Rais Magufuli awatumbua Kitila Mkumbo, Ole Sendeka na Katambi, awateua Jumanne Fhika, Dr. Aloyce Nzuki, Allan Kijazi, Josephat Paulo, Kemikimba

Rais Magufuli awatumbua Kitila Mkumbo, Ole Sendeka na Katambi, awateua Jumanne Fhika, Dr. Aloyce Nzuki, Allan Kijazi, Josephat Paulo, Kemikimba

Hizi Ni dharau kwa mwenyekiti wao, kwamba pamoja na angalizo alilolitoa bado wanamuona si lolote si chochote.

Ngoja tuone Kama Mwenyekiti wao atawalamba miguu kwa kuruhusu uteuzi wao, maana alishawapiga ban wasithubutu
Hapana, siyo dharau. Angalau sasa naanza kuona kitu hapa, nilikuwa kabisa sielewi nini kinaendelea. Ni haya maswala ya watu wataalamu wa kufikiria, believe me!
 
Mimi naona mwenyekiti na yeye wangemzuia kugombea mimi naisi asingefika hapo alipo hii ni kuzuia demokrasia
Siwezi kushangaa, kampeni zake 2015 alisema kwny serikali yake mtu akiharibu sehemu moja kamwe hatahamishiwa sehemu nyingine atamfukuza tu.

Lakini tumeona kwa Mwigulu, Simbachawene, Kamishina Andengenye aliwaponda balaa wkt wa kuwatumbua ila baadae akawarudisha serikalini na kuwapa vyeo huku akisema ni wazalendo haswaa.
 
Nikukua sijui kwamba wewe ni katambi
Magufuli aache watu wawe huru kufanya watakalo muhimu wasimuharibie kazi, huwezi kumfungia mtu ndani kama mbuzi, sio siku zote mtu afanye unalotaka wewe tu, huu nao ni udikteta.

Kwa muendelezo huu ataendelea kuteua wapya kila siku, vyema ajifunze kuheshimu taratibu alizozikuta, asitake kubadilisha kila kitu.
 
Siwezi kushangaa,kampeni zake 2015 alisema kwny serikali yake mtu akiharibu sehemu moja kamwe hatahamishiwa sehemu nyingine atamfukuza tu.

Lkn tumeona kwa Mwigulu,Simbachawene,Kamishina Andengenye aliwaponda balaa wkt wa kuwatumbua ila baadae akawarudisha serikalini na kuwapa vyeo huku akisema ni wazalendo haswaa.
Hahahaha, Mh Rais MTU wa huruma, ukiomba msamaha unasamehewa na kupewa shavu jingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea point.. aliteua makada akidhani watamramba miguu
Ni matumizi tu mabaya ya kodi zetu. Badala ya kuteua Wataalamu, unawateua Wanasiasa wenzako! Unategemea nini muda wa kufanya hiyo siasa utakapofika/utakapowadia? Ni lazima tu wakukimbie ili wakatafute malisho ya uhakika.

Na tutamshangaa sana Rais iwapo atawateua tena watu wa aina hii iwapo watashindwa kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya chama au hata kushindwa kabisa kwenye huo uchaguzi mkuu ujao.
 
Kijazi wa TANAPA ameteuliwa kua Naibu katibu Wizara ya Mali asili huku akiendelea pia na u-boss wake pale PANAPA.

Hao ndio wenye nchi sasa,wanyonge walie na umaskini wao tu.
Hahahaha
Hivi Hawa akina Kijazi wako wangapi huko serikalini ?
Tanapa
Ikulu
Hali ya hewa
Kote huko nadhani kuna Kijazi au nachanganya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo Magufuli huwezi pimana naye ubavu.. ni mtata balaa.
Ndio madhara ya kumzuia mbwa kubweka wakati ndo utamaduni wake. Basi hata na mawaziri watumbuliwe maana na wao wameacha ofisi wamekimbilia majimboni kugombea. Tena wengine ni wateule kabisa na hawakuwa na majimbo. Mfano Mzee wa jalalani, Mwl wa hesebu (Ndalichake), Buhingwe kule kwa Mwl Mpango na wengine weeeeeengi tu akiwepo First lady mstaafu.
 
Ukitumia akili vizuri, ubunge miaka 5 tu unatosha kutoka kimaisha. Mambo mengine ni stress tupu ndiyo maana watu wanaona isiwe tabu.
 
Magufuli amefanya madudu mengi yanayosababisha wengi tumpinge ili awe bora na akishindwa kujirekebisha aondoke au aondolewe. Lakini kwa hili namuunga mkono. Watu wamefanya Ubunge kama uenyekiti wa VICOBA!!!
 
Picha ndio kwanza linaaanza. Yani hii ni vita ya ndani kwa ndani kwanza kabla ya kwenda kushindana na upinzani. Mungu awasaidie wote na wakishindwa wasirudishwe na wasipewe vyeo tena hawana nidhamu kukiuka amri ya mheshimiwa Rais.
 
Hahahaha
Hivi Hawa akina Kijazi wako wangapi huko serikalini ?
Tanapa
Ikulu
Hali ya hewa
Kote huko nadhani kuna Kijazi au nachanganya?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahah Agness, Balozi, TANAPA ni kula maisha tu mzee baba.

Hao sasa wakisema tuko uchumi wa kati unawaelewa vizuri ila wale ndugu zangu dizaini za kina Le Mutuz nawaonea huruma tu hahah.
 
Back
Top Bottom