Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Miongoni mwa mambo yanayowatia sana wasiwasi wananchi katika kipindi hiki ni Uchaguzi Mkuu unaotegemewa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Ingawa Rais Magufuli umetoa uhakikikisho kwa Jumuiya ya kimataifa kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na haki, lakini maneno na vitendo vya viongozi wako wakuu wa CCM, pamoja na vyombo vya dola, hayaelekei kuuona uchaguzi huo ukiwa huru na wa haki.
Nitajaribu kuelezea "indicators" zangu ninazoziona za wasiwasi wangu kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru na wa haki.
1. Nakumbuka mara tu ulipochukua madaraka ya kuongoza Taifa hili, ulipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani, hadi mwaka huu wa 2020. Lakini pamoja na kufika mwaka huu wa 2020, lakini bado Jeshi la Polisi linaendelea kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani, kama huafiki vitendo hivyo vya Jeshi la Polisi, ni kwanini hukemei vitendo hivyo vya Jeshi la Polisi nchini, ambavyo ni vya kuvunja Katiba ya nchi, ambayo inasema kuwa nchi yetu itaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi?
2. Kama kweli Mheshimiwa Rais "hubariki" uonevu huu, unaofanywa na Jeshi la Polisi nchini, dhidi ya vyama vya siasa vya upinzani, tunategemea uchukue hatua ya kuwawajibisha vyombo hivyo vya usalama wa nchi, kwa kufanya mambo kinyume cha maelekezo yako mwenyewe, ambapo ulisema kuwa vyama vya siasa vitaruhusiwa kufanya mikutano yao ya hadhara mwaka huu wa 2020, bila kubughuziwa na vyombo vya dola
3. Kumekuwa na kilio cha muda mrefu sana kutoka vyama vya siasa vya upinzani, kukutaka wewe uridhie uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi, ni kwanini unashikwa na "kigugumizi" kulikubali ombi hilo la vyama vya siasa vya upinzani, ambalo ni lenye maslahi mapana kwa Taifa hili?
4. Kumekuwa na kauli ambazo siyo njema na zinazotaka kuleta hali ya sintofahamu kwenye nchi hii, mathalani kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa chama chako cha CCM, Dkt Bashiru Ally, hivi karibuni kuwa wembe uliotumika kuwanyolea wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ndiyo huo huo utakaotumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu!
Niseme tu kitu kimoja kuwa nchi nyingi zimeingia kwenye machafuko, kutokana na viongozi wake wa chama tawala, kutotaka kuheshimu maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura. Kwa hiyo ningekusihi Mheshimiwa Rais, uepushe nchi hii, isiingie kwenye janga hilo.
Nimetoa maoni yangu kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) ambayo inampa haki kila mwananchi wa nchi hii, kutoa mawazo yake nje, kupitia chombo chochote cha habari na mawasiliano yake kutoweza ingiliwa, na chombo chochote cha dola.