Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Nimecheka. Sasa mtu ujifukizie vapour above 100 itauua Coronavirus. Wanasayansi anaongea kitu ambacho hajakifanyia experiment.
Nimemsikia Ndugulile, Naibu Afya, akisema hiyo kujivukiza sio salama. Inaweza kuleta shida kwenye mfumo wa hewa. Anasema sehemu hizo za mwili haziwezi kuhimili joto kali hivyo!
 
Umetembelea mortuary za Marekani na Italy ambako wamejifungia? Au unasema tu, hata Rwanda umetembelea mortuary zake? Usijidanganye kaka, wewe mtaani kwako unakokaa, kazini kwako, kanisani kwako, kwenye ukoo wako umeona watu wangapi waliokufa kwa CORONA? Au unasikia maneno ya mtaani?
Ulishawahi kujiuliza hao unaosema walijifungia walijifungia wakati gani?! Nchi imeshaathirika, ugonjwa umeshaingia mtaani, unadhani hata mkijifungia watu watakosa kufa wakati walishaathirika hata kabla ya hizo lockdown!!

Halafu acha kuongea mambo usiyoyajua... both Rwanda na Uganda HAKUNA hata mmoja aliyekufa kwa corona!!
 
Personally naamini Magufuli kuwaita jamaa kwenda kule, kuna kikao cha siri dhidi ya baadhi ya wanasiasa na watu wanaoonekana ni wasumbufu.

Otherwise angeweza kuongea nao akiwa kule na wao wakiwa Dar.

Kuna agenda zaidi ya hii.
Wakina Gates &com kuna upumbafu wa kindezi wanataka kufanya dhidi ya mataifa ya Africa lazma vyombo vyote vya ulinzi na usalama viwe makini otherwise nisu ya Africa tutapuputika wote
 
Ukitaka mfano wa kuigwa na sio huo wa kubahatisha unakokusifia bila ya kuwa na sayansi yoyote nyuma yake, basi mtazame kwa heshima Museveni.
Sayansi ipi kwenye CORONA? Sayansi ambayo haikufaa Marekani, Spain, UK, Italy, France, German, Canada ingevaa nini Tanzania?
 
Rais Magufuli hakupepesa macho alipowaruhusu watanzania waendelee na shughuli zao za kujipatia riziki huku wakiendelea kuchukua hatua mbalimbali za kujilinda. Kwa Mara ya kwanza hata wazungu wamemuona Kama kiongozi mwenye maono ya mbali asiyekuwa bendera fuata upepo wa wazungu.

Wakati nchi za Marekani na Ulaya zinawa kulegeza lockdowns sasa Tanzania ukiona kuwa haitawezekana kuwafungia ndani watu wote kwa Mara moja. Nchi zilizojaribu kufanya hivyo hazikupata matoe chanya dhidi ya CORONA.

Sio kila kitu lazima tuwaige wazungu Kama kasuku Kama baadhi wa maRais wa Africa walivyoumbuka. Sasa hivi mataifa yanahangaika kujibu maswali ya watu wao wanaozishindwa lockdowns, hata Rais Trump ameona upuuzi wa lockdowns kijamii na kiuchumi.

Tutamkumbuka hakiyaMungu huyu mswahili wetu akimaliza ngwe yake.
Mpaka na komenti muda huu walio like mada yako ni mataga wenzako.
 
Hotuba zote ukisoma mwanzo mpaka mwisho ni kuwa magufuli amewaangukia wale aliokuwa anawaita MABEBERU ohh sisi ni matajiri kiko wapi magufuli we wewe ohh IMF ,ohh BANK YA DUNIA 😁😁 kwisha kaziiii lockdown imekushinda aisee huyu bwana alivyoingia tu Ikulu kuwatukana wazungu sasa leo amekiri mwenyewe TUNAOMBA TUPUNGUZIWE yaani .
 
Hivi huyu jiwe amepata ushauri kutoka kwa madaktari au anajiongelea tu?Maana wenzetu daktari anakuwa pembeni anamshauri mambo ya kufanya sasa huyu sijui anapata wapi
 
Asante jf doctor.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mie wala sio Dr, isipokuwa kijijini kwetu hii vita inapiganwa kupitia health promotion ni muhimu zaidi wananchi kupata kila angle ya elimu hili wajikinge.

Yaani zaidi ya msisitizo wa kunawa na maji tiririka hakuna la ziada raia wengi awajui hata wakipata Corona wata deal na changamoto zipi.
 
Back
Top Bottom