Kapustakasha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2016
- 248
- 423
Rais Mhe. Dkt. John Magufuli leo atazinduzi mradi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia (Kinyerezi II) Jijini Dar es Salaam.
Mradi huu utaingiza megawatts 240 katika gridi ya Taifa. Matangazo ya moja kwa moja yatarushwa na TBC 1 & Azam Two kuanzia saa 3:30 asubuhi hii.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM , Humphrey Polepole naye yupo kwenyye uzinduzi huo, ansema mradi huu wa umeme utasaidia Tananzania kufikia kwenye uchumi wa kati mwaka 2025 kwa kuzalisha umeme utakaoendesha viwanda vitakavyochakata mazao ghafi
Rais John Magufuli, amabye nimgeni rasmi wa uzinduzi huo anawasili kwenye uzinduzi huo akipokelewa na waziri wa Nishati na Madini pamoja na maafisa wa Tanesco na wajumbe mbalimbali
Mradi huo unatarajiwa kuzalisha Megawatt 240 za umeme ambao utaingizwa kwenye gridi ya taifa yenye Megawatt 2200 na kupunguza upungufu wa umeme mikoa ya Kusini kama Mtwara na Lindi
Waziri wa Nishati na Madini anakaribishwa na Mkurugenzi wa Tanesco Mwinuka kumpa maelezo ya kiufundi kuhusu mradi huo
Wacha uwongo hakuna ni Megawati 180 tu na sio MW240 acheni kujipa ujiko kwanza mradi wenyewe ni ufisadi ndani nje serikali imepigwa na wajanja wa CCM takribani USD 100,000,000 halafu nyie washamba mnashangilia?