Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Nini kinatufanya tujuwe wagonjwa wameongezeka au kupungua? Nani anajua maambukizi yamepungua au kuongezeka Kama hakuna kupima?
Mkuu usishawishike hata siku moja kumuamini huyu mzee,hana ukweli hata mmoja.

Anatupeleka sipo kabisa mkuu,yaani kauli zake tu ni utata mtu alafu sijui hana kumbukumbu ya kile alichokinena hapo awali.

Tumeangamia kama taifa,dereva wenyewe ndo huyu basi tupo hatarini kutumbukia mto wami.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mzee tumsamehe tu. Huenda hayuko sawa kichwani. In fact hayupo sawa kichwani!
"hili ni taifa huru! Linajiamulia mambo yake lenyewe, lilishapambana na majanga mengi likashinda.
Na sisi katika EAC tuko pamoja tunafanya kazi pamoja, lakini katika kutatua tatizo kila taifa lina njia zake, wewe unaambiwa kajilockdown unaenda na huna chakula,
Za kuambiwa changanya na zako! "

Hiyo ni sehemu ya nukuu toka kwa JPM.

Usipomuelewa wewe utaendelea kuitwa nyumbu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemsikia Rais akisema kuwa mwanae ilipata Corona hii inaweza kuwa sababu aliamua ajitenge ili kuepuka maambukizi ya Corona, kwa maoni yangu Rais alifanya jambo jema kama Kiongozi wa kitaifa na kuamua kufanya kazi kutoka Kijijini kwake Chato

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo haiwezzi kuwa sababu kwasababu yeye anapingana na maelekezo yote ya kitaalamu
 
Mungu azidi kumlinda Rais JPM..
Hakika ni chaguo la Mungu

Leo naamini nikiwa kama Mkristu niliye na Imani tele maishani mwangu.. naamini wengi watakuwa wameondoa hofu kwa kumsikiliza.. kweli angekuwa Mchungaji tu.. ana upako..

Kama alivyosema.. endeleeni kuchukua tahadhari na kusali.. msiruhusu hofu iwaingie..

Magufuli oyeeeeeeeee

Hi Baby!!! Habari ya kuadimika. Tunakushukuru kwa kutuletea mtoto mzuri Bia yetu.

Magufuli oyeeeeeeeee

Makonda oyeeeeeeee

Cocochanel oyeeeeeeee

Jamii Forums oyeeeeeeee
 
Na kuna watu laki kadhaa waliougua wakakaa tu nyumbani wakajifungia wakapona. Hahah zee jinga hili, mtu moja kupona haimaanishi ni dawa, ingekua hivyo watu milioni waliopona duniani kwa kukaa tu miili yao ikapambana na virusi tungesema hiyo ni dawa kwa hiyo tusifanye lolote.
PhD hivi aligawiwa bure? Au alifanyiwa research na mtu mwingine? Mbona jinga sana?
 
Haya ameyasema mheshimiwa rais Magufuli hoko Chato alipokuwa akiongea katika ibada ya Jumapili leo katika kanisa la KKKT.

Pia rais amesema ana mpango wa kufungua utalii hivi karibuni, booking za ndege zimejaa hadi August.

Wagonjwa wa corona wamebaki wachache mahospitalini amesema.

Rais amesema vyuo, michezo vitafunguliwa wiki ijayo. Na mengine mengi fuatilieni.

Nawasilisha tu kama nilivyosikia, maoni yangu yanafuata.
 
Back
Top Bottom