Wakuu poleni na majukumu na wale waliondokewa na ndugu na jamaa katika kipindi hiki Mungu awatie nguvu.
Moja kwa moja kwenye Mada, Wakuu Jana mzee baba kaeleza kuwa tutumie na vitu vya asili ikiwemo kujifukizia kupambana na huyu Mwamba fagia fagia Covid19. Nikisindikizwa na Maandiko matakatifu kutoka kitabu Cha Yeremia 46:11".....pandeni Gileadi enyi watu wa Misri,mkachukue dawa ya marhamu,mmetumia dawa nyingi bure, hakuna kitakachowaponya nyinyi'. Ifuatayo ni baadhi ya mimea ambayo tunaweza kuitumia kipindi hiki cha Covid19 ikaleta nafuu.
1. Kitunguu swaumu(Allium sativum) kwa matibabu ya Kikohozi,mafua,madonda ya Koo na sinusitis.
I.Kula kikonyo kimoja cha kitunguu swaumu mara tatu kwa siku.
II.Tumia kijiko kimoja cha chai Cha asali ya kitunguu swaumu kila baada ya saa chache.
III.Tumia kijiko Cha chai kimoja cha mafuta ya kitunguu swaumu mara 6 kwa siku.
IV.Watoto wanaweza kutumia kijiko kimoja cha chai Cha mchanganyiko wa dawa ya Kikohozi ya kitunguu swaumu kila baada ya saa chache.
2. Artemisia annua anamed (A3). Kikohozi mafua na sinusitis.
I.Vuta mvuke kutoka kwenye chai ya moto ya Artemisia kwa dakika kumi mara tatu kwa siku. Chai isiwe na joto kali wakati wa kuvuta mvuke.
3. Limau (Citrus limon)
Homa.
Kuliko kunywa Asprin ni Bora zaidi kuimarisha mfumo wa kinga!.
Kunywa juisi ya Limau mara tatu kwa siku kwenye kikombe kimoja kikubwa cha mil 5000.Usichemshe juisi,utaharibu vitamin C.
4. Kitunguu maji (Allium cepa)
Kikohozi na madonda koo. Changanya kikombe Cha vitunguu vilivyokatwakatwa na kikombe Cha maji,koroga,kunywa kwa siku mzima.
5. Mranaa (Detura stramonium).
Kushindwa kupumua. majani huvutwa Kama sigara kwa ajili ya kusaidia kupumua pamoja na kutibu pumu(sio sugu.Utomvu unatumika kutibu sugu),majani mengine Ni majani makavu ya mkaratusi mil150,majani makavu ya mpapai mil700. Mambo ni mengi mimea mingine mtaongezea wakuu kwa faida ya wale wenzangu na Mimi pangu pakavu.
Onyo: Usibebe ukaipeleka kwenye blogu yako.
NB: Endelea kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya na sio wanasiasa.Hatma yako iko mikononi mwako.