Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Hivi Magufuli anajua (kuheshimu )boundaries (mipaka)zozote? Anawatia watu majaribuni kila upande, bora kwake sifa iwepo. Hela za kanisani vyanzo vyake vingine kwa wenzetu ni haramu.
 
Kama Magufuli alifanya vile kwa upendo, Kwa nini wakati wa ujenzi wa lile kanisa hakwenda msikitini kuomba waislamu wachangie ujenzi wa hilo kanisa?
 
Inawezekana ni kweli sijaelewa aisee [emoji3][emoji3]

Sasa Naomba nisaidie kuelewa kwa kifupi hoja ya za msingi ni zipi ?

Je mleta mada msingi wa madai yake ni nini?
Msingi wa medai ni kwamba huwezi changisha pesa za kujenga msikiti ukiwa kanisani. Ni haramu. Labda kwa mashekhe kama kuna al ahd yule shekh mpuuzi wa Mkoa wa dar ambaye anaweza kula hata nguruwe kumlidhisha NYAPARA
 
Nahisi siku akikutanishwa na Lissu anaweza akatimua mbio aisee! Maana hataamini kama ni Lissu yule yule aliyeshambuliwa kule Dodoma mchana kweupe wakati ule, au ni mzimu.
[emoji23] [emoji23]
 
..nadhani tunazunguka-zunguka bila kwenda kwenye MSINGI/KIINI cha tatizo.

..mimi nadhani Jpm ni mwanasiasa asiye na hoja na haiba ya uongozi, hivyo amekuwa akitumia makanisa na misikiti kufanya siasa...
Kama kawaida yako siasa ndio kila kitu.

Unamsaidia vipi Alhaj ambaye anafanya kazi na Rais lakini ikifika ijumaa hana nyumba ya Ibada?.

Aendelee kuteseka kisa Rais akianzisha mchango wa msikiti kanisani itaonekana ni siasa?

Rais anampa Peter Tino tshs milioni tano anachangia ujenzi wa vyoo vya shule, atashindwa vipi kuchangia ujenzi wa msikiti?.
 

..bwana mkubwa anatumia dini kama kichaka cha kufanya siasa.

..mbona Mwalimu Nyerere aliwapatia Waislamu wa Butiama msaada wa Msikiti lakini hatukumsikia akijitangaza kila mahali?

..yeye kila akisali anataka atangazwe.
 
UFAFANUZI KUHUSU MCHANGO WA FEDHA ULIOCHANGISHWA NA MH. RAIS KANISANI KWA AJILI YA UPANUZI WA MSIKITI.

MIMI NI MUISLAAM, NINAYEIFAHAMU DINI YANGU VIZURI KIASI KWA KUKAA DARASANI KUISOMA...
Kutangaza sadaka ya kumsaidia mtu mwingine ni kujipendekeza na kutafuta umaarufu kupitia shida za watu.

Waarabu wanatoa matrilioni ya pesa kusaidia misikiti dunia nzima lakini hawatangazi na kuonyesha jinsi wanavyozichanga kwa harambee ama laa. Inakua ni siri ya sadaka yao.
Kujitafutia kura kwa njia ya dini ni tatizo na halifai kuungwa mkono zaidi ya kukataliwa kabisa.
Watu watatuletea siasa za udini udini hata akija Mwingine naye akifanya hivyo kwa dini yake au kuona kuwa ni zamu ya kabila au dini yake tumkatae pia.

Uchaguzi uwe huru na haki ili watanzania waonyeshe kuwa wanajua wanachojaribu kudananywa na watu wachache kwa maslahi yao.
 
..bwana mkubwa anatumia dini kama kichaka cha kufanya siasa.

..mbona Mwalimu Nyerere aliwapatia Waislamu wa Butiama msaada wa Msikiti lakini hatukumsikia akijitangaza kila mahali?

..yeye kila akisali anataka atangazwe.
Enzi za Mwalimu ni tofauti na za sasa. Kila mtu anayo hulka yenye kumtofautisha na mwingine.
 
Lissu ni Mwanaharakati makini, Ni Mwanasheria Nguli, ni Wakili Msomi, alikuwa ni Mbunge Machachari, Ni kiumbe jasiri! Hastahili kupaishwa na mtu yoyote yule! Anajipaisha mwenyewe.
Kwa mm mjinga kama wewe lisu ni nguli wa sheria. Sijawahi kumwona mbunge taahira kama lisu tangu bunge la enzi ya mkapa.
 
..kila chama wakiamua kumuiga bwana mkubwa na kufanya siasa kwenye nyumba za ibada tutakuwa salama kweli?.
Bwana Mkubwa ni rais wa nchi anaweza akaongea popote anapoona inafaa kwake kuongea.

Anaweza akatoa agizo lolote hata akiwa ndani ya Bar au nyumbani kwa mtu yoyote.
 
Bwana Mkubwa ni rais wa nchi anaweza akaongea popote anapoona inafaa kwake kuongea.

Anaweza akatoa agizo lolote hata akiwa ndani ya Bar au nyumbani kwa mtu yoyote.

..yah, lakini asifanye mama ambaye yanaharibu misingi ya taifa letu.
 
Kama Magufuli alifanya vile kwa upendo, Kwa nini wakati wa ujenzi wa lile kanisa hakwenda msikitini kuomba waislamu wachangie ujenzi wa hilo kanisa?

Sawa bro. Hakufanya kwa upendo. Nyie chochoeni ujinga, utaishia pabaya. Jifanye mfia dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…