Rais Magufuli: Benki ya Dunia wanatoa pesa wakijua Tanzania tuna msimamo gani na tunafanya nini, wapiga kelele wapuuzwe

Rais Magufuli: Benki ya Dunia wanatoa pesa wakijua Tanzania tuna msimamo gani na tunafanya nini, wapiga kelele wapuuzwe

Mkopo haujawahi kuwa msaada!

Unakopeshwa tu kama una uwezo wa kulipa Mkopo pamoja na riba!

Uko sahihi, lakini mkopo wa hizo taasisi za kimataifa huwa una masharti yake. Uwezo wa kulipa sio kigezo pekee cha kupata mikopo toka kwenye hizo taasisi. Halafu hata kama ni uwezo wa kulipa bado Tanzania sio ya hivyo, otherwise nchi yetu isingekuwa na hili deni la taifa. Tafuta sababu nyingine hii uliyotoa ni dhaifu.
 
Yes naweza kuwa Ingabire kasoro mimi kamwe siwezi jitolea kama Ingabire alieacha familia yake Holland kwenda pambana na Kagame.
Hongera sana. Nimekupenda. Usijali sana hata hiyo unayoita kasoro yaweza toka. Kuacha familia nini? Waweza hata kuwa tayari kuacha dunia! Mwanzo mzuri wa kupigania haki kwa wote. ( Mark you not Lipumba style)?
 
Huwezi kupata mkopo kama sio tajiri ambaye unaweza kurudisha mkopo na riba!

Ni kweli sisi ni matajiri ndio maana tunakopesheka!

Kuweza kulipa deni hakumaanishi wewe ni tajiri bali ni kuaminika kuwa utajikusanya na umasikini wako na kulipa deni.
Unataka kuniambia wale wanaokopa dukani kwa mpemba unga wa ugali wanakopeshwa kwa vile ni matajiri na watalipa?
Acheni utani wenu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu sio msaada bali ni mkopo!

Mkopo sio msaada kwa sababu huwezi kukopeshwa kama huwezi kulipa na riba!
Kama tungeweza kulipa basi tungekua na deni lisilokua, wewe deni linakua kila siku linakua alafu unajigamba eti una uwezo wa kulipa.

Anyway, tuna uwezo wa kulipa, kwani hizo serikali zilizopita hazikua na uwezo wa kulipa? Maana zilikua zinakopeshwa na hatukuwahi kusikia zikijigamba kama ya sasa ambayo kila siku unasikia tuna hela, hela zipo ila mikopo kila siku.
 
Kwa akili yako unadhani utajiri ni pesa pekee!

Halafi kumbuka unapewa mkopo kulingana na utajiri wako!

Nani alikudanganya kuwa kuaminika ni kigezo pekee cha kupewa mkopo?
 
Kama tungeweza kulipa basi tungekua na deni lisilokua, wewe deni linakua kila siku linakua alafu unajigamba eti una uwezo wa kulipa.
Kwa kukusaidia, pitia hii tovuti uone deni la taifa la Marekani na jinsi linavyokua/kuongezeka kila sekunde!
LINK>>>
Anyway, tuna uwezo wa kulipa, kwani hizo serikali zilizopita hazikua na uwezo wa kulipa? Maana zilikua zinakopeshwa na hatukuwahi kusikia zikijigamba kama ya sasa ambayo kila siku unasikia tuna hela, hela zipo ila mikopo kila siku.
Nani amekuambia kuwa hazikuwa na uwezo wa kulipa? Kwani deni limeanza wakati wa serikali ya awamu ya tano?

Sema HUKUWAHI KUSIKIA na sio kusema HATUKUWAHI KUSIKIA!

Usiweke mwanvuli wa fikra zako changa kwa watu wote!
 
Ni joja ya ajabu ku-justify deni letu na deni la Marekani.

Sijawahi kusikia marekani wakisema wana pesa za ndani, pesa zipo, alafu wanalilia mikopo.
Kumbuka kama hujawahi kusikia haina maana hawajawahi kusema!
 
Huu sio msaada bali ni mkopo!

Mkopo sio msaada kwa sababu huwezi kukopeshwa kama huwezi kulipa na riba!

Mzee, IDA uwa wanatoa mkopo kwa wale wasio creditworthy. Ndiyo maana wanatoa hata mikopo yenye zero interest. Ndiyo maana IDA uwa inachukuliwa kama ‘a development agency au aid agency’ wing ya WB.

Unless, mkopo uwe umetoka IBRD, ambayo ni wing halisi ya kibenki ndani ya WB, pamoja na IFC.
 
Nakubaliana kwa 100% kwamba watu aina ya Zitto na wale wanaofanana nao ni wa kupuuzwa na hawastahili kujibiwa.

Zitto anafahamika kwa kutafuta kiki akitumia njia ya uzushi na kuparamia mambo asiyoyaelewa vizuri. Kujibishana na watu wa aina hii ni kuwapa promo ya bure ya kujulikana kuwa bado wapo.

Nakubaliana na Rais Magufuli kwa 100% kwamba hawa wazushi ni wa kupuuzwa ili tuweze kusonga mbele.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wameshamjibu na tayari kwa mara nyingine mnamjadili tena, hivyo kashinda, hakuna kitu mtoto anataka zaidi ya attention!
 
Mzee, IDA uwa wanatoa mkopo kwa wale wasio creditworthy. Ndiyo maana wanatoa hata mikopo yenye zero interest. Ndiyo maana IDA uwa inachukuliwa kama ‘a development agency au aid agency’ wing ya WB.

Unless, mkopo uwe umetoka IBRD, ambayo ni wing halisi ya kibenki ndani ya WB, pamoja na IFC.
Kumbuka hata kulazimishwa kubadili sera za kiuchumi kwa manufaa ya mkopeshaji anayeitwa IDA pia ni njia mojawapo ya kulipa riba ya mkopo!
 
Nakubaliana kwa 100% kwamba watu aina ya Zitto na wale wanaofanana nao ni wa kupuuzwa na hawastahili kujibiwa.

Zitto anafahamika kwa kutafuta kiki akitumia njia ya uzushi na kuparamia mambo asiyoyaelewa vizuri. Kujibishana na watu wa aina hii ni kuwapa promo ya bure ya kujulikana kuwa bado wapo.

Nakubaliana na Rais Magufuli kwa 100% kwamba hawa wazushi ni wa kupuuzwa ili tuweze kusonga mbele.

Maendeleo hayana vyama!
hasiishie tu kumpuuza Zitto. Mwambie haache kufanya maamuzi ya matumizi ya pesa za watanganyika bila kuwashirikisha wabunge.
 
Back
Top Bottom