Rais Magufuli awatumbua Kitila Mkumbo, Ole Sendeka na Katambi, awateua Jumanne Fhika, Dr. Aloyce Nzuki, Allan Kijazi, Josephat Paulo, Kemikimba

Magufuli aache watu wawe huru kufanya watakalo muhimu wasimuharibie kazi, huwezi kumfungia mtu ndani kama mbuzi, sio siku zote mtu afanye unalotaka wewe tu, huu nao ni udikteta.

Kwa muendelezo huu ataendelea kuteua wapya kila siku, vyema ajifunze kuheshimu taratibu alizozikuta, asitake kubadilisha kila kitu.
 
Ni matumizi tu mabaya ya kodi zetu. Badala ya kuteua Wataalamu, unawateua Wanasiasa wenzako! Unategemea nini muda wa kufanya hiyo siasa utakapofika/utakapowadia? Ni lazima tu wakukimbie ili wakatafute malisho ya uhakika.

Na tutamshangaa sana Rais iwapo atawateua tena watu wa aina hii iwapo watashindwa kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya chama au hata kushindwa kabisa kwenye huo uchaguzi mkuu ujao.
 
Kijazi wa TANAPA ameteuliwa kua Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mali asili huku akiendelea pia na u-boss wake pale TANAPA.

Hao ndio wenye nchi sasa,wanyonge walie na umaskini wao tu.
 


Kama ni hivyo kuna haja gani sasa ya kuchagua Raisi mpya kama kila kitu ni lazima kibakie kama kilivyo alivyokikuta? Raisi wa JMTZ Katiba inamruhusu kufanya anavyofanya, shida iko wapi?
 
Kijazi wa TANAPA ameteuliwa kua Naibu katibu Wizara ya Mali asili huku akiendelea pia na u-boss wake pale PANAPA.

Hao ndio wenye nchi sasa,wanyonge walie na umaskini wao tu.
Anafaya kazi sehemu mbili na kupata mshahara mara mbili ama🤔🤪
 
Ndio madhara ya kumzuia mbwa kubweka wakati ndo utamaduni wake. Basi hata na mawaziri watumbuliwe maana na wao wameacha ofisi wamekimbilia majimboni kugombea. Tena wengine ni wateule kabisa na hawakuwa na majimbo. Mfano Mzee wa jalalani, Mwl wa hesebu (Ndalichake), Buhingwe kule kwa Mwl Mpango na wengine weeeeeengi tu akiwepo First lady mstaafu.
 
Jamaa walishtuka pale walipogundua kuwa hata ubunge akikuteua anakutumbua. Bora kucheza salama! CCM asilia wananifurahisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…