Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Sasa huoni kama katika vipimo vilivyofanya na nchi jirani kwa wagonjwa bado ugonjwa unaongezeka sana??
Hiyo sana toa. Wanaopona ni wengi kuliko wagonjwa wapya na mwisho wa siku wataisha. Ninawashangaa watu kuikomalia Tanzania wakati si miongoni mwa nchi zenye maabukizi. Hata majirani zetu wa kaskazini mashariki wana maambukizi mengi zaidi. Afrika maambukizi mengi yako Afrika ya kusini, Afrika ya kaskazini na Aftika Magharibi. Sisi Afrika mashariki ikiwemo nchi yetu maambukizi ni kidogo sana. Lakini dunia nzima inapigia makelele nchi yetu utafikiri wana hasira fulani na sisi vile! Huwezi kuwasikia wakizungumzia nchi zenye maambukizi kwa maelfu!! Watukome!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea. Kama corona imepungua kwa nini bado yeye yuko Chato amejificha. Arudi ofisini na yeye achape kazi.
 
Katika akiri tu Ya kawaida, kwa kipindi hiki huwezi kwenda kwenye sehemu ya mikusanyiko mikubwa ukakuta hakuna alievaa mask ,kitu kingne sidhani kuwa kwenye kikao cha rais unaweza kuruhusiwa kuingia pasipo kuvaa mask.

Picha zinaonesha kuwa watu wote hawakuvaa mask, hiii maaana yake wote walikatazwa wasivae?na kwa nini walikatazwa wasivae mask? Ni Kwa faida ipi? Inamaaana watu hawa walipangwa na Kama walipangwa nikuwa kuna usaniii Mkubwa unafanyika tena usaniii ambao hujui kwa nini unafanyika, Mimi nashindwa hata kuelewa, why inafanyika hivyo? Nikwa ajiri ya kumfurahisha mtu Fulani Au nikwa ajiri ya kumkomoa mtu au ni kutaka kulazimisha kuwa hakuna tatizo? Ila kwa levo ya Yule kiutawala haya mambo hayastahili ayafanye bhana, haya huwa yanafanywa na watoto

Kufanya hivyo hata utakayoyaongea kwa watu wenye akiri wataona kuwa ni usaniii tu, maaaana Kama umefanya hivi kuwaambia watu waingie pasipo masks utashindwa nini kudanganya? Hiii imenifikirisha Sana


Sent using Jamii Forums mobile app
Mask ni muhimu tu mahali ambapo haiwezekani kukaa mbali mbali!! Utaratibu kanisani siku hizi wameongeza idadi ya ibada ili watu wawe wachache kwenye ibada moja na watu wanakaa mbali mbali.
Hajasema watu wasivae Barakoa, amesema tuchape kazi huku tukiendelea kuchukua tahadhari (kwa kusema tuendelee kuchukua tahadhari maana yake tuvae barakoa mahali ambapo haiwezekani kukaa mbali mbali kama kwenye mabasi nk). Usimlishe maneno!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumbe ule ukimya wa mzee week na siku kadhaa zilizopita ni venye alikuwa anauguza mwanae na kile kikombe cha madagascar kilifuatwa specifically kwa mwanae ndiyo maana hakigawiki kwa watz wote
 
Kwenye hospitali ya Agha Khani nako wamepungua wamebaki watu 31,
- Hindu Mandal wamebaki 16,
- Ragent Hospital wamebaki 17,
- TMJ wamebaki 7,
- Labinisia kule Tegeta wamebaki watu 14
Haya majibu yalitokana na vipimo vya maabara ipi? ile ile iliyosema kuwa haitoi majibu sahihi? au kulikua na maabara nyingine tofauti na hii?
 
Mkuu Mimi sizungumziii aliyoyaongea nazungumzia zile Picha kuwa, ilikuwaje wakaenda wote pasipo mask? Nadhani hata wewe huenda unajiuliza hivyo Mkuu, Kama wameelekezwa hivyo maaana yake ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikuulize je unafikiri walikaa umbali wa angalau mita moja kati ya mtu na mtu au chini ya mita moja kati ya mtu na mtu?
Kwa ukaaji wa siku hizi makanisani ni zaidi ya Mita moja kati ya mtu na mtu. Kwa hiyo katika mazingira hayo barakoa haina kazi. Wamezitunza barakoa zao watazitumia kesho wakienda sokoni au kwenye dala dala!! Halafu usifikiri korona ipo kila kona yz nchi!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom