Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Jiulize kwanini anachukiwa!
Jiepushe na majibu ya "kawabana wapiga dili" maana kina rostam wanapiga mulemule!!
Tatizo sio kuchukiwa, hata wewe kuna watu kibao wanakuchukia kwasababu ya tabia zisizoeleweka, ila mnaleta utani na upumbavu kwenye ishu serious. Anyway unafikiri chuki zinampunguzia nini?, Watu wenyewe ma keyboard warriors.
 
SueIsmael,
Mkuu kifo ni kifo hata kikiwa Cha malaria au mzazi. Hebu ona idadi inayouliwa na Corona na ile inayouliwa na Malaria nchini uone ni ipi kubwa zaidi kwa siku. Idadi kubwa ya watu wanaougua COVID-19 huwa wanapona wenyewe huko majumbani na hospitali.

Wenyewe wanapiga chafya tu siku mbili, wengine wanakohoa tu siku 3 basi wanapata nafuu ispokuwa wale wenye matatizo mengine Kama uzee, kisukari, pressure au pumu. Hawa ndio watu ambao tungewashauri wawe na lockdown kwakuwa sio wengi na hata serikali ingeweza kuwahudumia. Waliobaki wote hawafi kwa CORONA hapa nchini.
 
Isitoshe, huyu ni kiongozi wa nchi hivyo hatua zote za kiusalama, na kiafya kwake na familia yake ni lazima zipewe kipaumbele mbali ya yote, huyu ni raia namba moja wa Tanzania.
Utterly nonsense stemming from self-enslavement mindedness.
 
Utterly nonsense stemming from self-enslavement mindedness.

It is you, who has the self-enslavement mindedness.

Always stem toxic views.

This lockdown will somehow help you with detoxing steps and how to go about them.
 
Tanzania ipo kwenye soft lockdown na ndio maana shughuli zingine muhimu za kiuchumi zaendelea kama kawaida.

Pia, katika soft lockdown hiyo mji wa Dar -es-Salaam unapaswa uendelee na shughuli zote za kiuchumi kuingiza mapato ya serikali yetu maskini.

Hiyo ni kutokana na sababu za kijiografia kwani tuna bandari inayopitisha mizigo ya nchi jirani, wataka tuzuie hiyo mizigo na tusipate ushuru?

Hizo nchi utajazo kama Uingereza wao mpaka sasa wana hard lockdown isipokuwa maduka ya mitaani na supermarkets ambapo kanuni zote za usafi mita 2 kati ya mtu na mtu zinafuatwa.

Nch zingine kama Ujerumani, Austria na Italia wameondoa hard Lock-down na kuweka soft lockdown ili shughuli za kiuchumi ziendelee.

Georgia siku ya Ijumaa wanarudisha shughuli kama gym na sehemu za kukata nywele kabisa.

Hard Lockdown inaleta taabu kiuchumi in a long run na ndio maana kule Marekani walianza vurugu siku nyingi huku wakiandamana na silaha wakitaka hard Lock-down iondolewe.

Kuhusu kwamba raisi anajificha huko Chatoi wewe una uhakika gani kama anajificha?

Inawezekana yeye pia yupo kwenye lockdown wewe na mimi hatufahamu.

Isitoshe, huyu ni kiongozi wa nchi hivyo hatua zote za kiusalama, na kiafya kwake na familia yake ni lazima zipewe kipaumbele mbali ya yote, huyu ni raia namba moja wa Tanzania.

Halafu, wewe wasema kwamba anatisha watu ni vipi anatisha? Ikiwa watu wanapotosha ukweli wa habari na kutoziamini taarifa za wizara husika ya afya wewe wataka upotoshaji wa taarifa uendelee ama?

Respect, man.
Kwanza ninavyo hisi huwezi ku-classifie watu wa nchi moja, huyu ni first class citizen so he needs special protection na mwengine ni second class citizen umu-exposed deadly contegeos deseas ambayo hayana dawa na longterm side effects are unknown.
Kuhusu kujificha atuambie tu kama yupo annual holiday,
Umesema tupo kwenye soft lockdown, umetafautiana na Rais, yeye kasema no lockdown at all.
Jengine German, Spain, Italy ku-lift restriction, wamefanya hivyo kwa sababu they already reach the peak sasa wana-flatting the curve (haya ni kama virus wa flu, wa nakuja ghafla wanaondoka ghafla) Baada ya kuwa full lock down for more than 8 weeks, ni lazima wapunguze some restrictions kwa umakini wa hali ya juu, jengine maafa yaliotokea Italy na Spain sababu moja wapo ni kucherewesha restrictions.
 
Hapa tulipofika kila mmoja Yarab nafsi yake. Fullstop. Akili za kuambiwa changanya na zako
 
kavulata,
Ni kweli kuwa malaria ni hatari na inaua. Hiyo ina vita yake na japo hatujafanikiwa kuishinda ila kwa kuwa kuna kinga, chanjo na tiba, inaweza kudhibitiwa na haiathiri mfumo wetu wa afya kwa kiasi cha kuielemea kabisa. Pili kila ugonjwa unauzito wake na mapambano yake, hatudogodishi.

Mpaka sasa hivi sijui tumeshafanya vipimo kiasi gani vya Corona, maana itatupa ratio ya kasi ya maambukizi. Wenzetu namba ni kubwa pia kwa sababu wanafanya vipimo kwa wingi. Duniani kote testing kits ni tatizo na nchi chache zinafanya mass testing.

Hivyo hata kwa Tanzania, uwezekano wa walio ambukizwa ni wengi zaidi kuliko waliopimwa na kuthibitika. Ni kweli pia kuna wanaoweza kupona wengi zaidi kuliko watakaopoteza maisha. Lakini hilo siyo tatizo pekee. Unajua Tanzania ina ventilators ngapi? ICU ngapi? Technical staff wangapi katika health centres zetu?

Sasa kwa kasi ya huu ugonjwa, piga picha watu mia moja kwa mara moja wanahitaji ventilators. Tutakuwa na uwezo wa kuwahudumia wote kwa wakati mmoja? Hii ndio hoja ya flattening the curve. Kuumwa tunaweza kuupata wote, ila tukiumwa wengi kwa wakati mmoja, tutaweza kuhudumiwa?!
 
Jaribu kufanya ziara kwenye mochwari zetu ujionee

Jr[emoji769]

Hata kama kuna idadi kubwa ya maiti huko mochwari lakini kwa hili ambalo magufuli amelifanya la kutozuia watu kufanya shughuli za kiuchumi, kwa kweli anastahili pongezi huyu jamaa hata kama hatumpendi jamani lakini ni Rais mwenye maono mapana sana.
 
norbit,

Mkuiu, tuwe waelewa kidogo.

Kwanza, raisi Magufuli ni raia namba moja na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania.

Kutokana na hivyo basi, afya yake katika kipindi hiki kigumu ni lazima iiangaliwe na kupewa uzito wake kama ambavyo viongozi mbalimbali kama Donald Trump na Boris Jonnson na wengine ambao wameangaliwa afya zao na sasa wanaendelea na shughuli.

Waziri mkuu wa UK Boris Johnson aliwekwa ICU na akatoka ndani ya siku saba tu ni hiyo ni kwasababu huyu ni mtu muhimu anaendesha serikali.

Raisi Magufuli yaonekana iliamuliwa apumzike kwa sababu ambazo serikali inazo za kiusalama zaidi.

Pili Raisi amesema wazi kwamba Dar hakuna lockdown kutokana na kwamba ni mji wa kibiashara.

Hiyo ni soft lockdown kwasababu sehemu zingine kama mashule, madrasa na chekechea kumefungwa na sehemu zingine mambo yanaendelea kama kawaida.

Pia ni soft lockdown kwasababu njia ya usafiri wa anga ni ndege za mizogo tu ndizo zinaruhusiwa kuruka na kutua lakini si abiria.

Mwisho, Tanzania haiwezi kuiga hizo lockdown za nchi zilizoendelea hatujafika huko, ila tunafuata miongozo yote ya WHO kama nchi mwanachama.
 
SueIsmael,
Sio kweli ulichokiandika hapa..huu ugonjwa pamoja na kwamba unauwa na watu weusi lakini rate ya vifo kwa watu wenye asili ya Africa ni ndogo sana kulinganisha na wazungu ambao kinga zao za mwili zi nategemea sana msaada wa dawa za Hospital tofaut na sisi ambao kinga zetu zinapewa nguvu sana na mfumo wetu wa lishe na vyakula tunavyokula.
 
Kuna raisi na rahisi, sijui tuna rais au rahisi? Bado natafakari...Maana wahenga walisema "rahisi ni ghali".
 
Titicomb,
Ni bora kuwa jenga watu katika imani na ujasiri wa kukabiliana na tatizo kuliko kuwajengea hofu na uoga wa hatari iliyoko mbele yao. Yani hii insue ya covid-19 ni kwamba the strongest will survive lakini ambao kinga zao ziko chini wajiandae kudondoka maana hakuna chanjo wala tiba mpaka muda huu.
 
Bursting,
Sijadanganya na bado ninasimamia nilichosema, kinga ya mwili haitegemei rangi ya mtu bali hutegemeana na aina ya maisha, umri, vyakula, magonjwa, nk aliyonayo mtu. Hizo nchi nyingine zilizoathiriwa kuna watu weusi pia ambao wamefariki.

Pili, bara la Afrika limekumbwa na hili janga hivi karibuni na hivyo ni bado ni mapema kusema tutaathirika kiasi gani.

Halafu, upimaji na ufuatiliaji wa kesi za maambukizi bado viko chini na hivyo kufahamu uhalisia wa maambukizi kwa asilimia mia moja ni changamoto. Tuombe Mungu tusiathirike kama Bara la Ulaya ila muda pekee ndio utasema.
 
Kama mabeberu wanaweza kupandikiza virus kwenye baraakoa na kutupaatia msaada, kumbe barakoa zinatunza virus

Sent using Jamii Forums mobile app

Huo Ndio uhalisia ingawa walengwa hawapendi kuchukuliwa katika huo mtazamo. Usidhani kila msaada mnaopewa ni kwa ajili ya huruma za kibinadamu, misaada mingine ni chuki na maangamizo kutoka kwa baadhi ya wazungu na usifikiri unapendwa kiasi hicho na hao mabeberu
 
..misamaha ya madeni huwa inaambatana na masharti ya kibajeti na vipaumbele ktk matumizi ya serikali.

..sijui ulikuwa na umri gani ktk awamu ya kwanza ya Mzee Mkapa. Lakini kuna hatua za kubana matumizi serikali ililazimishwa kuzichukua ili ku-qualify kuingia ktk debt relief program.

..sina uhakika kama Jpm atakubali usimamizi na masharti makali ya mabeberu wa WB na IMF.
Moja ya masharti ilikuwa 'devaluation'', kusimamisha ajira (hiring freeze), Gov. restructuring etc.
Hakuna namna ila kukubaliana nao kama walivyokubali masharti ya watoto wa kike. Hao ndio wenye dunia

Hili la ' no lock-down kwaa Dar na Tanzania ' halihitaji nguvu wala misuli, litakuja lenyewe tu bila kupenda

Spain na Italy walikuwa wakaidi yakawakuta. Borison wa UK alikuwa kaidi yakamkuta hadi aliporudia ICU

Kwa Tanzania hakuhitajiki Tangazo, lockdown itatokea naturally, subirini tu ni suala la wakati.

Kitu kimoja cha kukumbuka, hili ni balaa asitokee mtu akakudanganya, Ni balaa kubwa sana
 
Back
Top Bottom