Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Jamani najua hana mke, mwenye namba yake anipe, wife material Nipo hapa
 
Bwashee hebu mstue mwenyekit amteue pia mr.P mana njaa ishapanda mpk.kichwan
Natoa tu ushauri kutokana na heshima kubwa ambayo komredi Polepole amekijengea chama basi ni vema siku atakayoapishwa na Spika tukio hilo lifanyike ukumbi wa Pius Msekwa.

Hongera komredi Polepole kwa kuteuliwa kuwa mbunge.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hahaaaa!!!unafik bongo unalipa
Polepole waziri ajae. Tanzania kufanikiwa kisiasa ni rahisi sana. Yaani uwe mnafiki,uwe CCM ,umsifie Magufuli at any cost. Utetee CCM at any cost. Yaani ufanye propaganda zote kuwa Magufuli kafanya maajabu ya kuipaisha Tanzania ndani ya miaka mitano.Hongera Polepole.
 
View attachment 1637307

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Wabunge 2 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

View attachment 1637284
Huyo riziki lulida,nani anamjua,atupe maelezo yake?
 
Magufuli anatengeneza team bungeni ya kubadili katiba ili kuondoa ukomo. Pole pole anayajua sana kujenga hoja. Tuweke uongo pembeni.
Alikuwa anajua kujenga hoja zamani, sasa hivi anachofanya ni uzandiki tu. Ukishakuwa biased huwezi kujenga hoja, maana utakuwa hutumii logic. Akitolewa kwenye ulaji ataweza kujenga hoja. Huwezi kujenga hoja huku chama chako 50%+ imetangazwa washindi kwa hila.
 
Ukweli lazima usemwe, Mh. Polepole ailipga kazi bwana...najua hakuwa peke yake ila kuanzia majukwaa ya kampeni, burudani, mikwara kwa yule dogo wa Bavicha aliyetaka kulipua transifoma Arusha, nk
Mungu akupe maisha marefu Mh. Polepole.
 
Safi sana, ndo wadau wa maendeleo waone demokrasia yetu ilibyopevuka. Yaani katibu mwenezi anakuwa mbunge wa kuteuliwa nafasi maalum za Rais zinazohtaji wataalamu.
kwani unazani polepole hajasoma we jamaa vp
 
Alikuwa anajua kujenga hoja zamani, sasa hivi anachofanya ni uzandiki tu. Ukishakuwa biased huwezi kujenga hoja, maana utakuwa hutumii logic. Akitolewa kwenye ulaji ataweza kujenga hoja. Huwezi kujenga hoja huku chama chako 50%+ imetangazwa washindi kwa hila.
Sasa anajenga hoja kutetea huu upande alipo. Majority wanamkubali.
 
Back
Top Bottom