Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Ni makosa yao kutofunga mipaka kwa abiria wote halafu wanataka kufuta makosa yao kwa speculation kama walio changanyikiwa.
 

Bado unategemea summary zinazofanywa na some members wa JF? Hotuba ipo hapo, huu uvivu mtaacha lini?
 
Naona ulikuamkaririshaji mzuri shuleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba swalehe habari ya siku
Nimefurahi kukuona tena maana kuna post yako moja niliiona niliumia sana

Bila shaka unaendelea vizuri
 
Raisi wa Tanzania JPM amesema Tanzania inalipa bilioni 700 katika taasis mbalimbali duniani zilizoikopesha nchi yetu kila mwezi ikiwemo benki ya dunia inayolipwa bilioni 200 kila mwezi. Hii ina maana kwa mwaka hulipwa zaidi ya trillion 8.4 fedha ambazo ni zaidi ya mishahara yote wanayolipwa watumishi wa umma.

Kwa hili nani anabisha kuwa Tanzania siyo koloni la mabeberu? Tuna safari ndefu ndugu Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SALAAM ZA PONGEZI KWA MH RAIS MAGUFULI.

Na Elius Ndabila
0768239284


Leo Mh Rais amelihutubia Taifa alipokuwa akizungumza na wakuu wa vyombo vya usalama nchi. Hotuba ya Mh Rais imegusa mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, kubwa likiwa ugonjwa wa Corona ambao unaiandama dunia kwa sasa. Nilipata wasaa wa kusikiliza vizuri sana hotuba ya Mh Rais.


Ninaomba nitumie wasaa huu kumpongeza Mh Rais kwa kuzungumza na Watanzania na kutoa ushauri wake kama amiri jeshi mkuu. Hotuba ya Mh Rais ni ya kutia matumaini na kuwapa ali kubwa Watanzania. Ninaimani kubwa Kama ushauri wa Mh Rais utazingatiwa ugonjwa wa corona hautakuwa tishio Bali utakuwa sawa na magonjwa mengine.


Nimpongeze Mh Rais kwa kuzumzia pia suala la kinga na tiba. Mh Rais amesema kwa kuwa bado hakuna dawa za kutibu corona ni vema WATANZANIA tukajiongeza kwa kutumia dawa za asili ikiwepo kujivukiza. Waafrika tumekuwa na tabia za kupuuza dawa za asili na kuamini dawa za magharibi. Wakati mwingine hata dini zetu zimekataza kutumia dawa za asili na kutushauri kutumia dawa za hospital. Tumedanganywa kwa kuwa watu hawajui hata hizo dawa za hospital ni dawa za kienyeji zilizoboreshwa zaidi. Ni vema tuwape furusa Wataalamu wetu wa asili kuonyesha juhudi zao ktk hili ambalo limewashinda wazungu. Hotuba ya Mh Rais inawapa nguvu madakitari wa asili kuonyesha vipaji vyao. Ugonjwa huu ni vita ya KIUCHUMI, hata dawa wakipata wazungu si rahisi kutufikia huku kwa kuwa maombi Yao ni afrika kufa ili wapate fursa ya kuja kuchukua Uchumi wetu.


Mh Rais ninampongeza pia kwa kutolea ufafanuzi suala la mask. Hivi tunategemea kama virus vya corona ni watu walitengeneza wanaweza kututengenezea maski za kuzuia? Ninaamini ile tathimini tuliyoambiwa Afrika kufikia mwezi wa nne itakuwa na wagonjwa wengi hupenda walikuwa wamepiga ni idadi ya mask zilizoingia Africa ambazo zinaweza kuwa na virus. Walitegemea kadiri tutakavyotumia maski ndivyo tutakavyoambukizwa. Mh Rais amesema kuna tetesi kuwa baadhi ya nchi hizi barakoa zimeonyesha kuwa na virus. Mh Rais amewapongeza wale wote wanaotumia mask za vitambaa vilivyotengenezwa hapa nchini. Hongera sana Mh Rais kwa kushauri viwanda vya hapa nchini vijiongeze na kuanza kutengeneza barakoa n.k


Mh Rais amesema uoga ni hatari kuliko ugonjwa wenyewe. Ameshauri tuchukue tahadhari zinazotolewa na Wataalamu lakini tusitishike. Rais ameonya pia wanaosambaza habari za uzushi kuwa watafutwe na washughulikiwe. Kwa hili ninampongeza mh Rais kwani kila mtu alikuwa anaandika anachokitaka.


Mwisho Rais amekemea vikali kufanya upuliziaji wa dawa kwenye miji na magari . Amesema hii haisaidii. Ameenda mbali kwa kusema hawezi kutangaza kuiweka lockdown DSM. Binafsi ninampongeza Mh Rais kwa kuwa amesaidia kuweka sawa suala la ubaguzi lililokuwa limeanza kujitokeza kwani ni wiki iliyopita tu moja ya wateule wake alionekana mbele ya camera akisema watu wa Dar Es salama muwakimbie na msiwakaribishe.


Mwisho ninampongeza mh Rais kwa kuonyesha msimamo wa kijasiri. Tutoke nje tukafanye kazi. Kukaa ndani ni hatari kuliko corona. Hivi Corona isipoisha wale wenzetu wa Kenya wataendelea kukaa ndani? Tupambane na corona tukiwa kazi ni na si kujifungia ndani. Ninaamini kwa kauli ya Mh Rais sasa vyuo na shule si MUDA mrefu masomo yataendelea.

#corona inaua chukua tahadhari
Kijijini Lali Ibaba.
 
Sijakuambia kuwa iko USA yote hata hiyo NY mbona imeendelea kwa muda mrefu sana unataka kuniambia walikuwa wameambukizwa wote?. Kwa taarifa yako tangu juzi wamarekani hawataki tena lockdown wanaandamana mitaani. Bado hatujapata mwarobani wa kumaliza tatizo hili sana sana ni hali ya hewa na immune ya MTU husika. Utaona next month maambukizi US yatapungua kwa sababu ya mabadiriko ya hali ya hewa toka baridi kwenye kwenye joto. Hapa TZ tunatoka joto kwenda baridi hivyo maambukizi yanaweza ongezeka ingawaje sisi immune yetu iko juu kidogo ukilinganisha na watu weupe hivyo inaweza saidia sana.
 

Na namba umeweka 😂 😂

Ungekuwa wa kwanza kusema kujifukiza inasaidia
 
Dakitari Faustine kamjibu mkulu
 
Subiri viwavi vya ufipa vije

Sent from my Infinix X624 using Tapatalk
 
Huyu mzee ni kiongozi mbovu, wa hovyo. Kwa alichoongea leo ni kwamba ana tatizo kubwa kuliko tunavyomdhania. Mungu tusaidie
 
Jamani madaktari Bingwa na Ma professor mko wapi? Mnaacha siasa inatawala badala ya ninyi kuokoa Jahazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao wanasiasa ndiyo hawatai kuwapa nafasi. Hat angetokea msomi akazungumza jambo la kisayansi kensho anaweza kujikuta yuko rumande. Na mbaya zaidi wananchi wa Tanzania hawana msaada wowote kwa mtu alikyekuwa anawapigania anaponyanyaswa. Hivi mtu anayeamini virus wa corona hukaa kwanza puani na kooni na unaweza kuwaua kwa kujifukiza utafanya nini kumbadilisha? Hivi mtu anayeamini kuwa chlorine haiwezi kuuwa virus utafanya nini kumbadilisha kwa muda mfupi? Na akipewa facts za kisayansi atazikubali?
 
Hapo lazima akope sehemu nyingine ili alipe deni la.zamani kwa matumizi ya ovyo kama kununua viongozi wa chadema.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…