Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Vika.haba nyie mmeachwa mseme sana na sasa mnavuka mipaka, wacha muanze kushughulikiwa sasa mshike adabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona mwachukia HIVI mitazamo tofauti na YENU wajameni. Rais ni binadamu tu, pamoja na mavyombo yote mbona keshawahi chemshaga kwingi tu. Hebu jiruhusuni kutulia ili pamoja na mengine muweze kutafakari.

Kwenye hali ya majanga kama hii panahitajika utulivu zaidi wa akili na sio kulazimisha maamuzi kwa kutumia dola.

Amen
 
Habarini za wakati huu!

Kwanza kabisa poleni na harakati zote za maisha na tuendelee kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Nimesikitika Sana kuona maneno haya yanatoka kwa kiongozi wa nchi yetu kwamba huenda hata hio misaada tunayopokea kutoka China kwa Jac Ma na mataifa mengine misaada yao imekua injected corona viruses.

Kwahali ya kawaida tu je! Wao Kama wafadhili wakisikia kauli Kama hii watajisikiaje! Kuna maisha baada ya Corona! Je mataifa hayo ambao kwa muda mrefu yamekua msaada kwa maendeleo ya taifa hili wanajisikiaje baada ya kusikia maneno haya.

Huku Ni kutafuta kichaka Cha kujifichia na kulaumu watu. Raisi umeonyesha kushindwa tangu hapo mwanzo kukabiliana na hili gonjwa la Corona.

Wafadhili wetu na wote wanaolisaidia taifa hili kukabiliana na Corona waombe radhi kutokana na kauli hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu wanabodi, hotuba ya jana ya mh raisi ambayo ilikua ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi, ukizingatia watu walitamani kusikia neno la faraja kuhusu hali halisi ya ugonjwa ulivyo nchini hasa baada ya mkanganyinyiko na uvumi wa mambo mengi hasa baada ya viongozi wa mbalimbali wa serikali kutoa kauli na matamko yanayokinzana.

Mfano mkuu wa mkoa wa Mbeya kuagiza bar ziwe zinafungwa saa tatu usiku na baadae kufuta kauli yake, mkuu wa wilaya ya Iringa kusema wananhi wajitenge na watu kutoka Dar na baadae kufuta kauli, mkuu wa mkoa wa Dar kutaja majiana ya wagonjwa na baadae kushambuliwa na watu mbalimbali , baadhi ya makanisa kusitisha misa kwa muda kinyume na msimamo wa serikali n.k.

Ndugu zangu baada ya huo mkanganyiko nilitegemea jana raisi kuweka mambo sawa, kwa kuweka miongozo ya serikali katika mambo yenye mkanganyiko yanayowachanganya wananchi badala yake rasi alizidi kutuchanganya na mpaka na hakutoa majibu na miongozo ya madukuduku yetu au mwelekeo wa pamoja kama serikali. Mfano

1.Hatutakiwi kupuliza dawa za kemikali
Tofauti na tunavyoona kwa wenzetu huko nj wakipuliza dawa ku disinfect sehemu mbalimbali hasa zinazokusanya watu wengi raisi kasema tusifanye hivyo, na kufanya hivyo ni upumbafu.
Naamini raisi ana wataalam mbali mbali ambao wanaweza kumshauri vizuri kabisa hasa ukizingatia hili ni janga la kimataifa kuna miongozo ya shirika la afya Duniani kusiana na upuliziaji dawa nk, je raisi alisema vile kutokana na ushauri au ni mawazo yake? na mbadala ni nini?
Hapa katuacha wananchi wengi na maswali yasiyo na majibu

2.Usalama wa barakoa
Katika hotuba yake jana mh raisi alisema barakoa tunazovaa hasa zinazotolewa kama msaada zinaweza kua na visusi vya corona. ndugu zangu hapa wananchi tulio wengi ndo tumeendelea kuchanganyikiwa zaidi, tumekua tukielezwa na viongozi mbalimbali hasa waziri wa afya tuvae barakoa kila mahali ili tujikinge na maambukizi, mkuu wa mkoa wa Dar alisema ni amri asievaa atakamatwa.

Jana raisi katwambia sio salama, je, taarifa kapewa na nani? je kuna utafiti wowote uliofanya kuthibitisha madai ya raisi? kwa nini tusizipeleke barakoa hizi kwa mkemia mkuu wa serikali zikapimwa? kwa nini tunaendelea kupokea msaada wa vifaa vya kujikinga na corona zikiwemo barakoa?

3.mkanganyiko wa idadi ya walioambukzwa
Huku mtaani kuna mkanganyiko wa watu walioambukizwa corona Tanzania, wengi wakisema namba zimepikwa hasa baada ya kutofuatwa kwa mfumo wa WHO wa kutoa taarifa, taarifa zinazofuata mfumo wao wa taarifa ukiangalia nchi nyingi hasa za jrani, taarifa zao ziza idadi ya walioambukizwa, idadi ya vifo, jumla ya waliopimwa na idadi ya waliopona. jana raisi amesema ana wasi wasi na taarifa za wizara ya afya zinazotolewa za idadi walioambukizwa, akisema kwa takwimu zake yeye waliopona ni 100 kuku wizara ya afya ikitwambia ni 11.

lakini mh raisi hajatwambia takwimu zake za walioambukizwa na waliokufa, tumuamini nani? takwimu raisi anatoa wapi? na raisi anasema watoe taarifa za kweli...za ukweli ni zipi?

5.Tusitenge watu
Wakati Dunia nzima, hasa kutokana na ushauri wa shirika la afya duniani kua ndani ya siku 14 ndo tunaweza kua na uhakika kama mtu ana maambukizi au la hasa kutokana na utafiti wa watu kuonekana hawana maambukizi na kuonekana na maambukizi baadae, iliamuliwa watu wanaohisiwa kutengwa kwa mda wa siku 14 ili kujiridhisha kuwa hawana au wanao, raisi anasema ni ni kuwaste resorces! je njia mbadala ni ipi? hapa tumeendelea kuchanganyikiwa

6.Tiba mbadala

Wakati naibu waziri wa afya akitwambia njia mbadala kama kujifukiza, malimao nk si salama, mh raisi ametwambia tuzitumie, je kashauriwa na nani?

Hitimisho

Kwa maoni yangu binafsi, tuache kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaalam, tunawachanganya wananchi kabisa, waziri anasema vaa barakoa raisi anasema zina corona, sisi wananchi tunamwelewa nani? ukiangalia nchi zote Duniani vita hii inaongozwa na mawaziri wa afya, ushauri wa mambo ya kinga n.k cha msingi iwepo transparency, tupime watu kwa wingi wenye maambukzi watibiwe, nchi jirani wameaanza kutunyanyapaa kua tunawapelekea maambukizi kwao hii ni baada ya madreva wengi kutoka Tanzania kwenda Uganda na Rwanda kukutwa na maambukizi.
Huu sio wakati wa siasa hata kdogo, tuwaache wataalam wetu wafanye kazi yao
 
Rais ni wetu, Sisi ni Watanzania, nchi ni yetu

Hata tufanye nini kwa sasa hatuwezi ku-change chochote tutulie kila mmoja atumie njia zake kulinda uhai wake

Wanasiasa kamwe hawawezi kuleta tija kwenye uhai wetu. Tuchukueni hatua.
 
Waliofanya fumigation siyo wajinga. Utafiti uliofanywa na Marekani, unaonesha mabwawa ya kuogelea yaliyowekwa chlorine, virus au wanakufa au wanakuwa inactive.

Na wanaoogelea kwenye mabwawa wamehakimishiwa kuwa kama maji ya kwenye bwawa yamewekwa chlorine, hata kama mmojawapo wa wanaoogelea akawa ana virus vya corona, hawezi kuwaambukiza wengine kwa kupitia maji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna Mama nilikutana naye kwenye hizi Famasi kubwa akawa anaulizia water guard
Waliofanya fumigation siyo wajinga. Utafiti uliofanywa na Marekani, unaonesha mabwawa ya kuogelea yaliyowekwa chlorine, virus au wanakufa au wanakuwa inactive.

Na wanaoogelea kwenye mabwawa wamehakimishiwa kuwa kama maji ya kwenye bwawa yamewekwa chlorine, hata kama mmojawapo wa wanaoogelea akawa ana virus vya corona, hawezi kuwaambukiza wengine kwa kupitia maji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna Mama nilikuta naye Famasi hizi kubwa akawa anaulizia water guard akambiwa zimeisha kumbe ni nzuri sana
 
Kila sehemu ukakasi tuu, Basi mimi ngoja nimwamini kigogo2014,

Jikinge na corona ata kwa kujivukiza kwa moshi wa mikaratusi or dance with us
EWJ8yoVXgAEtG9g.jpg
 
Unatakiwankutumia akili huyu amejifungia kwako na huyo aliyeko kwenye site na kiwashuhulikia .mfano wawazi ni sawasawa na mkulima juu ya mazao na yule anayenunua bidhaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spain Italy France wako lockdown mwezi wa pili huu lakini new cases 2000+ kila siku, 400+ deaths kila siku
Jambo la kujiuliza wanaambukizwa aje?
Waliambukizana tangu awali mkuu...Socialization ya hao na nyie huko ni tofauti munno.
 
Back
Top Bottom