Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Hivi katibu muenezi wa chama na kuwa mbunge, nani anakuwa na cheo kikubwa?
Kwenye Chama Mbunge ni cheo kidogo maana nafasi ya maamuzi anayoishia ni kamati ya siasa ya wilaya na mkoa (sina uhakika sana kuhusu k/siasa mkoa). Mbunge haingii H/Kuu taifa. Halmashauri kuu CCM taifa ni chombo cha pili kikubwa kwa maamuzi baada ya Kamati kuu CCM taifa ambapo ndugu Polepole alikuwa ni katibu idara ya uenezi, siasa na itikadi.

Ila kisiasa na kimaslahi nafasi ya ubunge ni kubwa kuliko uenezi taifa kwa sababu nyingi ila kuu mbili ni

1.Ubunge unakupa promising future ya kisiasa nchini, maana mbunge anaweza kuwa waziri na kuingia kwenye Baraza la mawaziri.

2. Ubunge hauna ukomo kikatiba, ila nafasi ya uenezi sio rahisi kutumikia kwa muda mrefu maana zama za Mwenyekiti aliyekuweka zikiisha na wewe basi tena. Bila kuchanga karata za kisiasa vizuri unapotea. Ni bora uombe dakika za mwisho, Mwenyekiti akukumbuke hata uwe mkuu wa mkoa.

Ndio maana wengi wanakimbilia kugombea ubunge kama Nape.
 
Tukio la juzi la MWAMBA Mbowe lililotemesha nchi la kuwafukuza COvid-19 limezima njama zoote za JIWE za kuwapa Unaibu waziri Halima,Esther( square) kama alivyokuwa amewaahidi. Tayari duniani nzima inafahamu kuwa JIWE na MFUMO wamewarubuni wadada wa Covid-19. Maskini pole nyingi ziende kwa Job na Mahera kwa jinsi walivyojidhalilisha. Mda si mrefu Mahera atapangiwa kazi nyingine kwa jinsi walivyokosea kucheza karata zake vizuri katika movie ya Covid-19
 
Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwanini tangazo hili limetolewa kwa umakini mkubwa kuwa baadaye wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Msimseme vibaya huyo mama tafadhali, kumbukeni ni mlemavu huyo
 
Pascal Njaa hajateuliwa ? Mwambieni Jiwe amteue ataehuka avue nguo kwa mada anazoandika sasa ataehuka njaa imembana sana ..
 
Ya kupanga wizi wa kura? Unafanya kazi kubwa kisha 2/3 ya wapiga kura hawajitokezi, au ndio mambo ya kuvikana vilemba vya ukoka?
2/3 hawajitokezi alafu kuna manunda yanadai yameibiwa kura...
 
Hawa walioteuliwa leo, wataapishwa kwenye parking ya magari kama covid-19 au watasubiri hadi bunge lijalo?

Sisi wengine sheria hatuzijui jamani mtujuze siku wakila kiapo cha ubunge ili tuangalue TV
 
Hongera sana Mh. Humphrey kwa kuteuliwa kuwa Mbunge hakika unastahili umefanya kazi kubwa sana.
 
Back
Top Bottom