Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Mkuu Kuna tofauti kubwa sana Kati ya corona na ukimwi.
Totauti ni nini? Kinga ya ukimwi ni condom na Kinga ya corona ni barakoa. Pia maradhi yote yanasababishwa na virus. Tofauti ipo wapi hapo?
 
Nimeshangaa kuona anafurahi na kucheka kwa furaha kitendo cha waumini kutovaa barakoa kwenye mkusanyiko ule.
Hivi kweli huyu mtu ana nia njema na wale watu?
hili jambo kila nikifikiria nahuzunika sana. ndo maana nasema ili tuache kucheza na corona idondoshe mtu mmoja mkubwa tu akili zikae sawa
 
Adanganye ili iweje? Msiwe na hisia hasi kwenye kila jambo.

Watu walishaamka zamani boss, hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuambiwa uongo wa wazi akaamini, eti kisa asionekane ana hisia hasi.
 
Totauti ni nini? Kinga ya ukimwi ni condom na Kinga ya corona ni barakoa. Pia maradhi yote yanasababishwa na virus. Tofauti ipo wapi hapo?
Mkuu ukimwi ili uupate kwa kiasi kikubwa ni lazima ukafanye ngono.katika huu ulimwengu wa watu waliostarabika nowdays hakuna wanaochangia nyembe Wala sindano.Ila corona unaweza kuipata popote na muda wowote.kiwango Cha barakoa kukulinda na corona ni kidogo sana.Barakoa inazuia mate mate kutoka kwa mwathirika yasiingie moja kwa moja mdomoni au puani kwako Ila haizuii hayo maji maji kuingia machoni au kutua kwenye nguo zako au kwenye gari yako au kwenye siti uliyokaa kwenye basi au daladala.kirusi kikiwa kwenye shati yako au suruali au siti anytime waweza kukichukua na kukiweka mdomoni,puani au jichoni.
unless Kama hiyo barakoa unaivaa mwili mzima
 
Ni dhambi mbele za Mungu kutokumuamini kiongozi wako kiasi hicho. Alikutenda nini?? Mbona tulimuamini Mh Mbowe aliposema mwanaye kila akipimwa bado anao??
Ni sawa, mbona Makonda alimsema mtoto wa Mbowe....Vipi kuhusu huyo wa Magufuli mbona hakupelekwa kwenye vituo vya isolation kama wengine? Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu ni uchungu. Acheni double standard, tendeni haki ninyi watu.
 
Most likely hapakuwa na kitu hicho. Ni kuhalalisha anayoyafanya kuhusu corona, kuzipa uzito sentensi zake za mitishamba na kuwa siyo kuwa anawasukumia wengine bali na yeye ndizo anazotumia.
What are you smoking?
 
"Akili za kuambiwa changanya na za kwako."

Mtoto wa Rais kapata corona. Baba yake kafanya juhudi zote kuhakikisha akipona. Inasemekana hata ventilators ilipelekwa Chato na labda ni kwasababu ya kuokoa maisha ya mtoto wa Rais. Hata ndege kwenda kufata katon 13 za dawa ya madagascar inawezekana lengo ni kuokoa Maisha ya mtoto wa Rais.

Sasa kama Mtoto wa Rais anayetembea na ulinzi 24/7 ndani ya V8 full time AC. Vip sisi wanyonge tunaobanana kwenye mwendo kasi tunaendelea kupiga kazi?

Wengine tuna mpaka dalili zote za corona ila hatuwezi pata hata access ya vipimo tunapona kweli au ndyo tuendelee na herd immunity?

Hii nchi inawenyewe, wanyonge tuendelee kusindikiza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Most likely hapakuwa na kitu hicho. Ni kuhalalisha anayoyafanya kuhusu corona, kuzipa uzito sentensi zake za mitishamba na kuwa siyo kuwa anawasukumia wengine bali na yeye ndizo anazotumia.
Most likely anasema kweli ndo maana amekaa kijijini miezi miwili akifukiza kumponya mtoto hata akasahau ofisi yake iko Dar bado haijahamia Dodoma. Ofisi ya Serkali lazima ina physical address moja tu na ni occupant ndo anaweza akawa hayupo kwa muda tu lakini ofisi inabaki palepale mpaka itakapohamia address mpya officially. Mambo mengi hayaendi Awamu hii kwa sababu ofisi nyingi muhimu ziko Dar na Dodoma ikiongeza gharama za uendeshaji na usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma za occupants wahusika. Mtumishi akiwai likizo anakwenda kwao nje ya ofisi akimwachia MTU mwingine pale ofisini majukumu yake yote.
 
Most likely hapakuwa na kitu hicho. Ni kuhalalisha anayoyafanya kuhusu corona, kuzipa uzito sentensi zake za mitishamba na kuwa siyo kuwa anawasukumia wengine bali na yeye ndizo anazotumia.
watoto wake.
1, JESCA
2. JOHN JR -ambaye ni mwanasheria ila si wakili
Kati ya hao nani kaugua COVID?
atujuze tuendelee kumuombea
 
Mtoto wa Rais sio Rais. Nani aliyekuambia anatembea kwenye hizo gari tena akiwa na ulinzi.

Hii umeleta takataka.[emoji112]

Sent using iphone pro max
 
Most likely hapakuwa na kitu hicho. Ni kuhalalisha anayoyafanya kuhusu corona, kuzipa uzito sentensi zake za mitishamba na kuwa siyo kuwa anawasukumia wengine bali na yeye ndizo anazotumia.
This is none of your business go to hell!!
 
Back
Top Bottom