Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Ngonjera za wanasiasa hizo ,sehemu zote zinalindwa na JKT na hautakiwi kurandaranda katika hayo maeneo uliyoyataja!!
Siyo kweli, hizo ni hospitali na kuna saa za kuona wagonjwa!! We jiandae tu na PPE yako ukaangalie wagonjwa. Uwapelekee na matunda nk
 
Your argument is very weak
 
Kwa staili hii yule daktari naibu waziri lazima atofautiane na mteuzi wake!! Madaktari wamefundishwa umuhimu wa kuzuia MTU hata m1 asiugue,hatari ya virus I na pia kuwa na data sahihi sasa ukikutana na asiyejali anaweka maujanja ujanja kujipa ugangwe mob lazma mpishane
 
Hao wanasheria na mawakili walikuwa hawafi ila wameanza kufa kwa corona tu! It does not make any sense!

Sent using Jamii Forums mobile app
Haujui unalozungumza wewe njoo na takwimu mwaka jana walikufa watu wangapi kuanzia jan-may kisha fanya comparison ,numbers dont lie mkuu ,namba ikiwa tofauti lazima ndio unaweza kuconclude kwamba vifo vimeongezeka au vimepungua na kufanya more analysis ,naomba majibu kuanzia jan-may 2019 walikufa watu wangapi in general na mwaka huu jan -may wamekufa wangapi kisha tufanye analysis.
 
By Malisa GJ

1.Nampongeza Askofu Shoo kwa kuliongoza vizuri kanisa la KKKT na Askofu Keshomshahara wa Dayosisi hii kwa kazi kubwa anayoifanya. Mungu awabariki sana.

2. Wakati Corona inaingia niliwaomba watanzania waombe kwa siku tatu. Nawashukuru Wachungaji, Masheikh na Maaskofu kwa kuitikia wito na Mungu amejibu. Si vibaya tukatenga hata siku moja ya kumshukuru ktk sala zetu za wiki.

3. Mtoto wangu wa kumzaa aliugua corona. Akajifungia ndani akajifukiza, akanywa malimao akapona. Sasa hivi anapiga push-up hana tatizo lolote. Ugonjwa huu utasambaa lakini utaisha wenyewe, tusiwe na hofu.

4. Kuna mambo ya hovyo yalikuwa yanafanyika hospitalini. Kila anayefariki wanakimbilia kumpima corona. Mtu amefariki unampima ya nini? Nguvu za kumpima wanazo lakini za kumhudumia apone hawana.

5. Hali ya maambukizi imepungua sana. Amana ilikuwa na wagonjwa 198 wamebaki 12 tu. Mloganzila 30 wamebaki 6. Kibaha 50 wamebaki 22. Arusha kituo cha Moshono kina wagonjwa 11 vingine havina wagonjwa. Mwanza vituo 10 wagonjwa 6. Dodoma wagonjwa 42 wamebaki wawili tu.

6. Kama hali itaendelea hivi hadi wiki ijayo nimepanga kufungua vyuo ili wanafunzi wetu waendelee kusoma. Pia nimepanga kuruhusu michezo kwa sababu michezo ni sehemu ya burudani. Maisha lazima yaendelee.

7. Mtu akifariki kwa ugonjwa wowote azikwe kawaida. Hakuna sababu ya kumzika kwa dharura, Corona sio Ebola.

8. Hakuna cha lockdown wala baba yake lockdown wala mjomba yake lockdown. Watu waendelee kuchapa kazi.

9. Kuna uwezekano kutokea njaa baada ya corona, kwa sababu nchi nyingi zimefungia watu wake ndani hawazalishi. Kwahiyo tutumie vizuri mvua hizi ndogondogo kulima ili tuwe na akiba ya chakula. Wale waliojifungia siku wakifunguliwa tuwasaidie chakula.

10. Tuna ushirikiano mzuri na nchi za EAC na SADC ktk uchumi na mambo mengne. Lakini hili la corona nimeona kila nchi itumie njia zake. Sisi ni taifa huru hatuwezi kupangiwa cha kufanya. Hata mzee Kikwete alisema za kuambiwa changanya na zako. Wanaoona kujifungia ndani ni njia bora kwao wafanye. Na sisi tutumie njia zetu tunazoona zinafaa, ili mradi kila mmoja anapambana na Corona ktk mazingira yake.
 
Siyo kweli, hizo ni hospitali na kuna saa za kuona wagonjwa!! We jiandae tu na PPE yako ukaangalie wagonjwa. Uwapelekee na matunda nk
Sawa nyie teteeni uovu ila tunachoshukuru kwamba huu ugonjwa ni noma unatwanga kwa wale wale wapiga mapambio wa MEKO.
 

True Lies...



Cc: mahondaw
 
Mkuu wewe ndio hujui lolote unalozungumza. Tanzania ni kweli inaagiza baadhi ya bidhaa kama malighafi ya "Palm oil" toka Malaysia, lakini uagizaji wa mchele na mahindi ulishasimamishwa muda mrefu, sasa hivi tunazalisha zaidi ya matumizi yetu na ziada tunaeauzia majirani.

Kuhusu sukari, sasa hivi tunazalisha 75% ya mahitaji yetu, juhudi zinafanyika kuhakikisha ikifika mwishoni mwa mwaka Kesho tuweze kujitosheleza kwa sukari.

Hivi Mkuu ulishasikia wapi kwamba nchi imekumbwa na njaa kutokana na upungufu wa sukari?, sukari sio chakula, ila ni kiungo muhimu katika mapishi, unaweza kula mkate, chapati, maandazi bila sukari, kitakachopungua ni ladha ya chakula.

Kuhusu ngano, ni kweli kwamba baadhi ya viwanda, hasa vya Azam vinaagiza ngano toka nje, hii ni kutokana na kwamba, Azam anatengeneza bidhaa kwa ajili ya kuziuza nchi nyingi sio Tanzania pekee, kwahiyo ngano inayozalishwa Tanzania haimtoshi.

Mwisho ni kwamba, sisi tunazungumza kufunga mpaka wa Kenya na Tanzania, Kenya italazimika kutafuta Chakula toka nchi zingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
haaa haa inaudhi sana
 
Mnajidanganya kwa kujiaminisha kwamba Kenya inawategemea,njaa zetu ndo zinatusumbua zaidi na Wala si kwamba tunahuruma sana.Tunaangamia kwa kukosa maarifa
 
Na shule zifunghliwe, ukimwi ulikuwepo na masomo yaliendelea, nk
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…