Rais Magufuli azitaka Wizara kutominya taarifa na zikubali kukosolewa, aagiza Wizara ya Habari kufuatilia

Rais Magufuli azitaka Wizara kutominya taarifa na zikubali kukosolewa, aagiza Wizara ya Habari kufuatilia

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Akiendelea na ziara yake ya siku tatu mkoa wa Dar es Salaam, ambapo leo Februari 25, 2021 ameweka jiwe la msingi katika soko la Kisutu na kuzindua jengo la Jitegemee, Rais Magufuli ametoa wito kwa wizara zote nchini kuwa wepesi kutoa ushirikiano kwa wanahabari ili kufikisa taarifa kwa wananchi.



Niwaombe tutangulize maslahi na uzalendo wa taifa letu.

Lakini nitoe wito pia kwa watendaji wenzangu ndani ya serikali; wawe wepesi katika kutoa taarifa. Ziko wizara ambazo Waandishi wa Habari wakienda kutaka taarifa zozote zinafichwa, pamoja na kwamba kuna wawakilishi na wasemaji wa wizara. Na Wizara ya Habari, bahati nzuri waziri upo hapa na Katibu Mkuu wa wizara husika, hebu lifuatilieni.

Sisi ndani ya Serikali tuwe wepesi katika kutoa taarifa mapema ambazo zinaleta faida kwa Watanzania.

Tunaficha habari nyingine hata za maendeleo. Unakuta kumefanyika mambo mazuri katika wizara hiyo lakini hayatolewi kwa wananchi ili kujua ni yapi yamefanyika.


Tusiogope kukosolewa. Tukubali kukosolewa lakini pia tukubali kujirekebisha kwa ajili ya kuwapatia wananchi hawa habari muhimu ambazo ni haki yao kuzipata.

Upande wa serikali tuwe wepesi kutoa taarifa zilizo sahihi, na upande wa vyombo vya habari navyo viwe vyepesi kutoa habari za ukweli bila kuweka chumvi, lakini pia kwa kuzingatia maslahi ya taifa na uzalendo.
 
We Gwajima jichanganye uone cha MOTO.

Kumbuka ya Dr Mwele.

Anajikosha kua hafichi taarifa za Doportivo
 
Back
Top Bottom