Ndugu zangu wanabodi, hotuba ya jana ya mh raisi ambayo ilikua ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi, ukizingatia watu walitamani kusikia neno la faraja kuhusu hali halisi ya ugonjwa ulivyo nchini hasa baada ya mkanganyinyiko na uvumi wa mambo mengi hasa baada ya viongozi wa mbalimbali wa serikali kutoa kauli na matamko yanayokinzana.
Mfano mkuu wa mkoa wa Mbeya kuagiza bar ziwe zinafungwa saa tatu usiku na baadae kufuta kauli yake, mkuu wa wilaya ya Iringa kusema wananhi wajitenge na watu kutoka Dar na baadae kufuta kauli, mkuu wa mkoa wa Dar kutaja majiana ya wagonjwa na baadae kushambuliwa na watu mbalimbali , baadhi ya makanisa kusitisha misa kwa muda kinyume na msimamo wa serikali n.k.
Ndugu zangu baada ya huo mkanganyiko nilitegemea jana raisi kuweka mambo sawa, kwa kuweka miongozo ya serikali katika mambo yenye mkanganyiko yanayowachanganya wananchi badala yake rasi alizidi kutuchanganya na mpaka na hakutoa majibu na miongozo ya madukuduku yetu au mwelekeo wa pamoja kama serikali. Mfano
1.Hatutakiwi kupuliza dawa za kemikali
Tofauti na tunavyoona kwa wenzetu huko nj wakipuliza dawa ku disinfect sehemu mbalimbali hasa zinazokusanya watu wengi raisi kasema tusifanye hivyo, na kufanya hivyo ni upumbafu.
Naamini raisi ana wataalam mbali mbali ambao wanaweza kumshauri vizuri kabisa hasa ukizingatia hili ni janga la kimataifa kuna miongozo ya shirika la afya Duniani kusiana na upuliziaji dawa nk, je raisi alisema vile kutokana na ushauri au ni mawazo yake? na mbadala ni nini?
Hapa katuacha wananchi wengi na maswali yasiyo na majibu
2.Usalama wa barakoa
Katika hotuba yake jana mh raisi alisema barakoa tunazovaa hasa zinazotolewa kama msaada zinaweza kua na visusi vya corona. ndugu zangu hapa wananchi tulio wengi ndo tumeendelea kuchanganyikiwa zaidi, tumekua tukielezwa na viongozi mbalimbali hasa waziri wa afya tuvae barakoa kila mahali ili tujikinge na maambukizi, mkuu wa mkoa wa Dar alisema ni amri asievaa atakamatwa.
Jana raisi katwambia sio salama, je, taarifa kapewa na nani? je kuna utafiti wowote uliofanya kuthibitisha madai ya raisi? kwa nini tusizipeleke barakoa hizi kwa mkemia mkuu wa serikali zikapimwa? kwa nini tunaendelea kupokea msaada wa vifaa vya kujikinga na corona zikiwemo barakoa?
3.mkanganyiko wa idadi ya walioambukzwa
Huku mtaani kuna mkanganyiko wa watu walioambukizwa corona Tanzania, wengi wakisema namba zimepikwa hasa baada ya kutofuatwa kwa mfumo wa WHO wa kutoa taarifa, taarifa zinazofuata mfumo wao wa taarifa ukiangalia nchi nyingi hasa za jrani, taarifa zao ziza idadi ya walioambukizwa, idadi ya vifo, jumla ya waliopimwa na idadi ya waliopona. jana raisi amesema ana wasi wasi na taarifa za wizara ya afya zinazotolewa za idadi walioambukizwa, akisema kwa takwimu zake yeye waliopona ni 100 kuku wizara ya afya ikitwambia ni 11.
lakini mh raisi hajatwambia takwimu zake za walioambukizwa na waliokufa, tumuamini nani? takwimu raisi anatoa wapi? na raisi anasema watoe taarifa za kweli...za ukweli ni zipi?
5.Tusitenge watu
Wakati Dunia nzima, hasa kutokana na ushauri wa shirika la afya duniani kua ndani ya siku 14 ndo tunaweza kua na uhakika kama mtu ana maambukizi au la hasa kutokana na utafiti wa watu kuonekana hawana maambukizi na kuonekana na maambukizi baadae, iliamuliwa watu wanaohisiwa kutengwa kwa mda wa siku 14 ili kujiridhisha kuwa hawana au wanao, raisi anasema ni ni kuwaste resorces! je njia mbadala ni ipi? hapa tumeendelea kuchanganyikiwa
6.Tiba mbadala
Wakati naibu waziri wa afya akitwambia njia mbadala kama kujifukiza, malimao nk si salama, mh raisi ametwambia tuzitumie, je kashauriwa na nani?
Hitimisho
Kwa maoni yangu binafsi, tuache kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaalam, tunawachanganya wananchi kabisa, waziri anasema vaa barakoa raisi anasema zina corona, sisi wananchi tunamwelewa nani? ukiangalia nchi zote Duniani vita hii inaongozwa na mawaziri wa afya, ushauri wa mambo ya kinga n.k cha msingi iwepo transparency, tupime watu kwa wingi wenye maambukzi watibiwe, nchi jirani wameaanza kutunyanyapaa kua tunawapelekea maambukizi kwao hii ni baada ya madreva wengi kutoka Tanzania kwenda Uganda na Rwanda kukutwa na maambukizi.
Huu sio wakati wa siasa hata kdogo, tuwaache wataalam wetu wafanye kazi yao