Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Haushangai kenya wanatangaza watanzania madreva wenye COVID 19 lakini hawatangazi wakenya wangapi wamepata maambukizi mapya ndani ya masaa 24? Ingia kwenye internet - Worldometer uone wana wagonjwa wapya wengi zaidi ya hao kwa mbali!!! Ni sawa na kumwona mwenye boriti kwenye jicho lake halafu anamcheka mwenye kibanzi jichoni, haushtuki? Unaruhusiwa kwenda kwenye hospitali ukajionee hali halisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
My friend Kenya wapo very transparent wametangaza new cases 57 Na kati ya hao kuna 12 Truck drivers
Kila siku saa tisa mchana Lazima watoe Update
 
Hiyo sana toa. Wanaopona ni wengi kuliko wagonjwa wapya na mwisho wa siku wataisha. Ninawashangaa watu kuikomalia Tanzania wakati si miongoni mwa nchi zenye maabukizi. Hata majirani zetu wa kaskazini mashariki wana maambukizi mengi zaidi. Afrika maambukizi mengi yako Afrika ya kusini, Afrika ya kaskazini na Aftika Magharibi. Sisi Afrika mashariki ikiwemo nchi yetu maambukizi ni kidogo sana. Lakini dunia nzima inapigia makelele nchi yetu utafikiri wana hasira fulani na sisi vile! Huwezi kuwasikia wakizungumzia nchi zenye maambukizi kwa maelfu!! Watukome!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni vigumu kujua maambukizi halisi katika nchi zinazoendelea kwa sababu nchi nyingi hazina vitendea kazi kama nchi za wenzetu.
Unakuta nchi yenye zaidi ya watu milioni 50 inategemea mashine moja yakupima virusi vya Corona.
Aidha hatuna utaratibu wakuscreen watu wetu mpaka waonyeshe dalili za maambukizi au mpaka wawekwe karantini,angalia jinsi ya nchi zizoendelea jinsi zinavyopima watu wake:
1.Marekani mpaka sasa wana maambukizi 1,509,442 na wameshapima watu 11,989157.

2.Urusi wana maambukizi 281,752 na wameshapima watu 6,916,880.

3.Hispania wana maambukizi 277,719 na wameshapima watu 3,037,840.

4.Ujerumani wana maambukizi 176,450 na wameshapima watu 3,147,771

Kwa upande wa Afrika mashariki tuko hivi:

1.Uganda wana maambukizi 227 na wameshapima watu 72,161.

2.Rwanda wana maambukizi 289 na wameshapima watu 48,239.

3.Kenya wana maambukizi 830 na wameshapima watu 36,918.

4.Sudani Kusini wana maambukizi 236 na wameshapima watu 3,356.

5.Burundi wana maambukizi 15 na wameshapima watu 284.

6.Tanzania wana maambukizi 509 na hawapima mtu yeyote asiyekuwa na dalili za Corona au kuwa kwenye karantini.

Ukilinganisha sisi na nchi zilizoendelea jinsi gani wanavyotumia uwezo wao kubaini watu walioambukizwa ni vigumu kujua uhalisia wa picha halisi ya maambukizi huku kwetu.
Kwa kadri tutakavyoweza kupima watu wengi zaidi ndivyo tutakavyopata uhakika wa maambukizi kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifo ni kifo tu!! Kwa nini hao wanne waliokufa na corona (kama ni kweli maana humu uongo mwingi sana) unawashadadia sana. Kuna watu wengi zaidi wamekufa kwa magonjwa mengine kama malaria, Cancer, TB nk mbona hao huwazungumzii? Hao sio watu? Hao hawakuumi?? Hapo tu ndipo panaposhangaza!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kama korona hakuna basi msituambie tvae barakoa wala kutakasa mikono kwa maji tiririka au "Santaiza" maana hata tukifa kwa korona sio ajabu maana malaria ,ukimwi, tb nazo zinaua!! Turudi kama awali basi toeni tamko basi msituambie tunawe mikono,waambie wizara ya afya wastop tangazo la mpoto maana hali ni shwari sasa.
 
Amealika watu wanaotaka kuhakikisha ukweli wa taarifa yake waje wajionee wenyewe!! Na amesema ndugu ndio watakuwa wanazika, kwa hiyo hakuna kificho!!
Anayepinga kwa mfano idadi ya wagonjwa waliobaki hospitali mbalimbali si aende huko hospitalini akajionee mwenyewe! Aende Amanda, mlonganzila nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngonjera za wanasiasa hizo ,sehemu zote zinalindwa na JKT na hautakiwi kurandaranda katika hayo maeneo uliyoyataja!!
 
kasemaa ana,weza ruhusu week ijayo vyuo kufunguliwa
Usipotoshe Ndugu...Hajasema hivyo...Amesema Kama Hali itaendelea kuwa hivi yaani ikiendelea kuwa nzuri atafungua vyuo na michezo...which means Kama Hali itageuka na kuwa mbaya hatafungua..
 
Kwa taarifa yako hata huko ulaya si kila mtu anapimwa kwa sasa. Ni wale walioonyesha dalili ndio wanaopimwa na wale wanaofanya kazi kwenye ofisi nyeti tu ndio hupimwa.Hata China ilikuwa haipimi kila mtu. Ila kwa sasa China ndio imeamua kumpima kila mkazi wa Wuhan. Marekani pia hawapimi kila mtu. Wanapima wenye dalili za corona tu na yule ambaye ataamua kwa hiari yake kupimwa hata kama hana dalili.
 
WKama hauamini idadi ya wagonjwa waliobaki kwenye hospitali mbalimbali si uende huko mloganzila ukajionee! haukatazwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu washajionea na kugundua genge la wanaomzunguka meko wanatuongopea,Dar kuna wagonjwa 408 wa korona ,Moro 300+,Arusha ,200+ halafu mnatuambi wapo 6 na hapo hamjafanya mass testing na pia hamjawajumlisha wale madereva wa mipakani waliokutwa na FUTA.
 
*CROSS-EXAMINATION*

(1) *Wakili:* Unakubaliana na mimi kuwa tuna maabara moja tu ya kupima virus vya Korona hapa Tanzania.

🔹 *Mheshimiwa* Ndio

(2) *Wakili:* Na unakubaliana na mimi kuwa mahabara hiyo ipo kwenye uchunguzi na hivyo haiwezi fanya kazi kwa Sasa

🔹 *Mheshimiwa* Ndio.

(3). *Wakili:* Unakubaliana na mimi pia hospitali zote pamoja na Aghakan na Regency zinaitegea maabara ya taifa kupima Virusi vya Korona.

🔹 *Mheshimiwa* Ndio.

(4). *Wakili:* Sasa mwambie mheshimiwa hakimu iliwezekana vipi Aghakan kutoa negative na muhimbili positive.

🔹 *Mheshimiwa:* Hata mimi mwenye ninashangaa imetokeaje.

(5). *Wakili:* Pia ieleze mahakama umejuaje kuwa wagonjwa wa wa Virusi vya Korona wamepungua ikiwa maabara ipo kwenye uchunguzi.

🔹 *Mheshimiwa:* Mhe. Hakimu ili swali gumu sana, ninaomba kwanza nishauriane na wataalamu wangu kabla ya kujibu swali hili.
 
Najivunia sana kuwa na Rais Shupavu na Imara kama DR. Magufuli, natembea duniani huku nikijiamini kuwa nina ongozwa na mtu Imara sana.

Kwa mara ya kwanza Imani yangu ya uzalendo Kwa nchi yangu imeongezeka mara dufu ktk kipindi hiki cha awamu hii yatano chini ya Magufuli.

Kwa mara ya kwanza nimeliombea Nchi Yangu Tanzania pamoja na Rais wetu dua maalum. haijawahi kutokea bali yote yametokana na Mtu mwema na Mwenye hofu ya Mungu kuongoza nchi yetu.
[emoji16][emoji16][emoji16] mkuu uzalendo umeongezeka
 
Watalii kutoka nchi gani??? Ni nchi IPI iliyonaakili timamu itaruhusu rain wake waje/warisk maisha Yao Tanzania.....Hivu unadhani hawajui kuwa Tz watu wanakufa kwa Corona na Data zinafichwa?????


Endeleeni kujitekenya
Ni wapii ambako watu hawafii kwa Corona? Umeambiwa na Nani kuwa data za Corona TZ zinafichwa?
 
Back
Top Bottom