Rais Magufuli: Benki ya Dunia wanatoa pesa wakijua Tanzania tuna msimamo gani na tunafanya nini, wapiga kelele wapuuzwe

Rais anatuchanganya tu. Mara atuambie sisi ni matajiri. Tunajenga miradi kwa kodi za watanzania. Inakuwaje tena anasema kuhusu benki ya dunia tena ?
Akili za kuambiwa changanya na zako.
Huwezi kupata mkopo kama sio tajiri ambaye unaweza kurudisha mkopo na riba!

Ni kweli sisi ni matajiri ndio maana tunakopesheka!
 
Hivi kuna mtu ameona hayo maneno "huwa hawaishi duniani"?Lissu ilitamkwa tu akalambwa risasi
 
Mbona mnatumia nguvu kubwa sana kutaka mabeberu wawape hela wakati nyie ni matajiri? Mbona hamueleweki? Hata elimu tu lazima mkope? Mnakopa mnunue chaki na kujenga matundu ya vyoo? Serious?
Nguvu kubwa sana ni relative term!

Kile unachodhani ni nguvu kubwa sana inawezekana kwa wengine ni tofauti!

Kumbuka hata ujinga unazidiana!
 
Mbona mnatumia nguvu kubwa sana kutaka mabeberu wawape hela wakati nyie ni matajiri? Mbona hamueleweki? Hata elimu tu lazima mkope? Mnakopa mnunue chaki na kujenga matundu ya vyoo? Serious?
Matajiri wote duniani wanakopa. Nchi tajiri zote zinakopa. Marekani na China zinakopa. Masikini hakopeshwi, anasaidiwa.

Unashangaa mkopo kutumika kuboresha mazingira salama ya kujifunzia na nyenzo? Zipo nchi zinakopa ili kununua hifadhi ya chakula. Yaani zinakopa hela ya kula.

Sijui wengine mnatazamaje mambo!
 
Nashangaa anayenunua ndege kwa cash halafu anakopa hela ajenge matundu ya choo na kununua madawati. Hilo halikushangazi wewe?

Wakati huo huo kutwa kujitapa yeye ni tajiri anatoa elimu bure? Kumbe anakopa ili atoe elimu bure😄😄
 
Madawati ni muhimu lakini hayaingizi pesa ya haraka na hayaitangazi nchi kivyovyote. Hayana mchango kwa utalii na sekta ya biashara. Ni huduma isiyo na mrejesho wa fedha, tofauti na ndege au miundombinu.

Pesa ya mkopo ni yako kwa sababu utailipa. Kwahiyo kama anakopa ili atoe elimu bure, maana yake ametoa pesa yake/yetu haijalishi ameazima au la.
 
Hoja yako ni ipi hasa?
 
Rais anatuchanganya tu. Mara atuambie sisi ni matajiri. Tunajenga miradi kwa kodi za watanzania. Inakuwaje tena anasema kuhusu benki ya dunia tena ?
Akili za kuambiwa changanya na zako.
Huu mwaka una mambo! Victoire hivi ni wewe? Heri za mwaka mpya. Hakika leo akili za kuambiwa umechanganya na zako! Kumbe binti akili zako si zile za level ya akili ni nywele kila mtu anazo. Mbona taahira na machizi wana vichwa misitu lakini ndani ombwe? Leo tufurahi, Victoire wetu kumbe aweza kuwa pia Ingabire!
 
Yes naweza kuwa Ingabire kasoro mimi kamwe siwezi jitolea kama Ingabire alieacha familia yake Holland kwenda pambana na Kagame.
 
Back
Top Bottom