Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Wabunge 2 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
View attachment 1637284
Makonda huenda akachukua nafasi ya Polepole ndani ya chama cha makanjanja.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Spika akawaapishe kwenye gereji kama kawaida yake.... asisubiri mpaka February
 
Nilitegema hii nafasi atapewa Hamisi Mwinjuma, Mwana FA. Kwakuwa kama kusoma kasoma, na alikuwa kwenye mfumo huo huko Basata na ni msanii pia
Hajui siasa huyo mwana FA.Ubunge kapewa unamtosha.
 
Natoa tu ushauri kutokana na heshima kubwa ambayo komredi Polepole amekijengea chama basi ni vema siku atakayoapishwa na Spika tukio hilo lifanyike ukumbi wa Pius Msekwa.

Hongera komredi Polepole kwa kuteuliwa kuwa mbunge.

Maendeleo hayana vyama!
Na asipoapishwa gereji akina halima watauzunika sana
 
Nikikumbuka kuanzia bunge la katiba. Mara kwenye serikali ya JPM alivyobadilika. Unafki unalipa. Hivi nyie mnaolalamika hamna kazi mbona fursa zipo pale Lumumba. Au hamna number ya Magufuli niwape ????Hongera Polepole ukale keki ya taifa waziri wa utalii na maliasili.
 
Back
Top Bottom