Rais Magufuli azindua umeme wa gesi asilia Kinyerezi II, asema ataendelea kushirikiana na wananchi kulinda amani

Rais Magufuli azindua umeme wa gesi asilia Kinyerezi II, asema ataendelea kushirikiana na wananchi kulinda amani

Rais Mhe. Dkt. John Magufuli leo atazinduzi mradi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia (Kinyerezi II) Jijini Dar es Salaam.

Mradi huu utaingiza megawatts 240 katika gridi ya Taifa. Matangazo ya moja kwa moja yatarushwa na TBC 1 & Azam Two kuanzia saa 3:30 asubuhi hii.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM , Humphrey Polepole naye yupo kwenyye uzinduzi huo, ansema mradi huu wa umeme utasaidia Tananzania kufikia kwenye uchumi wa kati mwaka 2025 kwa kuzalisha umeme utakaoendesha viwanda vitakavyochakata mazao ghafi

Rais John Magufuli, amabye nimgeni rasmi wa uzinduzi huo anawasili kwenye uzinduzi huo akipokelewa na waziri wa Nishati na Madini pamoja na maafisa wa Tanesco na wajumbe mbalimbali

Mradi huo unatarajiwa kuzalisha Megawatt 240 za umeme ambao utaingizwa kwenye gridi ya taifa yenye Megawatt 2200 na kupunguza upungufu wa umeme mikoa ya Kusini kama Mtwara na Lindi

Waziri wa Nishati na Madini anakaribishwa na Mkurugenzi wa Tanesco Mwinuka kumpa maelezo ya kiufundi kuhusu mradi huo

Wacha uwongo hakuna ni Megawati 180 tu na sio MW240 acheni kujipa ujiko kwanza mradi wenyewe ni ufisadi ndani nje serikali imepigwa na wajanja wa CCM takribani USD 100,000,000 halafu nyie washamba mnashangilia?
 
Raisi mchapakazi nzalendo wa kweli nakipenzi cha walio wengi asante kwa mega watts nyingine ila nitafurahi zaidi tukipata zile 2000 pale selou
Jinga kama hili linalodhani rais anagawa megawatt kwa hela za kuuza ng'ombe wake chato sijui unalikomboaje
 
Uzi wake wa kumuhesabia miradi anayizindua upo active...

Uzi unaanza kupata contents sasa
 
Mnakuza mambo ili mpate kicki.

Hata wakati wa JK vilizinduliwa vingi tu ila bado kura zilishuka.
Kamanda yaani kabisa na akili zako zote unamfananisha JK na JPM?!
Japokuwa JPM ana miaka takribani 3 tu madarakani ila hakika JK kaachwa mbaali mno!
Alichomzidi sanasana labda ni uhandsome tuu, ofkoz na lugha nzuri adhimu ya kiswahili!!.
 
Nanukuu "Nakupungiza upungufu wa umeme kwa grmikoa ya kusini mtwara na lindi"
Swali kwani hiyo mikoa pia imeunganishwa kwenye hiyo 2200kv?/grid ya taifa?
Punguzeni siasa kwenye vitu vya technical
 
Kamanda yaani kabisa na akili zako zote unamfananisha JK na JPM?!
Japokuwa JPM ana miaka takribani 3 tu madarakani ila hakika JK kaachwa mbaali mno!
Alichomzidi sanasana labda ni uhandsome tuu, ofkoz na lugha nzuri adhimu ya kiswahili!!.
Huyu jamaa kawachota akili na mnadhani ni watanzania wote.
 
April 2 kaweka jiwe la msingi la ujenzi wa rada na kupokea ndege mpya, April 3 anazindua mradi wa kinyerezi ambao hapo kabla ulishazinduliwa na JK, April 6 atakuwa mererani kuzindua ukuta, April 7 atakuwa Arusha kuzindua nyumba za makazi ya polisi. This is called one man show
Hayo wasema wewe
 
Hivi huyu JPM anafanya kazi muda gani Ofisini!? Kauli mbiu yake ya "HAPA KAZI TU" anaitendea haki!? Binafsi, sioni kbsa huyu Rais km anafanya kazi zaidi ya kupiga misele ya hapa na pale Nchini! Utofauti wa JK na huyu JMP ktk muktadha wa kupiga misele, JK alikuwa anatembea Nje ya Nchi lkn huyu jamaa anafanya misele yake ndani ya Nchi, speed na viwango vya kutokuketi Ofisini vinafanana!! Uzinduzi wa miradi ambayo haijakamilika, imeshika hatamu! Simuuelewi kbsa
 
Kinondoni tu penyewe ilibidi mtumie nguvu za ziada na kupora masanduku.Msijisahau mkafikiri hii miradi ndio itapumbaza watu wakasahau machungu wanayoyapata leo hii.
Mimi hata kama ningekuwa na chama, kama Mtanzania, nafuatilia mipango na mikakati ya uchumi na maendeleo, kwa mtazamo wa kina. Wewe na wenzio endeleeni na siasa za majukwaani.

Labda nikuulize, hao viongozi wako wakiruhusiwa mikutano ya hadhara na maandamano, ndiyo nchi itaendelea?

Ada ya mwungwana ni vitendo. Serikali inajenga na kuboresha: Elimu na mazingira yake (km madawati shuleni); Afya; Maji; Umeme; Njia za usafiri nk. Mnayaona mabadiliko hayo lakini mnaona demokrasia ya maneno ndio kipaumbele chenu.

Mnajua ukweli jinsi mnavyotengeneza matukio ili nchi isitawaliwe na kudai maandamano kwa nia ya kujenga chuki ndani ya wananchi. Kuthibitisha Serikali iko makini, na inazijua mbinu chafu za CHADEMA, viongozi wake wamekamatwa na sheria itachukua mkondo wake, hilo halina ubishi. Wewe na wenzio endeleeni kujifariji kwa kejeli za matusi humu tu JF.

MNAJIAIBISHA
 
Anapenda uzinduzi huyu jamaa hivi hii ndio kilichompeleka ikulu jamani au ndio mambo ya kupenda kuuza sura
Anapenda kukata utepe masikini ya Mungu ameingilia kazi za makamu wake.
 
Back
Top Bottom