Rais Magufuli awataka TRA kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo

Rais Magufuli awataka TRA kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo

Rais Dk. John Magufuli, amekemea suala la wananchi kununua bidhaa bila kupewa risiti huku pia akiiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo.

'Wananchi hakikisha unachukua risiti kwa kila bidhaa unayonunua na muuza duka pia atoe risiti ambayo hela yake amepokea. Kumekuwa na tabia muuzaji anauza bidhaa ya milioni mbili yeye anatoa risiti ya elfu mbili, nimeagiza TRA hao wote washughulikiwe"
Akumbushwe kuwa vitambulisho vya ujasiriamali vina expire 30/12/2020.
Aanze kuvichapa vingine
 
Nimekutana na hii,friji bila risiti 450,000/=,ukitaka na risiti 500,000!Nikabaki njia panda!
Uamuzi niliouchukua naujua mwenyewe!

Wito:Serikali iwatendee haki wananchi wake wote bila kujali itikadi zao,dini zao au makabila yao!
Unaponiambia usiponichagulia fulani sileti maji halafu kesho fursa inatokea kama hiyo,nitaona wapi umuhimu wa kuwa mzalendo na kulipa kodi?Nilipe kodi kwa moyo,halafu baadae uniambie usiponichagulia fulani sileti huduma fulani?Si bora niokoe hela yangu kwa kutodai risiti na nikapata punguzo la bei!!
Tujengeeni uzalendo kwanza kwa kututendea haki,hata sisi wengine tutawaunga mkono mnapotuambia tudai risiti! Queen Esther Kadhi Mkuu 1
 
Kabla ya kuwachukulia hatua, wajiulize kwanini wafanyabiashara wanadanganya kutoa risiti zisizo sahihi au kutotoa kabisa,

Badala ya mamlaka kuwachukulia hatua watafute sababu ni nini au kwnini kuna udanganyifu, kwanini wafanyabiashara wanakwepa kutoa risiti
HAKUNA sababu ya kuhalalisha wizi.
 
Ni Tanzania tu ndiko Rais ana deal na trivialities yaani nitty gritty. Kweli mnampeleka mtu Ikulu badala ya ku-deal mambo strategic ya kujenga uchumi anaanza ku- deal na risiti za petrol station za Ths 10,000.

This is too low for a president of a country like Tanzania with 59 Million people.

Yani wewe ndo uko too low kama wasaidizi wake wamelala unataka na yeye alale. He knows what is doing....miradi lazima iishe na lazima tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi watu wangekuwa wanajua wajibu wao wa kulipa na Kudai receipt na wafanyabiashara kutoa receipt sahihi do you think Mr. President ungemwita too low[emoji23]
 
wamachinga ndio wanaokwamisha, wanachukua vitu kwa mali kauli kwa wahindi wanamwaga vitu mitaani alafu aje TRA eti anataka kodi alafu machinga anauza vitu nje bila risti hapo serikali itaendelea kupigwa tu
Na hili serikali inalijua au sio?
 
Kwa kweli Rais Magufuli ameongea jambo lenye kufaa sana kwa manufaa mapana ya uchumi wetu.

Haya ndiyo baadhi ya mambo ya kuunga mkono juhudi kwa muuzaji kutoa receipt bila shuruti na mnunuzi kudai receipt ili kwa pamoja tujenge Taifa letu.
 
Hivi wafanyabiasha kwanini hamtaki kutoa receipt za mashine ya EFD mfanyapo mauzo?
 
Yani wewe ndo uko too low kama wasaidizi wake wamelala unataka na yeye alale. He knows what is doing....miradi lazima iishe na lazima tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi watu wangekuwa wanajua wajibu wao wa kulipa na Kudai receipt na wafanyabiashara kutoa receipt sahihi do you think Mr. President ungemwita too low[emoji23]
Uzuri ni kwamba wasaidizi wake amewachagua mwenyewe siyo mimi. Kama wasaidizi ni mediocre basi na aliyewachagua naye ni mediocre.

Hii kitu ya risiti ameiongea kuanzia mwaka 2015 na amewahi kuchukua hatua nyingi ikiwa ni pamoja na kuingiza kipengele cha sheria kuhakikisha kuwa watu wanadai risiti. Unapoona miaka 5 bado watu hawa COMPLY ujue hiyo kitu imeshindwa.
 
Wamachinga ndio wanaokwamisha, wanachukua vitu kwa mali kauli kwa wahindi wanamwaga vitu mitaani alafu aje TRA eti anataka kodi alafu machinga anauza vitu nje bila risti hapo serikali itaendelea kupigwa tu
1.Serkali itoe wamachinga mijini katkat, haswa Arusha Dar na Mwanza. Watafutiwe maeneo yao rasmi. Mfano KWA Arusha Ile stand ndogo ijengwe maduka ya kutosha.

2.Hawa wamachinga hata wakipewa mali kauli wapewe risiti na hao wanaowapa hizo mahali kauli. Nakumbuka mh.Raisi alipoingia tu madarakani alilisema hili, watu wakabinga Sana, Ila Sasa naelewa mh.Raisi alikua sahihi Sana, Sana. Ili litatuliwe.

3. Tra ipitie KWA KILA machinga watoe risiti ya mizigo waliyo nayo. Maana Hawa hawalipi kodi wanauza bidhaa zile zile zinazopatikana madukani KWA Bei ya chini Sana, wanawafanya wafanyabiashara wa maduka wanashindwa kuuza kiushindani, hivyo wanakwepa kodi. Wanaowapa hizo mali wakitoa risiti ya efd watauza Bei ya ushindani.
 
Leo jioni au Kesho kuna wawili watatu washikwa na kutolewa kwenye taarifa ya habari kumuonesha Mungu kwamba wanafanya kazi

Check TV yako au gazeti utaona,leo au Kesho

Nchi isiyokua na mifumo,nchi inayofata matamko ya mungu mtu!
We toa risiti bhana! Biashara za kizembe achana nazo. Biashara siyo ujanja ni elimu na ufahamu.
 
Kweli ni kosa kutoa receipt isiyo na figure ya kweli, ila hata yeye juzi ametangazwa mshindi kwenye uchaguzi kwa matokeo yasiyo ya kweli. Tabia anayoikataa kwenye receipts, ndio tabia iliyompa madaraka. Pamoja na kuwa kweli kuna baadhi ya wafanyabiashara wanatoa receipts Zen figure ndogo kulingana na figure halisi, lakini ukweli ni kuwa makusanyo yameshuka kutoka na maamuzi yake mabovu kwenye sekta ya biashara.
Sheria zote duniani hutungwa kwa ajili ya wanyonge.
 
Rais Dk. John Magufuli, amekemea suala la wananchi kununua bidhaa bila kupewa risiti huku pia akiiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo.

'Wananchi hakikisha unachukua risiti kwa kila bidhaa unayonunua na muuza duka pia atoe risiti ambayo hela yake amepokea. Kumekuwa na tabia muuzaji anauza bidhaa ya milioni mbili yeye anatoa risiti ya elfu mbili, nimeagiza TRA hao wote washughulikiwe"
hali isha kuwa Mbaya paka kaamua kuingia Field
 
Kabla ya kuwachukulia hatua, wajiulize kwanini wafanyabiashara wanadanganya kutoa risiti zisizo sahihi au kutotoa kabisa,

Badala ya mamlaka kuwachukulia hatua watafute sababu ni nini au kwnini kuna udanganyifu, kwanini wafanyabiashara wanakwepa kutoa risiti
Biashara ni ngumu na Wafanyibiashara hawapati faida yoyote ndo maana wanadanganya kuhusu kipato chao !
 
Asante Rais Magufuli kwa kuliona hilo.

TRA wamelala usingizi wa pono. Duniani kote kodi lazima ilipwe! Nchi za wenzetu unafanya kulazimishwa risiti yako inaingizwa mfukoni. Maduka mengi hasa super markets kwa Tanzania ni mfano wa kuingwa.

Wizi huu kwa sasa umeshika kasi kwenye vituo vya mafuta. Mashine hazitoi risiti na kuna risiti za aina mbili.

Nashauri TRA wangetoa zawadi hata asilimia mbili ya pesa inayoibwa kwa kutokutoa risiti au kupewa risiti feki zoezi lingeenda kwa kasi kubwa nchi nzima. Ukitaka kula lazima uliwe by JK

Queen Esther
Dada ni petrol station za wapi hazitoi receipt? Mana bora ungetoa mfano mwingine lakini sio petrol station wao pump zimeunganishwa na mashine ya receipt akiuza receipt inatoka
 
Back
Top Bottom