Mkuu wewe ndio hujui lolote unalozungumza. Tanzania ni kweli inaagiza baadhi ya bidhaa kama malighafi ya "Palm oil" toka Malaysia, lakini uagizaji wa mchele na mahindi ulishasimamishwa muda mrefu, sasa hivi tunazalisha zaidi ya matumizi yetu na ziada tunaeauzia majirani.
Kuhusu sukari, sasa hivi tunazalisha 75% ya mahitaji yetu, juhudi zinafanyika kuhakikisha ikifika mwishoni mwa mwaka Kesho tuweze kujitosheleza kwa sukari.
Hivi Mkuu ulishasikia wapi kwamba nchi imekumbwa na njaa kutokana na upungufu wa sukari?, sukari sio chakula, ila ni kiungo muhimu katika mapishi, unaweza kula mkate, chapati, maandazi bila sukari, kitakachopungua ni ladha ya chakula.
Kuhusu ngano, ni kweli kwamba baadhi ya viwanda, hasa vya Azam vinaagiza ngano toka nje, hii ni kutokana na kwamba, Azam anatengeneza bidhaa kwa ajili ya kuziuza nchi nyingi sio Tanzania pekee, kwahiyo ngano inayozalishwa Tanzania haimtoshi.
Mwisho ni kwamba, sisi tunazungumza kufunga mpaka wa Kenya na Tanzania, Kenya italazimika kutafuta Chakula toka nchi zingine.
Sent using
Jamii Forums mobile app