Rais Magufuli awataka TRA kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo

Rais Magufuli awataka TRA kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo

Yeye anachojua ni kushughulikia watu tu hamna kingine
 
VAT siyo kodi inayotozwa kwa mfanyabiashara.
Mfanyabiashara yeye ni kama wakala anayetakiwa kuikusanya na kuiwasilisha TRA kwa wakati kwa mujibu wa sheria.

Sasa mnacholalamikia hapo ni nini hasa?
 
Sheria ya kodi inasema kuwa mfanyabiashara atatozwa kodi ya mwaka kutokana na mauzo yake ndani mwaka(siyo katika faida).
Mamlaka ya mapato inatambua mauzo yako ya mwaka kupitia rekodi ya risiti ulizotoa kwa kupitia hiyo mashine ya EFD.

Wafanyabiashara hawatoi risiti za EFD kupunguza hesabu za mauzo yao ya mwaka ili mwisho wa siku walipe kodi nafuu.

Kwa Kampuni na mauzo yanayozidi 20M kama sijakosea kwa sasa kuanzia 100M na wenye kuandaa hesabu hulipa kodi kwenye faida.

Hao wengine hulipia kwenye mauzo.

Hata hivyo huko kulipia kwenye mauzo mbona utaratibu wake uko vizuri wala haukandamizi mlipakodi?!

Jamani ifike mahali waTz tujivunie kutii sheria bila shuruti .

Tujivunie kulipa kodi kwa wakati.
 
Dada ni petrol station za wapi hazitoi receipt? Mana bora ungetoa mfano mwingine lakini sio petrol station wao pump zimeunganishwa na mashine ya receipt akiuza receipt inatoka
👍
 
Mimi nashauri kote tutengeneze mifumo ya kulinda tunachokikusanya.

Tunaweza kusanya kodi lakini kuna mahali pana vuja.

Tutaishia kulumbana kumbe kunauwezekano kuna mahali mfumo tulionao unapelekea kibubu kisijae.

Tuwekeze kwenye kutengeneza mifumo thabiti ya kulinda tunachokikusanya.
 
Kwa upande mmoja ni sawa ulichoandika lakini mimi naona yote yaende sambamba pamoja na swala kwa uhamasishaji , enforcements Na maximization of Tax collections .

Pia ubunifu wa tax bases ambazo hazitamuelemea mwananchi kwa sana.
 
Kuna watu wanajadili hili swala la kodi kisiasa !

Lakini mimi naona haifai kulifanyia mzaha sababu ni swala nyeti sana kwa manufaa ya kila mmoja wetu na ndugu zetu.

Ni kupitia kodi serikali huweza kuwalipa madaktari ambao mtu ukiumwa wanakutibu,

Kulipa walimu, wanajeshi wanaolinda mipaka yetu, maaskari wanaotulinda na mali zetu na watumishi wote wa Umma kila mmoja kwa umuhimu wake kwetu.

Zaidi kulipia gharama za miradi ya maendeleo yetu n.k

Tulipe kodi kwa hiyari na kuona fahari.
 
Mimi nashauri kote tutengeneze mifumo ya kulinda tunachokikusanya.

Tunaweza kusanya kodi lakini kuna mahali pana vuja.

Tutaishia kulumbana kumbe kunauwezekano kuna mahali mfumo tulionao unapelekea kibubu kisijae.

Tuwekeze kwenye kutengeneza mifumo thabiti ya kulinda tunachokikusanya.

Hata swala la kununua magari ya gharama kubwa kila Mwaka linapaswa kuangaliwa.

Mfano upotevu wa pesa za Umma kwenye rasimu ya katiba ambapo mpaka leo lengo halijafikiwa.

N.k
 
Hahahahah you killed on dat 1!

Mkuu aisee anadeal na mambo madogo sana ambayo hayawez kuipush hii nchi mbele, hakyamungu nakwambia tuanze kuhesabu majanga, yan sijui hata what the future holds for us. Nashangaa sana Young people wanavyomshangilia, Mzee kashajizeekea kazi ipo kwetu surprisingly watu hawaoni hilo
 
Inakuja hiyoo, maji muite mma.
Kodi kulipa kawaida tu sio kesi.
 
kuna uwezekano wa Tanzania Kukusanya Kodi Kubwa Tu na wafanya Biashara na TRA wakawa na amani na furaha katika utendaji wa majukumu yao.Kuna matatizo Kwenye idara za Serikali pamoja na TRA,ambayo kama ayatofanyiwa kazi tutabaki na lawama kila kukicha,EFD ni chanzo cha mapato Kiduchu na Kila kukicha tutaendelea kukusanya Kodi ndogo ,atuwezi kuongeza mapato hapa nchini kwa mfumo uliopo sasa ndani ya TRA .kwa nyakati tofauti,tofauti nimejaribu kuonana na kushauri hili kwa wahusika,awasikilizi !Why China wanakozalisha 80% EFD machines awazitumii kukusanyia kodi? Why Kenya wana EFD lakini awana Songombingo kama TZ?,Why USA,UK na India no drama kwenye ukusanyaji wa kodi?kule Bandalini ile metered Fuel Pump ipo na inafanya kazi?au bado meli zinashusha mafuta kwa kukadiria??Mungu ibariki Tanzania[emoji120]

Watu hawelew kwamba ni system ndio ipo fuwked up, na tuanze kuifi system ili iweze kumwajibisha kila mmoja kwa upande wake wenyewe wamekazana na kuziba tobo kwa kidole badala ya kutafuta permanent solution
 
Hizi kodi huwa hazipangwi na wizara kama unavyopanga matumizi ya familia yako, Bunge ndio lenye dhamana la kupanga na kupitisha sheria mbali mbali zinazotumika. Wasiliana na Mbunge wako.
Waziri ndiye anapeleka miswaada, na ana team na resouce zote za kuweza kufanikisha hilo.
 
Wafanya biashara hawatishiwi, ni kuongea nao, na kuweka mifumo inayozuia hali hiyo matatizo, hawa watu wanatumia akili sana kufikia kuitwa wafanya biashara, wakiingiwa na uwoga wanawekeza akili zao nying kwenye kujilinda na sio ubunifu wa kuongeza uzalishaji.
 
Rais Dk. John Magufuli, amekemea suala la wananchi kununua bidhaa bila kupewa risiti huku pia akiiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo.

'Wananchi hakikisha unachukua risiti kwa kila bidhaa unayonunua na muuza duka pia atoe risiti ambayo hela yake amepokea. Kumekuwa na tabia muuzaji anauza bidhaa ya milioni mbili yeye anatoa risiti ya elfu mbili, nimeagiza TRA hao wote washughulikiwe"
Hoteli ya Mt. Hotel Kilosa, Guest ya Leopard na Elephant Njia panda Moshi tunaomba TRA iwatembelee wajionee wanatoa huduma nzuri sana na risiti za efd
 
Rais Dk. John Magufuli, amekemea suala la wananchi kununua bidhaa bila kupewa risiti huku pia akiiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo.

'Wananchi hakikisha unachukua risiti kwa kila bidhaa unayonunua na muuza duka pia atoe risiti ambayo hela yake amepokea. Kumekuwa na tabia muuzaji anauza bidhaa ya milioni mbili yeye anatoa risiti ya elfu mbili, nimeagiza TRA hao wote washughulikiwe"
Yaan km kuna mwanya Serikali inapoteza mapato bc ni hapa.Unakuta umenunua bidhaa anakwambia machine ya EFD mbovu anakuandikia risit ya mkono , wengine ndo ivo thaman ya 200000 anakuandikia 50000.
 
Kuna kila dalili mambo sio mazuri. Mtashikana uchawi soon
 
Wamachinga ndio wanaokwamisha, wanachukua vitu kwa mali kauli kwa wahindi wanamwaga vitu mitaani alafu aje TRA eti anataka kodi alafu machinga anauza vitu nje bila risti hapo serikali itaendelea kupigwa tu
Hii post wale wanaompelekea taarifa wamlatie na hii. Hapa kariakoo tunachokifanya sisi wa maduka ya jumla ni kuwa na vijana wako kumi au ishirini. Kila siku unawapa mzigo kwa masharti wakauze kwa bei tunayowapa faida atajipangia mwenyewe auze kwa bei gani. Jioni analeta hela yangu na hanidai risiti kwanza nakua kama namsaidia maana yeye halazimiki kuwa na hela mkononi ili afanye biashara. Magu aliposema machinga waachwe kila kona ya mtaaa alitusaidia sana sisi wa maduka ya jumla maana sasa hivi hatukwepi kodi tu bali hatulipi kabisa.
 
Back
Top Bottom