Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Kwani Rwanda ina watu wangapi mkuu? Wagonjwa 147 kwa watu 12 mil na wagonjwa 284 kwa watu 56 mil. Ni wapi ugonjwa uko mwingi? Kama hujui statistics kaa kimya.
Na wakati Tanzania ina wagonjwa 3, na Rwanda ina wagonjwa zaidi ya 50 ni kwamba wakati huo Rwanda ilikuwa na population kubwa kuliko Tanzania, au?!

Btw, ina maana hata suala la kutokuwepo watu waliokufa ni kwa sababu population yao ni ndogo ingawaje waathirika ni wengi, au?!

Population ya Uganda ni almost 2/3 ya population yetu lakini wakati wao confirmed cases ni 61, TZ 284! Kama hoja ni population, how come tena tumewapiga gap kubwa namna hiyo ambayo haiendani kabisa na tofauti ya population kati yetu?!

Endeleeni tu kujidanganya lakini ukweli ni kwamba, issue sio population bali ni namna gani watu walikuwa serious kwenye ku-respond. Both Uganda na Rwanda walikuwa very strict.
 
Kwani Malaria na TB na kipindupindu na vifo vya akinamama wanaojifungua ni vya kwisha leo? Mbona mnajitoa ufahamu. Iko siku watu watapata kitu kinachoitwa heard immunity. Hata mafua yanauwa watu lakini sisi hatufi kwa flu kwakuwa tuna kinga.
Mkuu umepotosha mno imebidi nikujibu:

1. Virusi vya Corona ni aina mpya ambayo haijawahi kuonekana duniani. Mpaka sasa hakuna tiba wala chanjo iliyothibitishwa kutibu wala kujikinga. Magonjwa uliyoyataja aidha yana kinga au tiba yake ipo au yanazuilika.

2. Usambaaji wa virusi vya Corona ni wa kasi sana. Na hata mtu asiyeonyesha dalili bado ana uwezo wa kuambukiza wengine. Magonjwa uliyotaja usambaaji ni tofauti.

3. Madhara ya watu wengi kupata huu ugonjwa, hasa kwa wakati mmoja ni makubwa sana. Ukiacha athari za kiafya, hata sekta ya afya inaweza kuelemewa sana.

4. Watu weusi wanaathirika sawa na watu wa mataifa mengine. Hata hao waliofariki Tanzania ni watu weusi. HAKUNA KINGA KWA MTU MWEUSi. Acha kupotosha watu!
 
Tuonyesheni mfano jinsi ya kujifusha na mavi ya tembo😀
Tunamalizia zoezi muhimu kwa afya
IMG_20200422_235057.jpg
 
JK alisema za kuambiwa nami naongeza za kuona ( leo chato hatukuona yeyote alievaa mask/ barakoa) changanya na za kwako.

Pia kauli ya mkuu kuponda usalama barakoa kwa hisia mtandaoni! Kirusi cha corona huishi juu ya nguo na plastic kwa siku 2-4!

Logistic mzigo kwa ndenge si chini ya siku 7!!! Chukua tahadhari kadiri ya nafasi yako corona inaua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh Raisi amemaanisha wamepona 100 tangu ungonjwa uingie Nchini
 
Acheni Umavi kwani amfatili vyombo vya habari vya kimataifa kuhusu Mask zilizopelekwa USA kutoka China...

Mnachojua ni Umbea tuuu na udaku.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mask na vifaa vingine toka China vinalalamikiwa siku nyingi na nchi kibao za ulaya, sema sababu kaongea JPM yamejaa mapumbavu kibao yanaitana kutiana ujinga sababu ya chuki kwa JPM. Tatizo wanafatilia habari za hapa tu halafu wanajiona wajanja.
 
Mkuu mask na vifaa vingine toka China vinalalamikiwa siku nyingi na nchi kibao za ulaya, sema sababu kaongea JPM yamejaa mapumbavu kibao yanaitana kutiana ujinga sababu ya chuki kwa JPM. Tatizo wanafatilia habari za hapa tu halafu wanajiona wajanja.
Jiulize kwanini anachukiwa!
Jiepushe na majibu ya "kawabana wapiga dili" maana kina rostam wanapiga mulemule!!
 
Chige,
Very strick in what, shule na vyuo vimefungwa, kunawa tumeambiwa tunawe, barakoa na sanitizers tulifundishwa, distancing tumeambiwa pia. Kwahiyo ulitaka watu wafungiwe ndani wale mafi yao. You have to think globally and act locally, wewe unadhani hii hand to mouth ya watanzania ingemudu lockdown ya siku 14 bila ya kutoka nje?. Tunazo pesa za kutoa ruzuku kwa watu wetu wote wanaoishi leo kwa leo?

Mko brain washed kiasi hiki?

Nchi zetu hasa hizo unazozisifia hazina record ya kusema ukweli siku zote. Takwimu zao sio za kuaminika sana Kama unavyotaka kuwaaminisha watu.
 
Nilichangia hii kwenye uzi mwingine:

Hii itakua unpopular opinion ila nitasema ninachofikiri.

Pasi na chembe ya shaka Covid-19 ni ugonjwa hatari ila, kwa mawazo yangu, dunia nzima ime overact na jinsi ya kukabiliana na huu mlipuko.

Kinachoendelea sasa ni mashindano ya kutoa takwimu za waathirika na kutishana. Bado death rate ya corona sio ya kutisha sana kiasi cha kufanya shughuli zingine zote zisimame. Ikumbukwe watu walikua wanakufa kabla ya corona na wataendelea hata baada ya corona, it's the circle of life. Sasa kila anayefariki ni corona magonjwa mengine yote yamepotea ghafla. Hata mimi nikifa kwa corona hakuna sababu ya maisha ya wengine kusimama.

Nadhani kuchukua tahadhari tu ingetosha ila sio kusimamisha maisha ya watu juhudi ambazo hazionekani kuzaa matunda yoyote, mwishoe watu watasema potelea mbali na kurudi makazini. Dawa au chanjo ya corona isipopatikana hadi mwakani watu wataendelea kukaa ndani mwaka mzima?

Sasa bongo nao watu wanataka kila kitu kisimame sababu corona imeua watu watano toka ianze, really? I can assure you malaria imeua wengi zaidi ya hao in the last 24hrs.

According to Wikipedia, Mortality rate - Wikipedia, inakadiriwa watu laki moja na nusu hufa kila siku kwa sababu mbali mbali duniani. Sasa iweje corona iliyoua watu karibu watu laki moja na nusu kwa miezi mitatu isimamishe dunia.

www.worldometers.info/coronavirus/
Confirmed
2,173,432
Recovered
554,786
Deaths
146,291

Media nyingi zinatoa idadi ya vifo na waathrika wapya tu hawasemi wangapi wamepona. Nia ni kujazana hofu.

Come June maisha yataendelea aidha chanjo imepatikana au lah, vinginevyo we're facing economy Crashdown beyond repair. Kilichofanyika so far ni kuua sisimizi kwa nyundo.
 
Mi nadhani Jiji kama Dar linategemea sanaa mikoa mingine hasa kwenye upande wa mazao ya chakula so kwa upande wangu sioni effects kubwa zaidi ya kiuchumi ambayo the whole country inaexperiance kwa kipindi hiki.
Umeangalia upande mmoja ndugu ukuaji wa miji maeneo mengi ya Africa ulipewa jina " Primate city growths" kutokana na kukua sana kwa mji mmoja kuliko mingine ila at the expense of other regions.
Mikoa inalitunza Jiji la Dar es Salaam na Dar es Salaam inaitunza mikoa.
 
'm afraid usikute Magu wakati yeye anataka serikali zipate debt relief, serikali yake haina mpango wowote hadi sasa wa kuhakikisha sekta binafsi inaokolewa badala tu ya kusubiri kuwakamua kodi!
Correct!
 
Back
Top Bottom