Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Je unadhani angefanya nini ili watu wasife? Je kabla ya COVID watu walikuwa hawafi? Je umepitia takwimu za vifo za muda gani kuonyesha sasa hivi watu wanakufa zaidi? Je mtaani kwenu wamekufa watu wangapi kwa COVID?
Ni upepo tu utapita.
 
Hawezi ku comment kwa vitu kama hivyo!
Kwanini? Maana kama rais wa nchi ameongea kitu cha uongo na yeye Msigwa kama anajua ukweli asiseme kuwa hapo rais amesema uongo? Kwa sababu watu watazidi kuamini tiba ya kufukiza na malimao kwa sababu hata rais naye ameitumia kumtibu mwanae.
 
Maana kama rais wa nchi ameongea kitu cha uongo na yeye Msigwa kama anajua ukweli asiseme kuwa hapo rais amesema uongo
Unajua kuwa ndungulile amefurushwa kwa sababu ya kusema kujifukiza siyo scientifically approved, akipingana na boss wake?
 
Umefanya jambo la muhimu sana kurudi! personally nilimis sana michango yako. Karibu tena!
What I am doing nowadays ni ku- block nonsense yoyote ninayeona ana ujinga/utoto wa kutojenga hoja bali matusi! And this has been comfortable with me!
Sasa vuta picha ungekuwa rais wa nchi kama ya Tanzania ni wangapi ungewablock?
 
Kwanini? Maana kama rais wa nchi ameongea kitu cha uongo na yeye Msigwa kama anajua ukweli asiseme kuwa hapo rais amesema uongo? Kwa sababu watu watazidi kuamini tiba ya kufukiza na malimao kwa sababu hata rais naye ameitumia kumtibu mwanae.

Hahah na gazeti la TZ Daima limeandika pale mbele kabisa 'mtoto wa mzee baba apona Corona kwa kutumia malimao.'

Watu wa chini wasio na uwezo wa kuchanganua mambo kwa upana na ambao ni wengi saaaana kwny jamii ujumbe watakaoupata kuhusu Corona na malimao si wa mchezo.

Ma DR. wanakazi sana aiseee.
 
Huyu bwana ana agenda ya siri na anaicheza kwenye uhai wa Raia 41m. Hii ni zaidi ya siri na muda ndio utakao jibu nakuifumbuwa siri hii.

Taifa lipo vipande viwili wanao mwamini mtemi kwamba zile risasi wakipigwa zitageuka maji na kamwe hazito wadhuru. Kwa bahati mbaya wanao amini wanaenda vitani wanauwawa na hawarudi kumwambia Kinjekitile yule mganga wake ni fake. Wengi wakafa na mwishowe na yeye akauwawa.

Miaka imepita sasa tumempata kinjekitile wa dunia yakisasa amesema jifukizen chapa kazi. Well kwa njaa zetu tunachapa kazi ila kati yetu wengi watapotea nambaya hawato toa majibu ya kweli. Itakuwa ni hatari juu ya hatari.
Kiongozi umepiga u turn!!? Hakika kila mtu ataona rangi halisi.
 
Ni dhambi mbele za Mungu kutokumuamini kiongozi wako kiasi hicho. Alikutenda nini?? Mbona tulimuamini Mh Mbowe aliposema mwanaye kila akipimwa bado anao??
Yeye mwenyewe alishaitangazia dunia kuwa haamini test kits za mabeberu... Sasa imekuwaje Leo ameamini vipimo vya mtoto wake na siyo vile vya mapapai na mbuzi!!?
 
Unajua kuwa ndungulile amefurushwa kwa sababu ya kusema kujifukiza siyo scientifically approved, akipingana na boss wake?
Suala la kujifukiza linafanywa sana na watu hutoa shuhuda zao mbalimbali humu, kwa hiyo alichoeleza Magufuli ni kama ambavyo watu wamekuwa wakieleza sana humu kuhusiana hilo na hiyo tiba ya kujifukiza. Kwahiyo inawezekana hawa watu pamoja na Rais mwenyewe wote wanaongopa kwa kutoa shuhuda za uongo na ndiyo maana naona ni muhimu Mh. Msigwa kusema ukweli kuwa rais Magufuli anaongopa maana anachofanya ni kuhalalisha tiba ambayo haina ushahidi wa kisayansi kama alivyoeleza Ndugulile.
 
Je unadhani angefanya nini ili watu wasife? Je kabla ya COVID watu walikuwa hawafi? Je umepitia takwimu za vifo za muda gani kuonyesha sasa hivi watu wanakufa zaidi? Je mtaani kwenu wamekufa watu wangapi kwa COVID?
Ni upepo tu utapita.

WENGI TU.
 
Hizi tabiri hazijaisha tu? Ifike mahali tukubali tu ukweli tu kuwa athari za corona kwa afrika ni tofauti na kwa wenzetu, hivyo suala sio fulani amefanya/hajafanya nini .
 
Yeye anamaboksi ya Dawa za Madagaska ambazo ndio alimpa mwanae
Huku anawaambia wananchi kuwa alimpa malimao na nyungu

Na kama sikosei yeye huwa anakunywa kama kinga daile huku akiwasanifu wananchi kuwa barakoa hazina maana
 
Ninyi ni kina Mbowe au mmelipwa na mabeberu,ama ni kati ya wale mluokuaga mnakula pesa za wananchi ovyo mkaminywa,Corona mitaani iko wapi? Kweni tunaishi wapi mpaka tusione?wajinga wakubwa nyie..kubali jaribu la mzungu siyo la kwetu,mbona wao hawajawahi kupata kipindu pindu?wanalazimishaje taharuki yao iwe ya dunia nzima?acheni ufirauni wenu
Huyu bwana ana agenda ya siri na anaicheza kwenye uhai wa Raia 41m. Hii ni zaidi ya siri na muda ndio utakao jibu nakuifumbuwa siri hii.

Taifa lipo vipande viwili wanao mwamini mtemi kwamba zile risasi wakipigwa zitageuka maji na kamwe hazito wadhuru. Kwa bahati mbaya wanao amini wanaenda vitani wanauwawa na hawarudi kumwambia Kinjekitile yule mganga wake ni fake. Wengi wakafa na mwishowe na yeye akauwawa.

Miaka imepita sasa tumempata kinjekitile wa dunia yakisasa amesema jifukizen chapa kazi. Well kwa njaa zetu tunachapa kazi ila kati yetu wengi watapotea nambaya hawato toa majibu ya kweli. Itakuwa ni hatari juu ya hatari.

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Je unadhani angefanya nini ili watu wasife? Je kabla ya COVID watu walikuwa hawafi? Je umepitia takwimu za vifo za muda gani kuonyesha sasa hivi watu wanakufa zaidi? Je mtaani kwenu wamekufa watu wangapi kwa COVID?
Ni upepo tu utapita.
Je unaona ni sahihi kutumbuliwa Ndungulile kisa katofautina naye?
 
Back
Top Bottom