Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Kwani Rwanda ina watu wangapi mkuu? Wagonjwa 147 kwa watu 12 mil na wagonjwa 284 kwa watu 56 mil. Ni wapi ugonjwa uko mwingi? Kama hujui statistics kaa kimya.
Acha comparison za kipuuzi unajua Uganda ina watu 45 million na inawagonjwa 61 na 45 wameshapona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu kufanya ziara kwenye mochwari zetu ujionee

Jr[emoji769]

Mzee wa Fumigation ya kuua Virusi vya Corona keshatangaza Hali ya hatari: USIKANYAGE DAR BAKI HUKOHUKO MAANA WATU WANAPUKUTIKA KAKUKU!!!
 
PM ndo wakuamini.kwa sababu yupo site (vitani) huyo mwingne akawadanganye akina ngosha wenye IQ ndogo.
 
wazo langu lilikuwa kama tukifika cases 400 tufunge dar kwa wiki tatu. Ila naheshimu maamuzi ya mkuu wa nchi. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kuna ndugu yangu kanipigia simu anasema anadalili tano za corona na labda mbili kati ya zote ndio hana, hakina anasema anahis anayo, alichonisisistiza kwamba lockdown ni ya lazima na wanaosema watu watakufa njaa anasema watu watachelewa kula ila hawata kufa na njaa amekubali mateso ya covid 19 aisee


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
JokaKuu,
Sure... tena Mkapa sio tu alipewa hatua za kubana matumizi bali pia alipewa vipaumbele!

Ni kutokana na vipaumbele alivyopewa na mabeberu, ndipo ikaanzishwa MKUKUTA ili kuhakikisha yale yaliyotakiwa na mabeberu yanafanyika!

Shule za Kata kwa mfano, ni matunda ya hayo mashariki baada ya kuambiwa ili muingie kwenye program, basi muhakikishe kunakuwa na access to education!

Mambo yalikuwa mengi, and in fact, hata hizi kelele za Zahanati sijui elfu ngapi tunazopigiwa kelele awamu ya tano, na zenyewe msingi wake ndo yale yale masharti ambayo kutokana na ufinyu wa bajeti, ilibidi kutekeleza sharti moja baada ya lingine... awamu kwa awamu!!

Na kama ulivyosema, WB hawawezi kutoa msamaha bila masharti, na isitoshe kwa sasa wanaangalia sana policy response to coronavirus.

Kwamba, wakati Magu anafikiria kutaka kufutiwa madeni, je serikali kama serikali inayo fiscal and monetary policy to respond the situation?! It's obvious private sector inaathirika... je, serikali imefanya chochote kukabiliana na hiyo hali, kama vile kupunguza riba kwenye mabenki, kufanya tax exemption au angalau kuwapunguzia kodi... au kama ambavyo walifanya Stanibic Kenya kutoa grace period kwa debtors wake, nk!!!

I'm afraid usikute Magu wakati yeye anataka serikali zipate debt relief, serikali yake haina mpango wowote hadi sasa wa kuhakikisha sekta binafsi inaokolewa badala tu ya kusubiri kuwakamua kodi!
 
Si wewe unasema hadi Eid el fitri itagonga 4000,we mungu?
Mimi sijaomba mimi naeleza kwa rate hii ya maambukizi

Kenya ilikuwa na maambukizi mengi zaidi yetu na sasa tuko sawa na huenda tumeshaipita mbali sema tunaficha
 
Rebeca 83,
Kwani Malaria, HIV, TB, ajali za bodaboda, mimba vinaua watu wetu wangapi kwa siku wiki mwezi na mwaka? Mbona hatujifungii nyumbani kuepuka mbu?

Mbona hatupigi marufuku bodaboda kuwanusuru Vijana wetu na vifo? Tusifuate mkumbo eti kwakuwa wazungu wamejifungia.
 
norbit,
Tanzania ipo kwenye soft lockdown na ndio maana shughuli zingine muhimu za kiuchumi zaendelea kama kawaida.

Pia, katika soft lockdown hiyo mji wa Dar -es-Salaam unapaswa uendelee na shughuli zote za kiuchumi kuingiza mapato ya serikali yetu maskini.

Hiyo ni kutokana na sababu za kijiografia kwani tuna bandari inayopitisha mizigo ya nchi jirani, wataka tuzuie hiyo mizigo na tusipate ushuru?

Hizo nchi utajazo kama Uingereza wao mpaka sasa wana hard lockdown isipokuwa maduka ya mitaani na supermarkets ambapo kanuni zote za usafi mita 2 kati ya mtu na mtu zinafuatwa.

Nch zingine kama Ujerumani, Austria na Italia wameondoa hard Lock-down na kuweka soft lockdown ili shughuli za kiuchumi ziendelee.

Georgia siku ya Ijumaa wanarudisha shughuli kama gym na sehemu za kukata nywele kabisa.

Hard Lockdown inaleta taabu kiuchumi in a long run na ndio maana kule Marekani walianza vurugu siku nyingi huku wakiandamana na silaha wakitaka hard Lock-down iondolewe.

Kuhusu kwamba raisi anajificha huko Chatoi wewe una uhakika gani kama anajificha?

Inawezekana yeye pia yupo kwenye lockdown wewe na mimi hatufahamu.

Isitoshe, huyu ni kiongozi wa nchi hivyo hatua zote za kiusalama, na kiafya kwake na familia yake ni lazima zipewe kipaumbele mbali ya yote, huyu ni raia namba moja wa Tanzania.

Halafu, wewe wasema kwamba anatisha watu ni vipi anatisha? Ikiwa watu wanapotosha ukweli wa habari na kutoziamini taarifa za wizara husika ya afya wewe wataka upotoshaji wa taarifa uendelee ama?

Respect, man.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…