Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Nikikumbuka kuanzia bunge la katiba. Mara kwenye serikali ya JPM alivyobadilika. Unafki unalipa. Hivi nyie mnaolalamika hamna kazi mbona fursa zipo pale Lumumba. Au hamna number ya Magufuli niwape ????Hongera Polepole ukale keki ya taifa waziri wa utalii na maliasili.
Tupe connection mkuu
 
ila siasa ikikukubali unakula shumbwela sana..ndani ya miaka mitano pole pole katoka kuwa Dc bukoba,kaenda kuwa Dc Ubungo nadhani,, kaenda uenezi,,sasa ni mbunge na kesho atakua waziri..ni ndani ya miaka mitano haya yanatokea
 
Lakini kasoma kama Juliana Shonza aliweza kuwa naibu mwana FA uwaziri atauweza
Mwana Fa hawezi kupewa uwaziri kamili, akibahatika ni Naibu waziri, hana Cv yoyote ya uongozi zaidi ya kuwa msanii mzuri na msomi. Ubunge tu tayari ameanza kujitunisha akipewa uwaziri directly atatemea mate wenzie, acha apoozwe kwanza.
 
View attachment 1637307

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Wabunge 2 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

View attachment 1637284
Mipasho inahamia upande kwenye mjumba
 
Magufuli anatengeneza team bungeni ya kubadili katiba ili kuondoa ukomo. Pole pole anayajua sana kujenga hoja. Tuweke uongo pembeni.
 
Anaweza kuendelea kuishikilia kwani umesahau Nape alikuwa katibu muenezi na bado alikuwa mbunge kipindi cha kikwete

Nape hakuwa mbunge kipindi cha Kikwete, rejea vizuri kumbukumbu zako
 
Mr slow slow wa sasa Hana impact yoyote katika taifa amekuwa mwongo hata aliyosimamia mwanzo anayakana?
 
Back
Top Bottom