Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Polepole waziri ajae. Tanzania kufanikiwa kisiasa ni rahisi sana. Yaani uwe mnafiki,.uwe CCM ,umsifie Magufuli at any cost. Utetee CCM at any cost.

Yaani ufanye propaganda zote kuwa Magufuli kafanya maajabu ya kuipaisha Tanzania ndani ya miaka mitano. Hongera Polepole.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Wabunge 2 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
View attachment 1637284
Teuzi za siku hizi ni "personal" zaidi.Kama walevi na wana propaganda wanapata kuna jipya hapo? Acha tule magimbi tukisubiri muujiza wa saruji kushuka bei.
 
Back
Top Bottom