Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Hivi Mbowe nawe mbona anasemaga "anahutubia taifa"? Kwani nayeye rais
Sielewi kuhutubia taifa lazima uwe rais? Nadhani muhimu ni idadi ya wasikilazaji. Mfano A ameongea amesikilizwa na watanzania 10. B amenguruma amesikizwa kwa makini na watanzania 20. B atakuwa ametimiza kwa ufanisi zaidi azma yake ya kuhutubia watanzania.
 
Magufuli anasisitiza tuendelee kuchukua tahadhali na kumuomba Mungu. Kama wiki ya kesho itaendelea hivi amepanga kufungua vyuo ili masomo yaendelee. Michezo iendelee

Booking za ndege zimejaa mpaka agasti,watu wanataka kuja Tz,hakuna karantini
Mungu ni mwema
Vijana wetu warudi mashuleni sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
duh jamaa anapigiwa makofi kama yote kwenye hilo kanisa ila nimekaa na wadogo zangu hapa wanakataa kukubaliana na ukweli.
 
Hii ndio inaweza kuwa ndio habari kuu ya leo huku uwezekano ukiwa ni zaidi kwa ligi ya soka kuruhusiwa kuendelea ila kwa mashariti ya soka kuchezwa bila mashabiki

Lingine nii kutangaziwa matokeo ya kazi ya ile kamati iliyoundwa.

Naishia hapo.
 
Magufuli anasisitiza tuendelee kuchukua tahadhali na kumuomba Mungu. Kama wiki ya kesho itaendelea hivi amepanga kufungua vyuo ili masomo yaendelee. Michezo iendelee

Booking za ndege zimejaa mpaka agasti,watu wanataka kuja Tz,hakuna karantini.

Daaah,jamani hii inakuwaje?ila kweli hali ipo hivi
Mtalii gani yupo tiyari ku risk maisha yake in Dark country, aache kudanganya watu, labda afungue vyuo maana hilo lipo ndani ya uwezo wake lakini siyo kuleta watalii kipindi hiki
 
Back
Top Bottom