Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Mara hii au kwa kuwa aliandaa ile concert mchomvu alipompiga mtama mbasha
sarcastic.gif
 
Labda Polepole atapewa uwaziri alafu ule ukatibu Uenezi na Itikadi atapewa Makonda
 
Uteuzi ujao itakuwa ni kina halima mdee kuwa naibu waziri
 
Huyu ni Waziri wa mambo ya ndani au mambo ya nje au waziri wa ulinzi ajae.
 
Sawa mkuu, lakini pia hii CCM ya Magufuli ilipitisha sheria mpya ya mtu mmoja kofia moja kwahiyo nafasi hiyo inakuwa wazi automatically
Hivi katibu muenezi wa chama na kuwa mbunge, nani anakuwa na cheo kikubwa?
 
Ataapishwa kama akina mhe Halima mdee.Hoja ya kuapisha gereji itakua imekufa
 
View attachment 1637307

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Wabunge 2 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

View attachment 1637284
Wadau taratibu zipi wadau?Akina mdee na wenzake waliapishwa kea mujibu wa taratibu na Sheria zipi?
 
Back
Top Bottom