Uchaguzi 2020 Rais Magufuli heshimu maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura kwenye Uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka huu

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli heshimu maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura kwenye Uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka huu

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Miongoni mwa mambo yanayowatia sana wasiwasi wananchi katika kipindi hiki ni Uchaguzi Mkuu unaotegemewa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Ingawa Rais Magufuli umetoa uhakikikisho kwa Jumuiya ya kimataifa kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na haki, lakini maneno na vitendo vya viongozi wako wakuu wa CCM, pamoja na vyombo vya dola, hayaelekei kuuona uchaguzi huo ukiwa huru na wa haki.

Nitajaribu kuelezea "indicators" zangu ninazoziona za wasiwasi wangu kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru na wa haki.

1. Nakumbuka mara tu ulipochukua madaraka ya kuongoza Taifa hili, ulipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani, hadi mwaka huu wa 2020. Lakini pamoja na kufika mwaka huu wa 2020, lakini bado Jeshi la Polisi linaendelea kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani, kama huafiki vitendo hivyo vya Jeshi la Polisi, ni kwanini hukemei vitendo hivyo vya Jeshi la Polisi nchini, ambavyo ni vya kuvunja Katiba ya nchi, ambayo inasema kuwa nchi yetu itaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi?

2. Kama kweli Mheshimiwa Rais "hubariki" uonevu huu, unaofanywa na Jeshi la Polisi nchini, dhidi ya vyama vya siasa vya upinzani, tunategemea uchukue hatua ya kuwawajibisha vyombo hivyo vya usalama wa nchi, kwa kufanya mambo kinyume cha maelekezo yako mwenyewe, ambapo ulisema kuwa vyama vya siasa vitaruhusiwa kufanya mikutano yao ya hadhara mwaka huu wa 2020, bila kubughuziwa na vyombo vya dola

3. Kumekuwa na kilio cha muda mrefu sana kutoka vyama vya siasa vya upinzani, kukutaka wewe uridhie uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi, ni kwanini unashikwa na "kigugumizi" kulikubali ombi hilo la vyama vya siasa vya upinzani, ambalo ni lenye maslahi mapana kwa Taifa hili?

4. Kumekuwa na kauli ambazo siyo njema na zinazotaka kuleta hali ya sintofahamu kwenye nchi hii, mathalani kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa chama chako cha CCM, Dkt Bashiru Ally, hivi karibuni kuwa wembe uliotumika kuwanyolea wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ndiyo huo huo utakaotumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu!

Niseme tu kitu kimoja kuwa nchi nyingi zimeingia kwenye machafuko, kutokana na viongozi wake wa chama tawala, kutotaka kuheshimu maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura. Kwa hiyo ningekusihi Mheshimiwa Rais, uepushe nchi hii, isiingie kwenye janga hilo.

Nimetoa maoni yangu kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) ambayo inampa haki kila mwananchi wa nchi hii, kutoa mawazo yake nje, kupitia chombo chochote cha habari na mawasiliano yake kutoweza ingiliwa, na chombo chochote cha dola.
 
Pole sana mkuu kama bado unaamini hayo uliyoandika hapo juu na kuendelea kuwa na matumaini nayo.

Kimsingi, ni tabia ya kila binaadam kuwa na matumaini juu ya mambo anayodhani ni mazuri kwake au kwa taifa lake; lakini kama ujuavyo 'matumaini' ni matumaini tu, hata kama hayana msingi wowote wa kuwa yatakuwepo.

Dalili zote zilizopo sasa hivi nchini ni kwamba hapatakuwepo na mabadiliko yoyote katika mpangilio wa ratiba ya uchaguzi mkuu mwaka huu.

Basi, kama ni kujiandaa, ni kujiandaa tu katika utaratibu huo uliozoeleka.

Tofauti tu iliyopo ni kwamba haijulikani kampeni za vyama vingine nje ya CCM vitaruhusiwa lini na wao kushiriki kufanya siasa zao kwa kuwahusisha wananchi.

Ukiondoa kasoro hiyo mpya, mengine yote yanaaelekea huko huko tulikokuzoea kwenye ushindi mnono wa CCM wenye uhakika kabisa, iwe ni kwa kura walizopigiwa na wananchi kwa sababu mbalimbali, au kwa kujizolea ushindi kwa njia zozote wazijuazo wao, tena bila ya aibu.

Je, kuna njia zozote zinazoweza kuimarisha "Matumaini" kama ulivyoyaelezea hapo juu katika mda huu mfupi uliosalia kabla ya kufikia uchaguzi mkuu?

Mbali ya kuwalilia wananchi wenyewe wakatae kuruhusu haki yao ya msingi, ya kuwachagua viongozi wao wenyewe, sioni namna yoyote inayoweza kuizuia CCM kutimiza malengo yake.

Hii kazi ya kuwasihi wananchi inahitaji mbinu madhubuti, na sio kazi ya kuifanya kwa mda mfupi kama huu uliobakia sasa hivi. Ni kazi ngumu na inayotaka ustahimilivu mkubwa, uongozi imara.

Ni nini nafasi ya Jumuia za kimataifa - ni ndogo sana. Uchaguzi utafanyika katika mazingira iyatakayo CCM na jumuia zitabariki tu matokeo yake.

Sana sana, labda kuwalilia SADC kwa nguvu zote; na AU. Hawa African Union kukitokea sintofahamu wanaweza kujivutavuta kidgo siku hizi, lakini sio sana.

Nimalizie kwa hili: Model ya CCM ni Museveni, Kagame. Tumekwishajulikana waTanzania hulka yetu sio tofauti na wananchi wa nchi hizo. Tu wepesi sana kuingia kwenye mstari wa matakwa ya mwenye nguvu bila ya kuhoji chochote.

Kiukweli, waTanzania ni hata zaidi ya hao waganda au warwanda kutoshtushwa na lolote linalotokea nchini mwao.

Akina Mwinyi, Mkapa, Kikwete watakuwa wanashangaa sana kwa nini hili wao hawakuliona mapema kama alivyoliona huyu wa sasa!
 
Nchi imeshakuwa mali yake sisi wananchi ndio tunatakiwa kuheshimu maamuzi yake.
Ni Imani potofu Mkuu jabulani

Kwa kuwa kiongozi yeyote, amepewa dhamana na wananchi na siyo sisi wananchi tunaopaswa kutii matakwa yake.
 
Bila ya kuwa na tume ya uchaguzi iliyo neutral uchaguzi unaousemea ni ndoto,vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi yake kikatiba sio kuwa vinalinda chama dola ,AU na SADC ni coffee/tea clubs achana nazo na hazina la kusaidia,yaliyotokea hapo Malawi,Kenya,ni raia ndio wameleta mabadiliko hayo,sisi tuendelee kuwa mashujaa wa kulalamika kwenye key boards,mabadiliko yanahitaji jasho la damu.
 
Ni Imani potofu Mkuu jabulani

Kwa kuwa kiongozi yeyote, amepewa dhamana na wananchi na siyo sisi wananchi tunaopaswa kutii matakwa yake.

Mkuu kwenye bandiko lako namba moja, Tatizo la haya yote unayoyaona na yanayofanyika ni huyo Magufuli mwenyewe na hatayabadilika mpaka aidha yatokee machafuko au atoke madarakani. Magufuli hawezi ushindani wa kisiasa, na hatakaa aweze, hivyo ataendelea kufanya atakavyo kwani hata hiyo katiba kwake haina tofauti na gazeti la udaku.
 
OTE="tindo, post: 34546423, member: 55693"]
Mkuu kwenye bandiko lako namba moja, Tatizo la haya yote unayoyaona na yanayofanyika ni huyo Magufuli mwenyewe na hatayabadilika mpaka aidha yatokee machafuko au atoke madarakani.

Magufuli hawezi ushindani wa kisiasa, na hatakaa aweze, hivyo ataendelea kufanya atakavyo kwani hata hiyo katiba kwake haina tofauti na gazeti la udaku.
[/QUOTE]
Mkuu tindo umenichekesha sana, hapo uliposema kuwa Magu anachukulia Katiba ya nchi kama gazeti la udaku😀😀
 
Mkuu kwenye bandiko lako namba moja, Tatizo la haya yote unayoyaona na yanayofanyika ni huyo Magufuli mwenyewe na hatayabadilika mpaka aidha yatokee machafuko au atoke madarakani. Magufuli hawezi ushindani wa kisiasa, na hatakaa aweze, hivyo ataendelea kufanya atakavyo kwani hata hiyo katiba kwake haina tofauti na gazeti la udaku.
Mvua zimekuwa nyingi msimu huu mkuu tindo, mazao kule shambani kweli yataleta tija msimu huu?

Kile kimya cha mda mrefu kilitia wasiwasi kidogo, hasa kutokana na hali halisi iliyopo .
 
Navyojua mimi nchi kukabidhiwa dhidi ya vipande vya karatasi mnavyoita ballots au kura haijawahi kutokea at least Africa. Ni zaidi ya vipande vya karatasi ikiwa demokrasia haipo. Wafuatiliaji wengi wa masuala ya chaguzi duniani wanajua hili. Inahitaji sense of moral and dogma kuweza kumwachia mtu nchi.

Hivi tu ndani ya chama tawala inakuwa ngumu ndani ya chama kupeana vijiti hadi ijengwe hii sense of moral and dogma na ikishindikana ifanyike brainwashing kwa wagombea na ndipo vumbi litulie iwe dhidi ya upinzani?

Tuangalie Nyerere hadi IMF walipoingilia kati, Mwinyi hakuwa na shida ila Nyerere hadi apofanya mambo Mkapa sina rekodi ila alijitahidi Sumaye ashinde nadhani kura hazikutosha, JK mnakumbuka majina kukatwa na kura kurudiwa nk. Yaani ni shida! Si rahisi sasa CCM kuwapa upinzani against eti vikaratasi. Sioni huo utashi. Patachimbika na wacha pachimbike. Haya ni mawazo yangu!
 
Mvua zimekuwa nyingi msimu huu mkuu tindo, mazao kule shambani kweli yataleta tija msimu huu?

Kile kimya cha mda mrefu kilitia wasiwasi kidogo, hasa kutokana na hali halisi iliyopo .

Upande wa kilimo niko sawa.
 
Navyojua mimi nchi kukabidhiwa dhidi ya vipande vya karatasi mnavyoita ballots au kura haijawahi kutokea at least Africa. Ni zaidi ya vipande vya karatasi ikiwa demokrasia haipo. Wafuatiliaji wengi wa masuala ya chaguzi duniani wanajua hili. Inahitaji sense of moral and dogma kuweza kumwachia mtu nchi. Hivi tu ndani ya chama tawala inakuwa ngumu ndani ya chama kupeana vijiti hadi ijengwe hii sense of moral and dogma na ikishindikana ifanyike brainwashing kwa wagombea na ndipo vumbi litulie iwe dhidi ya upinzani? Tuangalie Nyerere hadi IMF walipoingilia kati, Mwinyi hakuwa na shida ila Nyerere hadi apofanya mambo Mkapa sina rekodi ila alijitahidi Sumaye ashinde nadhani kura hazikutosha, JK mnakumbuka majina kukatwa na kura kurudiwa nk. Yaani ni shida! Si rahisi sasa CCM kuwapa upinzani against eti vikaratasi. Sioni huo utashi. Patachimbika na wacha pachimbike. Haya ni mawazo yangu!
Umeyakoroga sana, hadi haijulikani kichwa na mkia viko wapi!
"...moral na dogma..."; mara, "vipande vya karatasi..." kutowahi kutumika kukabidhi nchi? Kibaki hapa Kenya, ulikuwa hujazaliwa? Botswana, Angola, Afrika Kusini, haziko Afrika?

"Sense of moral and dogma", mbona unaitumia kama silaha? Hii inapatikana wapi, inauzwa madukani nasi tukainunue?

Mkuu Mshiriri, ujue nimejitahidi sana sana kukuelewa, lakini nadhani 'moral na dogma' sina!
 
Miongoni mwa mambo yanayowatia sana wasiwasi wananchi katika kipindi hiki ni Uchaguzi Mkuu unaotegemewa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Ingawa Rais Magufuli umetoa uhakikikisho kwa Jumuiya ya kimataifa kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na haki, lakini maneno na vitendo vya viongozi wako wakuu wa CCM, pamoja na vyombo vya dola, hayaelekei kuuona uchaguzi huo ukiwa huru na wa haki.

Nitajaribu kuelezea "indicators" zangu ninazoziona za wasiwasi wangu kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru na wa haki.

1. Nakumbuka mara tu ulipochukua madaraka ya kuongoza Taifa hili, ulipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani, hadi mwaka huu wa 2020. Lakini pamoja na kufika mwaka huu wa 2020, lakini bado Jeshi la Polisi linaendelea kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani, kama huafiki vitendo hivyo vya Jeshi la Polisi, ni kwanini hukemei vitendo hivyo vya Jeshi la Polisi nchini, ambavyo ni vya kuvunja Katiba ya nchi, ambayo inasema kuwa nchi yetu itaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi?

2. Kama kweli Mheshimiwa Rais "hubariki" uonevu huu, unaofanywa na Jeshi la Polisi nchini, dhidi ya vyama vya siasa vya upinzani, tunategemea uchukue hatua ya kuwawajibisha vyombo hivyo vya usalama wa nchi, kwa kufanya mambo kinyume cha maelekezo yako mwenyewe, ambapo ulisema kuwa vyama vya siasa vitaruhusiwa kufanya mikutano yao ya hadhara mwaka huu wa 2020, bila kubughuziwa na vyombo vya dola

3. Kumekuwa na kilio cha muda mrefu sana kutoka vyama vya siasa vya upinzani, kukutaka wewe uridhie uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi, ni kwanini unashikwa na "kigugumizi" kulikubali ombi hilo la vyama vya siasa vya upinzani, ambalo ni lenye maslahi mapana kwa Taifa hili?

4. Kumekuwa na kauli ambazo siyo njema na zinazotaka kuleta hali ya sintofahamu kwenye nchi hii, mathalani kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa chama chako cha CCM, Dkt Bashiru Ally, hivi karibuni kuwa wembe uliotumika kuwanyolea wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ndiyo huo huo utakaotumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu!

Niseme tu kitu kimoja kuwa nchi nyingi zimeingia kwenye machafuko, kutokana na viongozi wake wa chama tawala, kutotaka kuheshimu maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura. Kwa hiyo ningekusihi Mheshimiwa Rais, uepushe nchi hii, isiingie kwenye janga hilo.

Nimetoa maoni yangu kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) ambayo inampa haki kila mwananchi wa nchi hii, kutoa mawazo yake nje, kupitia chombo chochote cha habari na mawasiliano yake kutoweza ingiliwa, na chombo chochote cha dola.
Vigezo vya uchaguzi huru na wa haki vinajulikana ambavyo ni pamoja na tume huru ya uchaguzi.
Kwahiyo dunia itajua kama tukio la November litakidhi vigezo hivyo au la.
CCM hawawezi kukubali tume huru ya uchaguzi, lakini hawawezi kusema uchaguzi hautakuwa huru.

Arbitrariness
Ambiguity
Capriciousness
Modus operandi ya CCM!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeyakoroga sana, hadi haijulikani kichwa na mkia viko wapi!
"...moral na dogma..."; mara, "vipande vya karatasi..." kutowahi kutumika kukabidhi nchi? Kibaki hapa Kenya, ulikuwa hujazaliwa? Botswana, Angola, Afrika Kusini, haziko Afrika?

"Sense of moral and dogma", mbona unaitumia kama silaha? Hii inapatikana wapi, inauzwa madukani nasi tukainunue?

Mkuu Mshiriri, ujue nimejitahidi sana sana kukuelewa, lakini nadhani 'moral na dogma' sina!
Nimekushangaa sana ikiwa nawe ni great thinker kwa kuishia kutaja nchi zenye demokrasia kidogo ku-justify mtiririko wangu. Usihemke mkuu, fikiri na kuwa huru tu.
 
[emoji51][emoji51][emoji51]
Screenshot_20200303-141241-picsay.jpeg
 
Nimekushangaa sana ikiwa nawe ni great thinker kwa kuishia kutaja nchi zenye demokrasia kidogo ku-justify mtiririko wangu. Usihemke mkuu, fikiri na kuwa huru tu.
Eeenh, yaani 'mkorogo' ulioubandika kwenye 'post' ile unataka nao uonekane kuwa ni 'fikra pevu' za kuwafikirisha watu?
 
Eeenh, yaani 'mkorogo' ulioubandika kwenye 'post' ile unataka nao uonekane kuwa ni 'fikra pevu' za kuwafikirisha watu?
Subiri basi kukabidhiwa nchi kwa vipande vya karatasi
 
Subiri basi kukabidhiwa nchi kwa vipande vya karatasi
Ni wapi nilipoandika nasubiri, au yeyote au chama chochote "kukabidhiwa nchi kwa vipande vya karatasi," kama sio mawazo yako mwenyewe.
 
Back
Top Bottom