekuwa na tabia muuzaji anauza bidhaa ya milioni mbili yeye anatoa risiti ya elfu mbili, nimeagiza TRA hao wote washughulikiwe"
 
Ni Jambo jema Sana mkuu jiwe..

Ni Bora kubaki na wafanya biashara Wachache wanaolipa Kodi kwa uaminifu kuliko kuwa na wafanya baishara wengi waliojaa wizi na ujanja katika kulipa Kodi kwa serika angali Sisi wananchi tunalipa Kodi kwa uaminifu Kupitia bidhaa zao.
 
Rais Dk. John Magufuli, amekemea suala la wananchi kununua bidhaa bila kupewa risiti huku pia akiiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo.

'Wananchi hakikisha unachukua risiti kwa kila bidhaa unayonunua na muuza duka pia atoe risiti ambayo hela yake amepokea. Kumekuwa na tabia muuzaji anauza bidhaa ya milioni mbili yeye anatoa risiti ya elfu mbili, nimeagiza TRA hao wote washughulikiwe"
Kabla ya kuwachukulia hatua, wajiulize kwanini wafanyabiashara wanadanganya kutoa risiti zisizo sahihi au kutotoa kabisa,

Badala ya mamlaka kuwachukulia hatua watafute sababu ni nini au kwnini kuna udanganyifu, kwanini wafanyabiashara wanakwepa kutoa risiti
 
Kwanza watoa darasa na elimu kuhusu namna ya ulipaji wa kodi VAT
Wafanyabiashara wengi wao wanaweka faida yao tu kwenye bidhaa bila kuongeza kodi ya serikali
Hapo inapofika mda wa kulipa kodi wanachanganyikiwa kwa kudhani anadhulumiwa
Inatakiwa wholesalers wakatwe kodi juu kwa juu, hivyo mteja wa chini atajua kuwa kalipia na kodi kabisa naye atamdai mnunuzi wa mwisho kodi stahiki la sivyo tutazungushana tu mpaka kiama
 
Wenyewe wanasema kuna wakati gharama za ukusanyaji kodi zinakuwa kubwa kuliko kodi inayokusanywa

Ila kanuni ya kodi duniani kote ni lazima iwe ndogo sana ili hata anaeilipa isimuumize ila gharama ya kuikwepa inatakiwa iwe haibebeki

Aiseh maisha haya yana kikanuni vingi ikikaacha kamoja tu unakula mitama ya mchomvu wa mawingu media
 
Kwa wasiotoa risiti za kweli

Kweli ni kosa kutoa receipt isiyo na figure ya kweli, ila hata yeye juzi ametangazwa mshindi kwenye uchaguzi kwa matokeo yasiyo ya kweli. Tabia anayoikataa kwenye receipts, ndio tabia iliyompa madaraka. Pamoja na kuwa kweli kuna baadhi ya wafanyabiashara wanatoa receipts Zen figure ndogo kulingana na figure halisi, lakini ukweli ni kuwa makusanyo yameshuka kutoka na maamuzi yake mabovu kwenye sekta ya biashara.
 
Rais Dk. John Magufuli, amekemea suala la wananchi kununua bidhaa bila kupewa risiti huku pia akiiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo.

'Wananchi hakikisha unachukua risiti kwa kila bidhaa unayonunua na muuza duka pia atoe risiti ambayo hela yake amepokea. Kumekuwa na tabia muuzaji anauza bidhaa ya milioni mbili yeye anatoa risiti ya elfu mbili, nimeagiza TRA hao wote washughulikiwe"
Asante Rais Magufuli kwa kuliona hilo.

TRA wamelala usingizi wa pono. Duniani kote kodi lazima ilipwe! Nchi za wenzetu unafanya kulazimishwa risiti yako inaingizwa mfukoni. Maduka mengi hasa super markets kwa Tanzania ni mfano wa kuingwa.

Wizi huu kwa sasa umeshika kasi kwenye vituo vya mafuta. Mashine hazitoi risiti na kuna risiti za aina mbili.

Nashauri TRA wangetoa zawadi hata asilimia mbili ya pesa inayoibwa kwa kutokutoa risiti au kupewa risiti feki zoezi lingeenda kwa kasi kubwa nchi nzima. Ukitaka kula lazima uliwe by JK

Queen Esther
 
Rais Dk. John Magufuli, amekemea suala la wananchi kununua bidhaa bila kupewa risiti huku pia akiiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo.

'Wananchi hakikisha unachukua risiti kwa kila bidhaa unayonunua na muuza duka pia atoe risiti ambayo hela yake amepokea. Kumekuwa na tabia muuzaji anauza bidhaa ya milioni mbili yeye anatoa risiti ya elfu mbili, nimeagiza TRA hao wote washughulikiwe"
Ni Tanzania tu ndiko Rais ana deal na trivialities yaani nitty gritty. Kweli mnampeleka mtu Ikulu badala ya ku-deal mambo strategic ya kujenga uchumi anaanza ku- deal na risiti za petrol station za Ths 10,000.

This is too low for a president of a country like Tanzania with 59 Million people.
 
Back
Top Bottom