Rais Magufuli azindua umeme wa gesi asilia Kinyerezi II, asema ataendelea kushirikiana na wananchi kulinda amani

Raisi yeye ndo anatoa pesa?kweli ww jamaa noma kodi ya wananchi unasema pesa ya raisi.....hivi bado unakula kwa baba na mama?
Wewe jamaa acha uzuzu hiyo kodi nani anakupangia kiwango na ukiitoa inaenda wapi na nani anayeimba kila siku pesa ipo!!! Wewe unadhani unaposikia Serikali imesema unadhani anayesema ni nani? Kuna kitu kinaitwa serikali kama sio rais. Ukisikia serikali imepinduliwa unaelewa nini? Si rais alokuwepo kaondolewa madarakani.

Usiishi ndotoni, jitahidi kuja kwenye uhalisia wa mambo. Pesa ikishakusanywa ni ya rais dogo. Sasa endelea kuota.
 
Mropokaji msingekuwa mnamjadili kila mara na kuonya kuwa mtaua, ueni ndugu zenu sasa, kwani mnaishi mbinguni?
Ushawahi sikia mtu anauliwa bila sababu, ikitokea ni bahati mbaya.

Hivi ukitoa ushauri wako bila kumkashifu mtu hawezi kukuelewa. Hauwezi kumkashifu baba ndani ya nyumba akaendelea kukuvumilia.Atakutimua au kukufanya lolote baya.
 

Hapana mkuu simaanishi kusifia, ila pesa ikishakusanya inaenda Serikalini. Kwani serikali ni nani mkuu kama sio rais? Anaweza kuamua afanye nini na hizo pesa kama tulivyoshuhudia awamu ilopita jamaa alikuwa akisafiri kila mwezi nje ya nchi. Kipindi cha Nyerere pia aliwekeza zaidi kwenye Ukombozi nchi za Afrika.

Hizi zana za Bunge ni zana tu lakini jamaa pale Magogoni akiamua kuwa mwizi anachota tu maana ana full control ya Hazina. Ndio maana nikasema anatoa pesa, hiyo hiyo kodi yako na yangu ndio pesa zake
 
Wacha uwongo hakuna ni Megawati 180 tu na sio MW240 acheni kujipa ujiko kwanza mradi wenyewe ni ufisadi ndani nje serikali imepigwa na wajanja wa CCM takribani USD 100,000,000 halafu nyie washamba mnashangilia?

Mimi nijuavyo ni 1MW saa na 1Mil USD.

Sasa nashangaa wqetu huu ni almost 240MW kwa USD 432 Mil.

Hii 432USd ni sawa na 986 Bil. 1Tril.

hahah tumepigwa!
 

Kwa katiba letu bovu sawa sawa na kwa vyma vyetu vibovu pia!
 
Mawee, naanza kuingiwa na hofu. A giant project without feasibility study, EIA, etc!!!. Ee Mungu twaomba utunusuru na haya majanga.
 
Eti rais anatoa pesa elimu ni kitu cha msingi sana.

Usijidanganye na Elimu wewe, kama unadhani una elimu basi haijakusaidia bado unaishi ndotoni. Katiba yako inampa mamlaka makuu Rais hadi kukalia mihimili mingine ya dola kiasi kwamba dola Serikali ina nguvu kubwa sana. Ukiongelea serikali una maanisha rais. Ukisema Serikali ina pesa kwa mfumo wa Tanzania una maanisha rais ana pesa. Ndiye anayeamua pesa apeleke wapi japo bunge linapitisha wa mwisho kuamua atoe ama asitoe ni rais na hamwezi kumfanya chochote.

SASA wewe baki na elimu ukidhani wengine tumekwepa umande. Shauri yako.
 
You have got nothing to share, nothing less nothing more. Nimekuomba tu kitu basic kabisa u disclose, kwamba umejua je tumepigwa $100,100,100? in relation to what as per regard. Unakuja na matusi mengii.
Hakuna tusi lolote hapo. Yeye kaonyesha pakuanzia, kama uko kwenye 'kitengo' kachimbue kunako Wizara husika na shirika husika ili mtoe ushauri sahihi. Mnataka mtafuniwe kila kitu?
 
Inaonyesha kabisa mpo tayari kuua, mtaua sana nyie mtakaoishi milele
Suala sio wapo tayari kuua. Tatizo waandamanaji au wanaandamana kwa msukumo wa mtu anayeishi kwa malipo ya kutukana rais. Hivi wewe huyo Mange ahamasishe maandamano ya kumpinga rais wakati anashinda mitandaoni kumtusi rais halafu Jeshi la Polisi liwasindikize. Kama mimi ndio Rais nalala mbele na IGP kwa uzembe huo mkubwa.

Hakika mkuu watakuua ukithubutu kuandamana. hata ikiwa mimi ndio polisi miguu yako ni halali yangu hiyo tarehe 26, hauwezi kuniharibia ulaji wa watoto wangu

Wewe upo tayari kuandamana kutetea maslahi yako na ya Mange, Polisi nao wapo tayari kuua kutetea kitumbua cha watoto wao.
 
Nimenunua jenereta mpya,namwomba mh.aje anizindulie.
 

TUMEPIGWA TU!



The first stone of the project to build a combined cycle natural gas power station, capable of producing 106 megawatts of electricity, was laid on Thursday in Maputo, in a ceremony that was attended by the Minister of Natural Resources and Energy, Mozambican news agency AIM reported.

The president of state power company EDM, Mateus Magala, said at the time that the plant, which will cost US$180 million, is the first major public investment in power generation infrastructure through the company.

To build this power plant, the government of Mozambique was granted a loan of US$167 million from the Japan International Cooperation Agency (JICA) at an interest rate of 0.01% per year, with a payment period of 40 years including a grace period of 10 years.

EDM’s contribution to the project, which is expected to start in December and take two and a half years, is US$13 million.
 
Eti rais anatoa pesa elimu ni kitu cha msingi sana.
Tatizo mkuu umekaririshwa elimu ya kujua kuongea kiingereza na kuvaa majoho chuo kikuu ndo elimu. Ni sawa na wale wanaoamini kuvaa shela ndio ndoa. Huu ni upumbavu wa hali ya juu sana. Kuna exposure ambayo pia ni elimu kubwa sana kushinda hata huo ujinga unaodhani ni elimu. Unapokuwa na exposure ndogo (limited exposure) katika mambo mbalimbali matatizo yake ndio hayo. Unabaki kudhani hizo theory na bookish ulizosoma darasani ndio kila kitu. Haujui hata kwanini vitabu vinakuwa na Editions kwa sababu vitu hubadilika na vitabu kupitwa na wakati. Haujiliuzi kwa nini vitabu hupitwa na wakati? Ni sababu kuna kitu kinachotangulia hiyo elimu and you need to update yourself ili uweze kuendana na changing situation.

Wasomi wa leo taabu kweli kweli na hivi vyuo vikuu ya sasa vinachukua hadi Division three ambazo enzi zetu ilikuwa unaishia kwenda Polisi ni taabu tupu. Basi mmebaki kujitapa ya kuwa ninyi ni wasomi, msomi unashindwa kupambanua kitu kidogo namna hii.
 
unajua watawala wetu wanakosea, kufanya kitu fair wao hawajui, ni mwendo wa double standards, mfano tizama uchaguzi wa madiwani wapinzani walivyofanywa, tizama na uchaguzi huu walivyofanywa, masanduku ya kura yanaibiwa na yanarudishwa na wenyewe, angalia mauaji ya akwilina, wanaua wao kisha wanabambikizia kesi ati wapinzani walikuwa wanaandamana, wale pale walikuwa wanafata vibali vyao, ambavyo mliviatamia mpaka akwilina kufa mkavitoa saa 5 za usiku baada ya kusikia askari wenu wameua, manake hawa sio askari wa kulinda wananchi ni askari wa kulinda ccm, mbaya na kilichowaumiza wapinzani ni kuwa ccm viapo wamepewa wiki kabla hawa wapinzani ati wasubiri siku 3 kabla, kweli inaingia akilini, wanapodai haki zao mnawaita ati ni wachochezi, wao ni wachochezi wa maendeleo na sio uchochezi wa kuua watu, kutesa, mbona haya mambo utawala uliopita hayakuwepo, ilikuwa ni nadra sana kusikia sasa ni hadharani, unadhani kama mbowe angeuwawa siku hiyo isingezungumzwa tena hiyo issue kama walivyofunika ya lisu, nahisi ile risasi hasa ilimlenga mbowe, nae ni kudra ya Mungu tu, lakini sasa hivi tungekuwa tunasema hayati mbowe, very sad indeed
 
Pokea 7000
 

Mkuu hilo ni hakika.
Tumerithi mfumo wa kikoloni na hatukuufanyia marekebisho. Jeshi linatii amri ya rais na linawajibika kwa rais. Dola Serikali ina nguvu nyingi inaweza kusumbua mihimili mingine. Huu mfumo utaendelea kwa muda mrefu lakini pia hata wanaodai mabadiliko wengi wao hawaaminiki wanatafuta jukwaa la kupandia lakini hawana nia ya dhati. Nasema hivo kwa kuwa ukifuatilia wafanyayo ni tofauti na wanayohubiri majukwaani.

Kwa hiyo kabla ya kubadili huu mfumo watu wakaidi wataumia na kitakachowaumiza ni ukaidi wao na kushindwa kuelewa wanashindana na mfumo wa utawala unaobebwa na katiba yetu.
 

Sasa nini kifanyike ili kuondokana na hali iliyopo ?
 
Sasa nini kifanyike ili kuondokana na hali iliyopo ?
Hapo solution mkuu ni kuwa na katiba ya wananchi inayowafanya watawala wawajibike kwa wananchi. Pia kuwe na sera na vipaombele vya taifa. Tuwe na mwelekeo mmoja kama taifa sio mwelekeo wa mtu. Maana kila kiongozi akija anakuwa na sera na mwelekeo wake sasa hii inarudisha nyuma maendeleo ya nchi. Hakuna mwendelezo.

Ila mpaka tufike huko bado ni safari ndefu. Tuombee tu kiongozi anayeingia awe muadilifu na mwelekeo wake na sera viwe sahihi kusaidia wananchi na kulinda rasilimali za nchi
 
Wakati wananchi wa Mtwara wakati ule wanapigwa na kuwekwa ndani kwa kupinga mradi wa bomba la gesi, tuliambiwa mradi wa gesi ni muhimu sana kwa taifa letu. Tena wakasema mradi huu ukikamilika, kukatika kwa umeme kutakuwa ni historia, na gesi ya kupikia itashuka bei. Wakasema pia Tanzania itakuwa nchi ya "Uchumi wa gesi" kwa maana itakuwa na gesi ya kutosha ya kuweza kuuza kwa nchi nyingine. WanaCCM wenzangu, mnakumbuka??? Sasa miaka michache baadaye: Je Tanzania ina uchumi wa gesi? Je sasa bei ya gesi imeshuka?, Je sasa tatizo la umeme ni historia?? Jibu unalo mwenyewe. You can do you yourself another silly justice by believing in lies if you wish. Good luck.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…