Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

IGP ana maagizo toka juu kuwashughulikia wapinzani hana nafasi ya ushauri wako. Labda ungeshauri taasisi zingine zilizoalikwa kwenye mkutano husika.
Raisi kaongelea FUMIGATION MASHINES (huvaliwa mgongoni) na hutoa aidha maji (liquid) au vapour.

na zile za ROSTAM ni SANITIZING MASHINES hutoa vapour tuu.

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
Na waliopuliziwa nao wapuuzi duh, JPM katisha kwa kweli...Watanzania tupambane kivyetu.
Raisi kaongelea FUMIGATION MASHINES (huvaliwa mgongoni) na hutoa aidha maji (liquid) au vapour.

na zile za ROSTAM ni SANITIZING MASHINES hutoa vapour tuu.

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
bado hujafiwa wewe ukifiwa na uwapendao wakazikwa kwenye makaburi ambayo wewe hutaweza kufika ndio utatia akili

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata ikitokea hivyo hutapaswa kumlaumu kiongozi yeyote, kwani ulikuwa na uwezo wa kujifungia ndani wewe na familia yako msitoke nje kabisa. Nini kinakufanya usubiri mtu akumbie ujifungie ndani? Halafu unasema una akili.
 
digba sowey,

Mkuu Magufuli yupo likizo? mbona mwezi mzima yupo Chato? unachosahau ni kwamba magufuli is entitled to tell the citizens anafanya nini Chato all these days? Hata sisi tunafanya kazi ambazo ukiwa hata home unaweza fanya ila unaenda station yako ya kazi, ofisi ni ofisi mkuu, kama chato ndio imebadilika imekuwa ikulu sawa ila anatakiwa awe ikulu saivi.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hapo namba 4 utafiti umeufanya lini kujuwa kuwa hakuna tofauti ya fatality rate kati ya mtu mweupe na mtu mweusi? Kati ya tropical and template Climate/Weather kwenye CORONA?

Kuambukizwa sio issue kwetu issue yetu ni mortality ratio sio morbidity
Oh Please!
COVID-19 does not discriminate against race! Fatality rates will depend on other issues but race is definitely not one of them.

Issue ya weather and climate can affect the lifespan of the virus on surfaces. Bado tafiti zinaendelea ili kukifahamu zaidi hiki kirusi. It's called a novel virus for a reason.

Unasema kuwa maambukizi siyo issue, but that is an issue and a half in every context.
 
Retired,
Jamaa ana hesabu kubwa,yaani weakest ni wazee na wagonjwa. Wakiondoka kwenye hesabu ya uhai,mifuko ya bima itatuna na atatumia gharama ndogo kifedha.

Ila comrade kama njia ndio hiyo,ni wazi itawakuba wengi haijalishi wewe ni waziri au mbunge au karani au bodaboda.At the end of the day mtego huu wa panya utaigiza waliokuwemo na wasiokuwemo.
 
Jana rais aliibuka hadharani akatuambia watanzania eti tuanze kutumia mbinu za asili katika kukabiliana na ugonjwa wa covd19 kwa kuanza kujifukiza na kutumia mwarobaini.

Binafsi sikutegemea kama rais mwenye weredi kama rais Magufuli atoe wazo ambalo wote tumemshangaa, pia aligusia kuwa eti tuache kutumia barakoa zile za msaada zilizotolewa na jack ma billionea wa kichina akidai sio salama.

Sasa swali langu ikiwa yeye ndie alieruhusu misaada ya jack ma kuja nchini iweje leo aje hadhrani tena bila aibu aanze kuikataa misaada hiyo, nilicheka sana baada ya kusikia rais wa Uganda Kaguta Museveni akituambia Mungu yupo bussy sana mda huu.

Nikajaribu kuifutilia kwa makini kauli hii ya huyu kiongozi shujaa kutoka Uganda ambae kwa sasa anafaa kupewa pongezi kutokana na hatua aliyopiga nchini mwake katika kupambana na ugonjwa wa corona.

Binafsi nakiri kuwa kuna mawasiliano hafifu kati ya rais na wizara yake ya afya na mda tu utaongea na tutajionea mengi, utabiri wangu ni kuwa tusipokuwa makini hadi kufikia mwezi wa 6 maafa makubwa yatatokea na pengine tutakuwa nchi ya kwanza ya Afrika itakayoshika nafasi ya kuwa na vifo vingi.
Notes it,
 
Nashindwa hata kuandika,yaani rais kututangazia kuwa bidhaa toka nje si salama wakati huo hizo bidhaa zikiwemo madukani nchini Tanzania maana yake anasema serikali yake imeshindwa kazi,hakuna udhibiti tena kila mmoja anaweza akaingiza bidhaa yake Tanzania as if anapekeka home kwake Kama nchi hii wangekuwa wanaishi watu hai sentence hii tu ingetosha kuanza maandamano ya kumng'oa maana anachezea maisha yetu
Raisi kajiweka pembeni as if ni mtazamaji amegeuka auditor wakati serikali ni yake
 
sblandes,
You might be right, but I do not think he had that in his mind. May be it might be an afterthought. Kama ulivyosema wataingia wote.

Kuja kutimiza azma hiyo na mke wake na watoto wanaweza wakawa wame perish! Time will tell!
 
You might be right, but I do not think he had that in his mind. May be it might be an afterthought. Kama ulivyosema wataingia wote. Kuja kutimiza azma hiyo na mke wake na watoto wanaweza wakawa wame perish! Time will tell!
Mkuu nimefuatilia kwa karibu sana na taarifa ya wataalamu wa afya. Nikichukulia jimbo la New York Marekani idadi ya vifo vingi vilitokea kwa watu weusi kuliko wazungu walio wengi.

Sababu ilikuwa weusi wa huko wengi walikuwa wanasumbuliwa na magonjwa yanayofanana na magonjwa sugu yaliyopo nchini kwetu tena kwa wingi.

Kwa Darwin's Theory, Weakest kiafya kwa case ya Corona ipo wazi.Maadamu tumekosa maarifa imebakia kumuomba Mungu.
 
Wakuu poleni na majukumu na wale waliondokewa na ndugu na jamaa katika kipindi hiki Mungu awatie nguvu.

Moja kwa moja kwenye Mada, Wakuu Jana mzee baba kaeleza kuwa tutumie na vitu vya asili ikiwemo kujifukizia kupambana na huyu Mwamba fagia fagia Covid19. Nikisindikizwa na Maandiko matakatifu kutoka kitabu Cha Yeremia 46:11".....pandeni Gileadi enyi watu wa Misri,mkachukue dawa ya marhamu,mmetumia dawa nyingi bure, hakuna kitakachowaponya nyinyi'. Ifuatayo ni baadhi ya mimea ambayo tunaweza kuitumia kipindi hiki cha Covid19 ikaleta nafuu.

1. Kitunguu swaumu(Allium sativum) kwa matibabu ya Kikohozi,mafua,madonda ya Koo na sinusitis.

I.Kula kikonyo kimoja cha kitunguu swaumu mara tatu kwa siku.
II.Tumia kijiko kimoja cha chai Cha asali ya kitunguu swaumu kila baada ya saa chache.
III.Tumia kijiko Cha chai kimoja cha mafuta ya kitunguu swaumu mara 6 kwa siku.
IV.Watoto wanaweza kutumia kijiko kimoja cha chai Cha mchanganyiko wa dawa ya Kikohozi ya kitunguu swaumu kila baada ya saa chache.

2. Artemisia annua anamed (A3). Kikohozi mafua na sinusitis.
I.Vuta mvuke kutoka kwenye chai ya moto ya Artemisia kwa dakika kumi mara tatu kwa siku. Chai isiwe na joto kali wakati wa kuvuta mvuke.

3. Limau (Citrus limon)
Homa.
Kuliko kunywa Asprin ni Bora zaidi kuimarisha mfumo wa kinga!.
Kunywa juisi ya Limau mara tatu kwa siku kwenye kikombe kimoja kikubwa cha mil 5000.Usichemshe juisi,utaharibu vitamin C.

4. Kitunguu maji (Allium cepa)
Kikohozi na madonda koo. Changanya kikombe Cha vitunguu vilivyokatwakatwa na kikombe Cha maji,koroga,kunywa kwa siku mzima.

5. Mranaa (Detura stramonium).
Kushindwa kupumua. majani huvutwa Kama sigara kwa ajili ya kusaidia kupumua pamoja na kutibu pumu(sio sugu.Utomvu unatumika kutibu sugu),majani mengine Ni majani makavu ya mkaratusi mil150,majani makavu ya mpapai mil700. Mambo ni mengi mimea mingine mtaongezea wakuu kwa faida ya wale wenzangu na Mimi pangu pakavu.

Onyo: Usibebe ukaipeleka kwenye blogu yako.

NB: Endelea kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya na sio wanasiasa.Hatma yako iko mikononi mwako.
 
Sharobaro la jf,
Uliloliandika ni kweli. Jana Rais alitoa ushauri wa kutumia dawa ya mitishamba ya kutumia mvuke. Bado nikaona andiko la naibu waziri wa afya akitahadharihsa watu kutotumia huo huo mvuke kwasababu njia ya hewa haina uhusiano na moshi watu wasije pata madhara. Sasa tufuate la yupi?
 
Back
Top Bottom