Mkuu nguruvi3, kwasababu mimi nilisupport hatua za Magufuli tangu day 1 kwa kuamini Corona sio tropical disease, ni ugonjwa wa Wazungu, ila ulipoanza kushika kasi nilibadili msimamo na kushauri.
Kwa sasa tuko kwenye injury stage, the best thing to do now ni kuendelea kushauri and help out, kunyoosheana vidole is adding an insult to an injury, halafu tatizo likiisha ndipo tufanye postmortem na pointing fingers where we did wrong.
Mkuu hili tulipingana sana nikakueleza kuwa Corona ni 'novel virus' hakuna anayejua tabia zake , na kwamba nchi zinazokaribiana na 'Tropical ' kama Italy ziliathirika vibaya sana.
Nchi za hali ya baridi ya wastani kama Spain ziliathirika na ilikuwa wazi Sub Saharan hatupo salama
Hilo ndilo lilichagiza tukashauri mambo 11 ya haraka kufanyika ili kuzuia ugonjwa au kuunguza makali kama wanavyofanya Kenya, Uganda na Rwanda. Kudos
Katika maambukizi (infectious disease) katika kiwango cha Pandemic kuna stage kama 4 au 5 kama sikosei.
Tanzania tumeshapita zote na sasa tupo stage ya mwisho ambayo ni kualika jeshi ili lisaidie katika kudhibiti watu na kusaidia shughuli kama za usambazaji wa vifaa tiba, huduma muhimu kama vyakula na hata mazishi.
Hili limefanyika kote duniani kuanzia Marekani, Australia, UK , China, Korea, Italy , Spain n.k.
Si bahati mbaya ni utaratibu wa control na upo katika ''Epidemiology'
Sasa hivi ni too late hakuna cha kufanya, community spread inashika kasi.
Tunachoweza kufanya ni kuzuia isiende vijijini kwenye wazee na watu wenye underlying disease
Nini kitatokea?
Mwezi wa May na June maambukizi yatafikia kileleni yakiambatana na vifo vingi sana.
Baada ya hapo graph itakuwa peak halafu plateau ambapo wanaoambukizwa ni wachache lakini idadi ya vifo itabaki kubwa kwasababu walioambukizwa watakuwa wanaugua kwa nyakati tofauti .
Mwezi July graph itaanza kushuka, kwa maana maabukizi machache , vifo vichache
Halafu itatokea Herd Immunity kwamba watu wengi wataambukizwa na hakutakuwa na maambukizi zaidi.
WHO wanasema hakuna uhakika kama mtu aliyeambukizwa hataambukizwa tena .
Kwa kawaida, Virus wakishamshambulia mtu, hawawezi kumshambulia tena kwasababu mwili una immunity.
Ndivyo ilivyo kwa surual(measles, small pox, chicken pox na hata baadhi ya strain za influenza)
Kinachoweza kufanyika sasa hivi ni kuzuia mikusanyiko kama Bunge n.k.
Haina maana kuzuia watu wasizike wapendwa wao halafu misikiti na makanisa yapo wazi.
It does not make sense!
JokaKuu MsemajiUkweli Mzee Mwanakijiji