Rais Magufuli azitaka Wizara kutominya taarifa na zikubali kukosolewa, aagiza Wizara ya Habari kufuatilia

Rais Magufuli azitaka Wizara kutominya taarifa na zikubali kukosolewa, aagiza Wizara ya Habari kufuatilia

Maneno matupu, mpaka pale atakapowajibishwa mtu kwa kutokutoa / kuminya au kuficha habari kama wanavyobana watu kwa kutoa habari ndio tutaamini kweli anamaanisha.

Unless otherwise itakuwa ni mwendo wa vyombo kuendelea kutangaza / kueneza propaganda.
 
Mwenye kumiliki chombo cha habari anaweza kumiliki fikra za watu.

Usemi wa wajuvi.
 
Tanzania inatakiwa kuwe na sheria ya Uhuru wa habari unayoishurutisha serikali na ofisi za umma kutoa habari, la sivyo zichukuliwe hatua za kisheria.

Haya mambo ya rais kasema rais kasema, rais anaweza kusema publicly kisiasa wizara zitoe habari, halafu akakaa pembeni na mawaziri na kuwaambia wizara zisitoe habari.

Kinachotakiwa ni sheria ya kuwashitaki wasiotaka kutoa habari.
 
Jana na leo kuna nini mbona kumekuwa na point chanya kutoka Ikulu?
Duh,

Yani imefikia wakati kukiwa na point chanya kutoka Ikulu watu wanashangaa kuna nini!

Halafu, unaweza kuona point chanya, kumbe ni maigizo ya kisiasa tu.

Mkuu anatoa tamko moja "for public consumption", halafu kwenye vikao vya ndani anatoa tamko tofauti linalolipinga hilo la public.

Kinachotakiwa ni kuwekwa sheria ya kushurutisha habari zitolewe.

Hizi habari za nchi kuendeshwa kwa matamko, kutoka kwa mtu anayebadili muelekeo kila siku, zimepitwa na wakati.
 
Sijui amemaanisha au ndio siasa zenyewe, ngoja tuangalie ni mapema sana kutia neno.
 
Create tatizo, then solve uonekane shujaa. However angeanza yeye kwanza
Basi tuanze nawalewanaoungana na redio washirika wakisikia baadhi ya habari zenye manufaa kwa raia,wapo tayari wajitoe hewani,ama wanaweka mziki mpaka habari hiyo ipite,hata kama ni yenye maslahi kwa umma.
 
Tusiogope kukosolewa. Tukubali kukosolewa lakini pia tukubali kujirekebisha kwa ajili ya kuwapatia wananchi hawa habari muhimu ambazo ni haki yao kuzipata.

Sun is shining.
The weather is sweet,
Make you wanna move,
Your dancing feet.....

images.jpg
 
Ni kweli kabisa kuficha ficha baadhi ya taarifa kunatengeneza vaccum ambayo wapotoshaji wanatumia kuingiza propaganda zao,

Wakifanya hivyo watapunguza wimbi la viwanda vya uongo huko mitaani.
 
Wewe mleta habari hii utashitakiwa kwa kumwekea Mzee maneno mdomoni, eti "tukubali kukosolewa!" Haya maneno hayawezi kutoka kwenye kinywa cha huyu tunayemfahamu. Labda ulete clip ya hiyo hotuba. Kama ni kweli basi kuanzia kesho jua litachomoza Magharibi na kuzama Mashariki
 
TBC tayari inafanya hayo... kishindo cha serikali ya awamu ya tano...
 
Ahsante mkuu.
Waambie wanaohusika watoe taarifa kuhusu mambo yafuatayo:

1.Watu kutekwa,kupotezwa na majaribio ya kuuawa kwa watu kadhaa km LiSSU,Ben Saanane,Azory.
2. Ajira za walimu 5000 za kimyakimya za walimu za TAMISEMI.
3.Uwekezaji wa Chato
 
Back
Top Bottom