Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

veca,
Umeandika mada yako vizuri. Mada ambayo wakuu wa JF wameona iimeze ile ya kwangu (kimakosa) kwa sababu hazifanani kabisa.

Pangekuwepo sehemu ya kukata rufaa ningewasilisha malalamiko yangu kwa huyo mfanya kazi aliyeunganisha ile mada na hii ya kwako. Nadhani hakusoma maudhui ya mada yangu, yeye kabwatuka tu na kuunganisha.

Sababu iliyonifanya niku'quote' hapa kwenye hiyo mistari ya mwisho katika hitimisho la mada yako ni kwamba binafsi sioni siasa yoyote anayoifanya Magufuli katika jambo lolote. Magufuli hajui siasa na sasa anaonekana ufahamu wake juu ya mambo mbalimbali hana kabisa.
Hata kisomo alicho nacho cha kiwango cha Ph>D. naona pia hakikumpa nafasi ya kupanua mawazo na kuwa na ufahamu mpana.

Rais Magufuli ni mvurugaji tu katika kila jambo analohusika nalo. Hakuna jambo analoweza kulifanya na akalikamilisha kwa utulivu, hata kama ni jambo zuri.
 
Kweli mkuu watu wasiwe na hofu si unaona Uganda eti nao waliweka lockdown sasa angalia madhara makubwa waliyo pata
Cases 58 ,Deaths 0 na recovered 38 ...Wamepigwa ...alisema Think Tanker Gwajima
Ni matumaini yangu makubwa ni kwamba umenisoma na kunielewa vizuri mkuu wangu 'Bishweko.'
Kutokana na uliyoandika hapa, inaelekea umesoma mistari miwili ya mwanzo na kuishia hapo!
 
idawa,
IMG-20200423-WA0008.jpg

Jamani Trump anatafuta dawa ya watu wake,hii la kujifukiza na mvuke wenye nyuzi joto Mia nadhani litamfaa na tutapiga hela sana
 
JokaKuu,
Ndugu cha muhimu ni umezungumzia kutoka wapi au aliyezungumza ana nafasi gani?Labda kama unaushahidi kuwa aliyezungumza kuto huko siyo raisi utuletee,na wanapokuwa kwenye mikutano wakitoa maagizo kwa sababu hawako ikulu huwa hayafuatwi?Nisaidie na mimi nijifunze hivi Trump akitweet huwa anakuwa whitehouse muda wote?

Maisha usiyafanye kuwa magumu kiasi hicho,kwa hiyo raisi akiwa nje ya ikulu anakuwa siyo raisi hawezi kuzungumza?

Je, kwakuwa waliomtangulia hawakufanya haya anayoyafanya je hili ni tatizo?Kwani hujua haya yeye kuna mazuri anafanya ambayo wenzake hawakuyafanya ,je wenzake hawakuwa maraisi wa Tz?

Labda kama katiba inamtaka akizungumza awe only Ikulu tusaidie ili nasi tujue. Inawezekana tumezoea kuona maraisi wakiongea kutoka Ikulu lakini je hawarusiwi kuongea na taifa kutokea eneo jingine? Tufahamishane hapa.

Zama zimebadilika ndugu be flexible.
 
Ni matumaini yangu makubwa ni kwamba umenisoma na kunielewa vizuri mkuu wangu 'Bishweko.'
Kutokana na uliyoandika hapa, inaelekea umesoma mistari miwili ya mwanzo na kuishia hapo!
Mkuu nimekusoma vizuri tu...ebu rudia tena kusoma karamu yangu
 
Nilikuwa napitia takwimu za nchi mbalimbali ikiwemo Marekani na Ulaya idadi ya wagonjwa wanaopona inaipita ile ya waliokufa kwa uwiano mkubwa kiasi.

Hapa kwetu idadi ya wanaopona na wanaokufa ni karibu inalingana ila namba ya wagonjwa ndio inabaki kuwa kubwa.
Au wagonjwa huwachukua muda mrefu kupata nafuu na kupona?

Natafakari tu!
 
johnthebaptist,
Wewe Mlumumba ni kwa sababu tumekwaa maambukizi mengi kwa muda mfupi. Tumia akili siyo kila kitu kwakuwa umeambiwa na boss wako basi unameza tuu. Hamna kiongozi mle!
 
Nilikuwa napitia takwimu za nchi mbalimbali ikiwemo Marekani na Ulaya idadi ya wagonjwa wanaopona inaipita ile ya waliokufa kwa uwiano mkubwa kiasi.

Hapa kwetu idadi ya wanaopona na wanaokufa ni karibu inalingana ila namba ya wagonjwa ndio inabaki kuwa kubwa.
Au wagonjwa huwachukua muda mrefu kupata nafuu na kupona?

Natafakari tu!
Haujasikia jana Rais akisema waliopona ni 100? Kati ya takwimu za Waziri Mkuu na Rais wewe unataka kutumia zipi?

Zilizotangulia kutangazwa au zilizotangazwa mwishonii? Na wameambiwa watangaze na waliopona..hivyo repoti ijayo tegemea kuona wamepona 200
 
Haujasikia jana Rais akisema waliopona ni 100? Kati ya takwimu za Waziri Mkuu na Rais wewe unataka kutumia zipi? Zilizotangulia kutangazwa au zilizotangazwa mwishonii? Na wameambiwa watangaze na waliopona..hivyo repoti ijayo tegemea kuona wamepona 200
Kwani rasmi ni zipi?
 
Hakuna aliyeambukizwa wala aliyekufa.Haya makofi kwa wana lumumba
 
Mtukufu kasema wame pona 100 ...nazani ili twende sawa na Kenya na Uganda
 
Haujasikia jana Rais akisema waliopona ni 100? Kati ya takwimu za Waziri Mkuu na Rais wewe unataka kutumia zipi? Zilizotangulia kutangazwa au zilizotangazwa mwishonii? Na wameambiwa watangaze na waliopona..hivyo repoti ijayo tegemea kuona wamepona 200
Mbona za waliokufa hawakumpa tofauti na alizonazo Waziri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkumbuke waliyo mahututi ni wanne tu na ni kwa sababu wana maradhi mengine yanayowasumbua,hao waliyobaki wako fresh wanapiga hadi push ups.
 
Nilikuwa napitia takwimu za nchi mbalimbali ikiwemo Marekani na Ulaya idadi ya wagonjwa wanaopona inaipita ile ya waliokufa kwa uwiano mkubwa kiasi.

Hapa kwetu idadi ya wanaopona na wanaokufa ni karibu inalingana ila namba ya wagonjwa ndio inabaki kuwa kubwa.
Au wagonjwa huwachukua muda mrefu kupata nafuu na kupona?

Natafakari tu!
Unahesabu na kina Pierre liquid waliotoroka leo🤣
 
Back
Top Bottom