Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

"chocheeni kuni mbichi moto ukolee,ugali uivee,mnachotaka kitokee........"
 
Mkuu mm sina tatizo na msimamo wako wa kuchagua kutomuamini "because as u said is non of my business and I respect that" tatizo lilikuwa pale tu unataka na wengine tusimuamini kwa sababu tu ww humuamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Lakini pia tukumbuke mwisho wa mwanadamu yeyote ni kifo" mwisho wa kunukuu
Na ukumbuke pia hakuna anaependa kutangulia kufa,na ndio maana watu wanaambiwa wachape kazi wkt wao wako MBOCHI.
 
Hivi Rais huyu hawezi hutubia bila vijembe na kufoka?!
 
Je wagonjwa wamepungua sababu Corona imeisha au sababu tumesimamisha upimaji wiki ya tatu hii sasa??
 
Nikikumbuka uongo wake kwenye sakata la korosho, siwezi kumuamini huyu jamaa, labda baada ya kuvuta bangi ya lumumba inayolimwa na chakubanga.
Yeye yuko vichakani, halafu anatuambia sisi tuchape kazi.
 
Huyo Anna Mgwira alijitangaza ana Corona then juzi kasema kuna majani ameyatumia sasa akipimwa anaonekana ni Negative,hayo ndio maajabu tuliyobarikiwa.
Hata angesema alikula mchicha akapona tusingemlaumu kuliko huyu anayetafuta Kiki nyepesi. Ina maana yeye alikuwa na mgonjwa ndani halafu akawa anatoka nje kuonana na wakuu wa vyombo vya usalama na mawaziri wake huku akijua ndani kwake kuna mgonjwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haombewi yeyote hapa.Kila mtu apambane na kushinda mechi yake. Na maabara ipi mtoto wako ulimpima kama ya taifa uliipiga kwara? Atakayekuamini ni kwa hasara zake mwenyewe.
 

Magufuli amesema ni ujinga wa kupitiliza kwa nchi ambazo zimeizunguka Tanzania kujaribu kufunga mipaka yao na Tanzania kwasababu nchi hizo zinaitegemea sana Tanzania.

Ametolea mfano kwa nchi moja(Kenya) ambayo inaitegemea Tanzania kwa mahindi, mchele na hata mifugo(nyama), kutangaza kufunga mipaka wakati ikijua kwamba hawana chakula cha kutosha.

Magufuli anategemea kufungua shule na vyuo vya elimu na kuruhusu ndege kuanzia safari zake za kawaida ndani ya wiki mbili zijazo kutokana na hali ya ugonjwa wa Corona kutengemaa nchini.
 
Rais ni muongo, hakuna aliyesema awafungie wakulima, kwanza lockdown ya Dar ndiyo ingewaepusha wakulima na maambukizi. Halafu watu hata hawaelewi. Dah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…